Wapenzi wa Wayback tukutane hapa

Able man

Senior Member
Nov 22, 2020
132
174
Tupia wimbo wowote ulioimbwa miaka hiyo unaoukubali.

Ukiwa na maelezo ya wimbo husika (mfano Kwa nini uliimbwa,msanii au wasanii na mwaka uliombwa) itakuwa njema Sana.

Lakini pia unakukumbusha nini wewe!

Naanza na hii...

Dionne Warwick anafanya cover ya That what friends are for mwaka 1985 akiwa na Elton John, Stevie Wonder na Gladys Knight.

Wimbo ulikuwa Kwa ajili ya kusaidia kukusanya fedha za utafiti na kinga dhidi ya UKIMWI. Ulifanya vizuri Sana mwaka uliofuata na kufanikiwa kingiza kiasi cha $3 million.
 
Mwaka 2015 capten John komba alifanya wimbo MBELEMBELE ukiwa na lengo la kuhamassisha mambo ya KAMPENI flan amaizing za kisiasa

Wimbo huo uliuza kopi kibao na kila ulikopigwa ulikuwa UNASIKILIZWA BILA KUPINGWA
 
Hahahaaa!
 
Whitney Houston hapa na I Will always love you...

Wimbo ulitungwa na kurekodiwa Kwa mara ya kwanza na Dolly Parton 1973.

1992 Whitney Houston anaurekodi kama sound track ya movie ya The Bodyguard aliyocheza pia.
 
Jamani huyu Whitney Alikuwa kiboko...anakushawishi uendelee kumsikiliza tuu

Binafsi ni mdau wa nyimbo zenye utulivu kama hizi. So ninaposikiliza hivi kwangu burudaaani kabisa
 
Muziki ulikuwa zamani aisee,kwasasa ni makopo kopo tu!! Ukija huku unaburudishwa na Shania Twain - You are still the one ,ukienda huku kuna Luther vandros maricah carey - endless luv ,ukienda huku una boy 2 men ,ukirudi huku unapata flavor za wako jako ,ukirudi nyuma unawakuta dru hill - i should be ,ukienda kule unakutana na kina julio glesias ,ukienda mbele kuna ,swv,ukienda kushoto kuna spice girls,ukienda kulia unakutana na britney spears luck,ukija juu unakutana na kci and jojo -tell me its real,ukija kati s club 7- 2 in a millioni ,spice girls-2 became 1...yaani sisi ndio tumeenyoj muziki aiseeeee! Yaani unakuta HDD disk umejaza mp3 zaidi ya elfu 10.

Ben E King,Jerry Leiber na Mike Stroller wanaandika Stand By Me 1960 na Ben anauimba na kuurelease 1961.

Ulisikilizwa saana mwaka huo na 1986 ulipotumika kama sound track ya movie ya Stand By Me aliyocheza pia Ben E King.

Zimerekodiwa versions zaidi ya 400 za Stand By Me na wasanii mbalimbali wakiwemo John Lennon, Cassius Clay (Muhammad Ali) na wengineo kibao.
Timu ya Melbourne city ya Australia kwa mfano huuimba wimbo huu kila wanapocheza Uwanja wa nyumbani kabla ya mechi kuanza. Wakati huo washabiki huinua skafu zao juu na kuimba wimbo Kwa nguvu!

Stand By Me
 
Muziki ulikuwa zamani aisee,kwasasa ni makopo kopo tu!! Ukija huku unaburudishwa na Shania Twain - You are still the one ,ukienda huku kuna Luther vandros maricah carey - endless luv ,ukienda huku una boy 2 men ,ukirudi huku unapata flavor za wako jako ,ukirudi nyuma unawakuta dru hill - i should be ,ukienda kule unakutana na kina julio glesias ,ukienda mbele kuna ,swv,ukienda kushoto kuna spice girls,ukienda kulia unakutana na britney spears luck,ukija juu unakutana na kci and jojo -tell me its real,ukija kati s club 7- 2 in a millioni ,spice girls-2 became 1...yaani sisi ndio tumeenyoj muziki aiseeeee! Yaani unakuta HDD disk umejaza mp3 zaidi ya elfu 10.

Bado hapo hujamgusia Michael Jackson na liberian girl wala boyz to men, kuna watu walikuwa wanaitwa Next... kwanza wazuri halafu sauti zao ni shiida, naona nisiendelee sana nisije nikaanza kuwakumbuka akina Tevin Campbel, christina augulera shakira na siwezi kuacha kuwataja nsync na this i promise you maana post haitakamilika
 
Haswaaaa yaani umetaja wanamuziki KONKI Next kina RL Too close ,Kina Tevin campbel -can we talk ,acha tu watoto wadogo kwasasa tunawahurumia na makopo kopo yao,kwenye vibanda umiza zamani tunapata mipini ya Nu shooz ,kina black box ,music factory huku tukisubiri ANODI ya JINI au ANODI YA JENI au RAMBO na KINA CHECK NORIS.
 
Bado hapo hujamgusia Michael Jackson na liberian girl wala boyz to men, kuna watu walikuwa wanaitwa Next... kwanza wazuri halafu sauti zao ni shiida, naona nisiendelee sana nisije nikaanza kuwakumbuka akina Tevin Campbel, christina augulera shakira na siwezi kuacha kuwataja nsync na this i promise you maana post haitakamilika
Watu walofaidi mziki bana na hisia za ndani kimziki hawawezi kuzificha hata iweje!
 
1608832444462.png
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom