Wapenzi wa dini tofauti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapenzi wa dini tofauti

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ilonza, Mar 11, 2011.

 1. I

  Ilonza Senior Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi ni kijana mkatoliki mwenye miaka 24 nina soma chuo mwaka wa tatu,mpenzi wangu ni muislamu anaelimu ya kidato cha nne kwa sasa anaishi na wazazi wake, mausiano yetu ni takribani miaka 2, ktk mazungumzo yetu ananitaka nibadili dini,ila mimi sijalizungumzia hilo kwasababu wazazi wetu wote hatujawafahamisha ila tuna mpango.kubadili dini siwezi na mpenzi wangu siwezi kumuacha,nina pata utata sana, hata sijui nifanyeje ndg zangu?
   
 2. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mapenzi ni commitments...time will tell!
   
 3. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu soma kwanza umalize,alafu usipende sana kujilegeza kwake wewe mkazanie tu abadili sio wewe ubadili,wewe ndio mtoto wa kiume bana..ila kwa upande mwingine unaweza kubadili tu wala haina tatizo....la sivyo muishi pamoja ila kila mtu na dini yake...
   
 4. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  my dear mambo kama hayo yapo mengi tu
  inategemea ni jinsi gani weye una respond back..
  kuna wengine mchumba mzungu, mwarabu , mwafrica n.k.....
  kuna wengine wazazi hawawataki watoto wao waolewe na fulani ..
  kwa hiyo ni mambo ya kawaida tu ..

  ushauri wangu kwako my dear ni muhimi kwako
  kuwa mwanaume na wewe ndo utakuwa baba wa nyumba
  kwa hiyo kama kawaida yeye abadili dini ..

  lakini kama hiyo ni ngumu na unampenda kupita kiasi ..
  chukua ushauri wa Papizo my dear kila mtu aishi na dini yake..
  ila fikiria sana kuhusu hilo sababu baadaye mkipata watoto
  ya weza leta matatizo...
   
 5. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Yap mwanamke ndio siku zote wa kubadilisha dini na sio mwanaume ndio abadili bana....la sivyo bora kukaa na kila mtu dini yake ila kama ulivyosema inaweza kuja kuwa problem kwa watoto kwa kukulia mazingira ya wazazi wasiokuwa na dini moja ya msimamo..
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Nenda kafunge ndoa kwa mkuu wa mkoa mambo yaishe
   
 7. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,157
  Likes Received: 1,889
  Trophy Points: 280
  Mwanangu fuata ushauri huu:
  Kwa mujibu wa Ukristo baba ni kichwa cha nyumba.
  Kwa mujibu wa Uislamu mwanamke hana dini kwa maana bwana akiuza bange au gongo mwanamke naye ni mdau.
  Hivyo basi usibadili dini abaadan kwa shinikizo la mapenzi utachekwa na ndoa yako itakosa amani hadi kizazi chako, kesho watakwambia sharti lingine gumu zaidi.
  Mueleze ukweli tupu huyo msichana kwamba hutabadili dini kwa shinikizo la wazazi wako sio nitakao ishi nao.
  Kama hataki hakupendi bali anapenda wazazi wake.
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Msichana wa kikristu akiolewa anabadilisha dini
  Msichana wa kiislam akiolewa anabadilisha dini pia
  Lakini my dear hii 21st century
  Sijui inatupeleka wapi...
  Ndoa siku hizo ni biashara
  aumikataba
  Wachache sana wana oana ajili
  Ya upendo wa kweli...
  sasa hivi kubadili jina la mwisho
  au dini ni mjadala. .
  na wakati enzi za bibi zetu
  ulikuwa wajibu. ...
   
 9. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Dini inanafasi kubwa sana katika maisha yetu, fanya maamuzi ya busara, usije ukajuta kwa maamuzi utakayo fanya, uweresponsible na tayari kwa yote. Fikiria kwa upana zaidi. Kwanza Watoto utakao wazaa watahitaji mwongozo wenu na kuiga kutoka kwenu/kwako, pili fikiria wazazi na ndugu zako. Ndoa ni watu wawili lakini maisha baada ya ndoa ni zaidi ya hapo. Mke na mume ni kama kitasa cha mlango, kitasa ndicho hasa huwahakikishia amani na usalama ya walio ndani. Kuwa na huyo mpenzi miaka miwili sio ishu, watu wana miaka sita lakini wanapigana chini.
   
 10. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mmhhhh!!! utaweza kuswali sala 5??? naona kama huyo binti anatamani ndoa zaidi, ndio kwanza kidato cha 4 aahh!! kashaanza kusema ww ubadili dini yeye hatabadili, anza kuwa mwangalifu kuna nafasi kubwa ya ww kuwa kama busheke ati!!!

  his nizangu hisia tu lkn!!
   
 11. s

  shosti JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Dana umeongea la maana kabisa wakafunge kwa mkuu wa mkoa,watoto wakikua watachagua dini zao,maangu muislamu babangu mkristo watoto tumechagua dini zetu kuna waislamu,wakristo na wapagani humohumo,ila bint mbona bado anasafari ndefu sana mnaanza kuongelea ndoa.furahieni mapenzi kwanza kamba inaweza katika mbele ya safari hiyo.....:lol:
   
 12. G

  Gathii Senior Member

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu,
  suala lako ni moja ya masuala ambayo siku zote huwa yanasumbua sana vichwa vya watu.Lakini kitu kikubwa na cha msingi ni kuwa imani yako kwa dini yako i kubwa kiasi gani?unachukuliaje dini/imani yako?ni kitu cha hapa tu duniani au kina nafasi hata baada ya maisha haya?hiyo ndiyo itakuwa nguzo ya kuegemea na dira itakayokuongoza katika kufanya uamuzi wako,kaa chini tafakari.
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  it is a time bomb, tuwe wakweli, situation ya tanzania sasa hivi, masuala ya udini yako seriasi sana ndani ya mioyo ya watu. kuna familia nyingi sana ambazo zina migogoro kwa sababu vijana wao wameoa au kutaka kuoa watu wa dini tofauti na zao. Familia ya kiislamu na nadra sana imruhusu binti yao kuolewa na mkristo and vice versa.

  My Take: Kijana soma, take/leave with time. You will see the result kama mpango wa Mungu muoane mtaoana la sivyo hamtaoana, waulize jamaa(ndugu zako) zako uone maoni yao (japo ndoa ni jambo la wtau wawili), ndipo utaona moto wake kisha pima wewe mwenyewe.
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  naomba source ya hii information.
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Siku zote mtu anayebadili dini kwa sababu ya mtu huwa namuona ni mtu aliyekosa msimamo.
  Leo akikubwaga utabadili tena urudi ulipotoka?
  Hakika utajuta sana.
  Simshauri yeyote kati yenu abadili dini.
   
 16. s

  shosti JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  umenena vyema mamito,mapenzi yakishaisha yakabaki mazoea utajuuuuta kwa uamuzi uliofanya....
   
 17. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  ushauri wenu ni wa manufaa makubwa sana kwangu mimi,maake yamenikuta na sasa nimechukua uamuzi wa kuudhi na kufedhehesha upande mmoja,....wacha niishie hapo....thanx alot all commentant.
   
 18. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Baki na dini yako bana, mwanaume atabaki kuwa mwanaume, mwanamke labda abadili. au kila mtu abaki na dini yake. embu leo ubadili dini, dini nyingine ni ngumu mpaka uweze kusali na huo uutu uzima hesabu miaka kama kumi hivi.
   
 19. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Dogo simama imara katika iman yako. Waisilam wanafurahi sana mkristu anapobadili dini na kujiunga na wao, usikubali kumkana kristu na kumfuata shetan. Kuwa imara na kumfia kristo, mwambie abadili dini. Ndoa ya mseto sikushauri kwan mara nying zimekuwa na matatizo sana hasa kwenye malezi ya watoto. Kumbuka mwanamke atawaacha wazazi wake na kuambatana na mumewe nao si wawili tena bali ni mwili mmoja. Tumsifu Yesu Kristo.
   
 20. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  kaka mm ninakushaur uachane nae kwasababu kama yeye amekataa kubadili din na wewe umekataa kubadil din. Kinachofuata ni kwamba mmoja akaja kufanikiwa kumshaur mwenzie kubadil din mkaja kuoana kitakapo tokea tatizo ndan ya ndoa ki2 cha kwanza kila m2 atarud kwny din yake ya awal na hapo ndipo mambo yatakuwa magumu zaid na tatzo zaid. Ninamaana kuwa din haina tofaut na kabila kama spirit umewekewa hvyo utaendelea kuwa nayo mpaka uzeen kaka jaribu kufikiria mara mbili mbili kama upo tayar kuja kugawa watoto wenye majina matatu matatu kuwa makin. Kaz kwako ushaur wangu ni huo kaka jaribu kufikiria
   
Loading...