Wapenda ugali mpo?

Napenda sana ugar nile na samaki,dagaa au mlenda
Dagaa wa Kigoma wakaangwe na pilipili mbuzi nyanya mshumaa nyanya chungu na kitunguu bila kusahau ndimu kidogo
 
Ugari una mboga zake, siyo ugari nyama au maharage, ugari mboga zake kama samaki wa kukaanga, nyama choma, mlenda sijui bamia ya kuchanganyikiwa na biringanya nyanya changu daaah, au ugari makange ya kuku au ya mbuzi
Maharage lililokolea nazi na samaki wa kukaanga pembeni pamoja na mboga za majani
 
Ushi kula ugali wa nazi ww....tuulizeni wa tanga....ugali chakula cha taifa...tunatofautiana mboga na wale wa masaki
 


Ugale nakulaga nikiumwa
 
mbona sijaona mtu akizungumzia ugali wa mtama unaoliwa kule kwetu kanda maalumu?
 
Wacha kabisa hakunaga kama ugali Mimi hata mwenz nakula niwekee tu mboga ya majani pembeni samaki,dagaa,au nyama..
 
mbona sijaona mtu akizungumzia ugali wa mtama unaoliwa kule kwetu kanda maalumu?
Ha ha haaaa, nilishukiaga pale Bweli stand, Musoma town nikamkuta dada wa kikurya anakamua ugali wa mtama na kichuri ndo nikajua "Sasa umeingia kanda ya wababe "
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…