Wapambanaji wenzangu, Ungewezaje kui-handle hali hii?

Wapambanaji wenzangu, Ungewezaje kui-handle hali hii?

Yofav

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
4,331
Reaction score
7,955
Habari yenu wakuu,

Huu uzi kama unavyojieleza hapo ni kwaajili ya wapambanaji wenzangu katika maisha, hivi katika hali ya kawaida upo kwenye 20-30yrs and still maisha hujayapatia kivile kwa kuwa una uwezo wa kujilisha wewe pekee yako hivyo basi hauna mke wala mtoto kwa wakati huo, Ila unakuta una wazazi ambao uliwaacha mji mwingine na wewe upo mji mwingine unatafuta.

aba aliachana na Mama hivyo pia hawaishi pamoja ila wewe kama mtoto still unawasiliana na wote normal pia kuna wakati kila mmoja anakulilia shida yake na unajaribu kutatua bila shida ila sasa inafika sehemu unatafakari maisha yako kiujumla kila ukicheki kesho yako unaona ina kipengele (Kama vile haina uhakika sana) Na ni heri basi ungekuta una elimu unayoitegemea kwa kiasi fulani lakini pia hauna elimu yoyote unaishi tu kiujanjaujanja na Msaada wa Mungu tu.

Ni heri ungekuwa una-focus kujiwazia kesho yako pekee lakini sivyo kwani unawaza Kesho yako pamoja na ya wazazi wako pia kwani umri unakwenda na huko mbele wao watahitaji msaada wako zaidi ya sasa. Mbaya zaidi wazazi washajenga ile mentality kwamba unapaswa uwasaidie shida zao kuanzia muda huu, Mama ni 38yrs na Baba 48yrs.

Ebu tushauriane hapa wakuu nawezaje ku-handle hii hali na niwe na future poa huko mbele maana sina mke wala mtoto ila pia mbele napaswa kuwa nao, Na pia mbele hukohuko napaswa pia kuwasaidia wazazi kwani wanaonesha kabisa huko mbele nina kazi kubwa sana kuliko hata sasa japo hata sasa nishaanza kulemewa, Kuna wakati nakula nikiwa na mawazo kwamba pengine nakula lakini wazazi wangu hawali huko walipo, Nashindwa kuwa huru kufurahia maisha kwa kuwa naona pengine nafurahi na wazazi wangu hawafurahi

Note: Sinywi pombe, Sio mtu wa mbususu (Single✅), Hunikuti viwanja na yote hiyo ni kwa kuwa sina hela ya kukidhi vyote hivyo, Ao starehe yangu kubwa naweza kusema ni kula.

Kama upo kwenye situation hii niambie unawezaje kui-handle na hata kama una ushauri nini nifanye ili niende sawa na niweze kuifurahia kesho yangu.

Karibu sana kwa maoni na ushauri wako.
 
Ila bongo kutoboa ni changamoto sana.

Maana kijana kabla hujaanza maisha yako unakuwa na majukumu tayari umeshabebeshwa. Yaani unaanza na negative.

Yaani kila kitu kinaenda kinyume nyume

Baba anamtegemea mtoto badala ya mtoto kumtegemea baba.

Kina Mo dewji wanawategemea baba zao Ila kina sisi tunategemewa na baba zetu
 
Kwanza pole sana.

Naelewa sana unachopitia but kuwa honesty na nafsi yako.

Kwa umri huo Baba na Mama wanaweza kabisa kujishughulisha na chochote,bora uwape hata mtaji wa 50,000/= mwingine auze matunda mwingine aangalie fursa zilizopo (watashauri wadau wengine).
Wafanye kazi waweze kujitegemea.

Watakutegemea mpaka lini?Hakuna mwanadamu ataeishi milele,wajifunze kumtegemea Mungu na kufanya kazi kwa bidii ukiwaendekeza utapata magonjwa yasiyoambukiza Kwa stress.

Me naona wanaostahili msaada Ni watoto na wazee kabisa 60+ wengine tufanye kazi.
 
Hapo umri wa wazazi umetupiga bro!

Ukweli maisha ni magumu sana wakati unapo anza , tena ikiwa unaanza na hauna msingi, iwe wa elimu au mtaji.
Brother ni changamoto haswa, mpaka unakosa nuru!

Lakini ni kwa wakati tuu, sote au wengi wetu tulikuwa kama wewe na kuzidi lakini hatukukata tamaa moja kwa moja japo kwa kiasi tulikata tamaa, lakini tulikaza na leo hii hata kama si kwa kiwango kile cha matarajio lakini kuna uafadhali.

Weka nia, ongeza juhudi, tafuta maarifa, kuwa na nidhamu kwa kila kitu, kuwa na malengo ya muda mrefu hata yawe madogo lakini yakitimia hutua moyo sana.

Mungu akuwezeshe ndugu yangu.
 
Wazazi wana shughuli zozote za kujipatia kipato?
If yes then jiangalie wewe zaidi sababu kwa huo umri wao naona bado wanajiweza.
Wasaidie pale unapoweza ila usijisahau kujiwekea akiba.
mom ni fighter at least ila mzee ndo amegive up na yupo kijijini tu
 
Kwanza pole sana.

Naelewa sana unachopitia but kuwa honesty na nafsi yako.

Kwa umri huo Baba na Mama wanaweza kabisa kujishughulisha na chochote,bora uwape hata mtaji wa 50,000/= mwingine auze matunda mwingine aangalie fursa zilizopo (watashauri wadau wengine).
Wafanye kazi waweze kujitegemea.

Watakutegemea mpaka lini?Hakuna mwanadamu ataeishi milele,wajifunze kumtegemea Mungu na kufanya kazi kwa bidii ukiwaendekeza utapata magonjwa yasiyoambukiza Kwa stress.

Me naona wanaostahili msaada Ni watoto na wazee kabisa 60+ wengine tufanye kazi.
🙏
 
Hapo umri wa wazazi umetupiga bro!

Ukweli maisha ni magumu sana wakati unapo anza , tena ikiwa unaanza na hauna msingi, iwe wa elimu au mtaji.
Brother ni changamoto haswa, mpaka unakosa nuru!

Lakini ni kwa wakati tuu, sote au wengi wetu tulikuwa kama wewe na kuzidi lakini hatukukata tamaa moja kwa moja japo kwa kiasi tulikata tamaa, lakini tulikaza na leo hii hata kama si kwa kiwango kile cha matarajio lakini kuna uafadhali.

Weka nia, ongeza juhudi, tafuta maarifa, kuwa na nidhamu kwa kila kitu, kuwa na malengo ya muda mrefu hata yawe madogo lakini yakitimia hutua moyo sana.

Mungu akuwezeshe ndugu yangu.
shkran mkuu
 
mom ni fihter at least ila mzee ndo amegive up na yupo kijijini tu
Ni kwa sababu wewe upo na hivyo wametengana basi kila mmoja anataka akutumie vizuri
Amka kijana, ni wazazi ndio ila kuna mambo ukiendekeza hutafanikiwa mwishowe utawaona mzigo na kuchukia wazazi.
Mwambie mzee ajishughulishe ili wakupunguzie mzigo maana hadi umelalamika means ni umelemewa
 
Kipengele huwa kipo tena unakuta mzee kaenda tena kuoa mwanamke mwenye watoto afu mzee wako anakua anakupigia simu uwahudumie hao watoto wa huyo mama kwa madai ni wadogo zako mimi nevaa nilikataa ni heri lawama[emoji112]
Kama uchumi upo vizuri wasaidie tu mkuu.
 
Back
Top Bottom