Wapambanaji wengine Serikali inawasahau

made

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
890
581
Hii nchi Ina viongozi wengi wameipambania sana hadi hapa ilipo lakini naona kama Serikali imeamua kuwasahau kabisa, mfano Mwl Nyerere jina lake limetumika kwenye taasisi na miundombinu mbalimbali mikubwa hapa nchini.

Kuna chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere lakini hiyo haikutosha Chuo Kikuu Cha Kilimo kule Butiama, Bwawa la Mwl Nyerere, Mwl Nyerere National Park, Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre.

Leo hii hakuna chuo au miundombinu mikubwa au taasisi zenye jina la Rashid Mfaume Kawawa ukiachana na barabara na shule za msingi na sekondari kama zipo ziwekeni hapa nasi tuzifahamu.

Ifike wakati viongozi wetu wa sasa muwakumbuke wazee wengine waliyoipigania hii nchi.

Mzee Kawawa ndio Waziri Mkuu wa pili baada ya Mwl Nyerere na aliwahi kuongoza nchi zaidi ya mwaka baada ya Mwl Nyerere kujiuzulu Uwaziri Mkuu na hata pale Mwl Nyerere aliporudi kama Rais bado Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wake wa kwanza.

Pia Mzee Kawawa aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Tanu. Rai yangu kwenu viongozi likumbukeni jina la Mzee Kawawa katika miradi mikubwa au taasisi kubwa hapa nchini Ili aendelee kukumbukwa kwenye historia ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom