Black Opal
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 304
- 543
Wakuu,
Hiki ndio kinachoendelea mtaani kipindi hiki! Wakati wa maandamano wananchi walishuhudia wapendwa wao wakipigwa risasi na polisi na kuona miili ikizagaa mtaani wengine mpaka siku tatu.
Walipojaribu kuchukua miili hii kwa taratibu nyingine za kupumzisha wapendwa wao, polisi waliwakataza, na kuwaambia miili itapelekwa katika hospitali husika (kutegemea na eneo) na wataweza kuichukua huku, lakini sicho kilichotokea.
Wakienda hospitali na kuomba miili ya wapendwa wao wanaambiwa haipo, hata kama mtu alifia hospitalini hapo!
Sasa huku mtaani shida zinaendelea! Misiba inafanywa na kumalizwa bila ya kuwa na miili. Na waandishi wakijaribu kupata taarifa hawapati ushirikiano toka kwa wananchi kutokana na hofu walizonazo. Ni kama polisi wamepita mitaani na kutisha wananchi kuongea na vyombo vya habari, jambo linalokuwa changamoto kupata taarifa kipindi hiki.
Yaani serikali inafanya kila jambo kuhakikisha wanazuia taarifa, lakini wanazuia vipi na mambo yapo akilini mwa kila mtu na vithibitisho kadha wa kadha kwenye simu zetu?
Yaani mmekosa kabisa njia bora ya kuwajibika na hili na kuponya mioyo ya Watanzania inayovuja damu? Hizi hasira zinazoongezeka zitakuja kuleta crisis kubwa zaidi ya hii iliyotokea, na kwa mara nyingine tumewaonya muda mrefu lakini mmeshupaza shingo.