Kufufuka inawezekana kabisa. Yesu ndiye ufufuo na uzima.
Wakati anajiandaa kumfufua Lazaro, Mariam na Martha walifikiri anazungumzia ufufuo siku ya kiama.
Kilichoshindikana kwa hawa jamaa ni mambo yafuatayo:
1. Yesu hakumuweka Lazaro kwenye jeneza, wala si yeye aliyemzika, sasa hawa jamaa miili wameiweka wenyewe kwenye jeneza tayari kuzikwa halafu wanaomba ufufuo, hapo hakuna Imani.
2. Yesu alikuwa anakesha milimani akiomba, mpaka kesho yake anapoingia hekaluni uweza wa Mungu unakuwepo kuponya, leo hii wachungaji wanakesha wakisengenyana, wamegeuza makanisa miradi, hapo hakuna uweza wa Mungu bali uweza wa mwekundu wa msimbazi ambao hauwezi kufufua.
3. Yesu alifufua kwa utukufu wa Mungu, hao jamaa wanataka mtu afufuke kwa uchungu binafsi walio nao, na wengine ili wajaze makanisa mapato yaongezeke, hapo Mungu hashawishiki kufufua.
4. Makanisa ya sasa yamemfukuza Roho mtakatifu na kumkaribisha roho ya fedha itawale, sasa bila Roho mtakatifu ufufuo utatokea wapi? Leo hii ukiingia makanisa yao unaendesha Hummer unapewa uzee wa Kanisa siku hiyo hiyo. Kuna ufufuo hapo?
5. Wakristo wa leo wanaogopa uchawi, shetani na kifo kuliko Mungu. Mungu anasema akiogopacho muovu ndicho kimpatacho. Leo hii ukitaka watu waache kusikiliza neno la Mungu na wakusikilize wewe masaa yote wewe danganya kuwa ulikuwa mchawi na sasa umeokoka. Wataacha mambo yote ya maana kanisani ili wasikilize ulivyokuwa mchawi mahiri Afrika nzima ukichezea mapadre, wachungaji na mashehe.
Naomba niishie hapo. Ufufuo unawezekana kabisa isipokuwa mwana wa adamu atakaporudi JE ATAIKUTA IMANI DUNIANI?