Haijawahi kutokea watu wakaombea mahiti kisha zikafufuka, hii kali...!
Duh jana niliokuwa natazama TBC1 taarifa ya habari sikuamini nilichokuwa nakitazama kuna baadhi ya wahubiri wanawapotosha waumini wao kiasi kwamba wanakuwa wanawaabudu wao badala ya mwenyezi mungu.
Watumishi wa mungu kama Askofu Kakobe wanaingia moja kwa moja katika hili kundi la kuabudiwa wao badala ya Mungu.Fikiria waumini wanashinda siku nzima kanisa kulinda TANESCO wasipitishe waya kwenye kanisa lao,sijui wanatafuta riziki zao saa ngapi ?.Twende mbali kidogo hivi Askofu Kakobe akitangulia mbele ya haki waumini wake wataacha kufanya vituko kama hao jamaa wa huko Kenya ?.Niliwahi kusema haya makanisa ya aina Mzee wa upako,Askofu Kakobe,Mtume na Nabii Jodev na nk yafaa yatazamwe kwa makini sana kwasababu mara nyingi badala ya kumhubiri Kristo mfufuka yamejikita zaidi kuwatukuza viongozi wao.
Kufufuka inawezekana kabisa. Yesu ndiye ufufuo na uzima.
Wakati anajiandaa kumfufua Lazaro, Mariam na Martha walifikiri anazungumzia ufufuo siku ya kiama.
Kilichoshindikana kwa hawa jamaa ni mambo yafuatayo:
1. Yesu hakumuweka Lazaro kwenye jeneza, wala si yeye aliyemzika, sasa hawa jamaa miili wameiweka wenyewe kwenye jeneza tayari kuzikwa halafu wanaomba ufufuo, hapo hakuna Imani.
2. Yesu alikuwa anakesha milimani akiomba, mpaka kesho yake anapoingia hekaluni uweza wa Mungu unakuwepo kuponya, leo hii wachungaji wanakesha wakisengenyana, wamegeuza makanisa miradi, hapo hakuna uweza wa Mungu bali uweza wa mwekundu wa msimbazi ambao hauwezi kufufua.
3. Yesu alifufua kwa utukufu wa Mungu, hao jamaa wanataka mtu afufuke kwa uchungu binafsi walio nao, na wengine ili wajaze makanisa mapato yaongezeke, hapo Mungu hashawishiki kufufua.
4. Makanisa ya sasa yamemfukuza Roho mtakatifu na kumkaribisha roho ya fedha itawale, sasa bila Roho mtakatifu ufufuo utatokea wapi? Leo hii ukiingia makanisa yao unaendesha Hummer unapewa uzee wa Kanisa siku hiyo hiyo. Kuna ufufuo hapo?
5. Wakristo wa leo wanaogopa uchawi, shetani na kifo kuliko Mungu. Mungu anasema akiogopacho muovu ndicho kimpatacho. Leo hii ukitaka watu waache kusikiliza neno la Mungu na wakusikilize wewe masaa yote wewe danganya kuwa ulikuwa mchawi na sasa umeokoka. Wataacha mambo yote ya maana kanisani ili wasikilize ulivyokuwa mchawi mahiri Afrika nzima ukichezea mapadre, wachungaji na mashehe.
Naomba niishie hapo. Ufufuo unawezekana kabisa isipokuwa mwana wa adamu atakaporudi JE ATAIKUTA IMANI DUNIANI?
Arguments zako ziko kisomi kiasi kwa maana ya kwamba unaamini yote yanawezekana kwa Mungu, lakini ni kwa utashi na mpango wa Mungu mwenyewe, na kamwe si kwa mpango wa mwanadamu. Hapo tuko pamoja.
Nisichoamini hata kidogo hapo ni kuwa ati kuna uwezekano wa kumshawishi Mungu afanye alichokuwa hajakipanga kiwe hivyo. Kama kweli Mungu ni mjuzi na mweza wa vyote, ninaamini kuwa Mungu alijua kabla hata hao wachungaji hawajazaliwa kuwa itafika tarehe hiyo iliyofika ya wao kupata ajali ya gari na kufariki dunia, na kuwa hao wafuasi wao wangeomba sana awafufue na pia Mungu anajua kuwa ombi hilo angelitimiza au la. Na tena basi hata ile hali ya utofauti kuwa kuna watakaoamini hayo na wengine hawataamini, bado ni Mungu pia ndiye aliyeumba tofauti hiyo (tukiamini hakuna muumbaji mwingine, na pia haiwezekani jambo lolote kutokea kama Mungu hataki ama hajaridhia jambo hilo kutokea). Kumbe basi wanaomba nini?
Hivi ukimwomba sana Mungu jambo fulani na likatokea hivyo kweli, ni matunda ya sala zako au ni mpango wa Mungu tangu awali kuwa ilikuwa iwe hivyo ilivyotokea? Na iwapo umemwomba Mungu jambo fulani na hukulipata, ni kwamba Mungu kakukatalia maombi yako au ni uleule mpango wake uliokuwako kabla hata hujazaliwa?
Kuna binadamu mwenye uwezo wa kumshawishi Mungu akubali kubadili mpango wa Mungu? Contradictions! Na wajinga wanaendelea kugugunwa tu! Pole yao.
Kufufuka inawezekana kabisa. Yesu ndiye ufufuo na uzima.
Wakati anajiandaa kumfufua Lazaro, Mariam na Martha walifikiri anazungumzia ufufuo siku ya kiama.
Kilichoshindikana kwa hawa jamaa ni mambo yafuatayo:
1. Yesu hakumuweka Lazaro kwenye jeneza, wala si yeye aliyemzika, sasa hawa jamaa miili wameiweka wenyewe kwenye jeneza tayari kuzikwa halafu wanaomba ufufuo, hapo hakuna Imani.
2. Yesu alikuwa anakesha milimani akiomba, mpaka kesho yake anapoingia hekaluni uweza wa Mungu unakuwepo kuponya, leo hii wachungaji wanakesha wakisengenyana, wamegeuza makanisa miradi, hapo hakuna uweza wa Mungu bali uweza wa mwekundu wa msimbazi ambao hauwezi kufufua.
3. Yesu alifufua kwa utukufu wa Mungu, hao jamaa wanataka mtu afufuke kwa uchungu binafsi walio nao, na wengine ili wajaze makanisa mapato yaongezeke, hapo Mungu hashawishiki kufufua.
4. Makanisa ya sasa yamemfukuza Roho mtakatifu na kumkaribisha roho ya fedha itawale, sasa bila Roho mtakatifu ufufuo utatokea wapi? Leo hii ukiingia makanisa yao unaendesha Hummer unapewa uzee wa Kanisa siku hiyo hiyo. Kuna ufufuo hapo?
5. Wakristo wa leo wanaogopa uchawi, shetani na kifo kuliko Mungu. Mungu anasema akiogopacho muovu ndicho kimpatacho. Leo hii ukitaka watu waache kusikiliza neno la Mungu na wakusikilize wewe masaa yote wewe danganya kuwa ulikuwa mchawi na sasa umeokoka. Wataacha mambo yote ya maana kanisani ili wasikilize ulivyokuwa mchawi mahiri Afrika nzima ukichezea mapadre, wachungaji na mashehe.
Naomba niishie hapo. Ufufuo unawezekana kabisa isipokuwa mwana wa adamu atakaporudi JE ATAIKUTA IMANI DUNIANI?
mbona havifanani? tafuta mahali pengie ambapo methali yako ina fit, hapo naona si mahali pakeWajinga ndio waliwao..
Speaking as a christian, what they are doing is absurd. Of-course in Jesus name dead can be raised, but with a purpose and a special reasons, and all miraclea are meant to show people who dont believe!
I dont see any spiritual katika hili, ilikuwa ni uchungu na mshtuko walioupata
Poleni kanisa, kila kitu kina sababu