Miezi miwili iliyopita niliacha rasmi kunywa soda, maana huu mwaka wakati unaanza nilikuwa nazipiga sana, nilikuwa nakunywa randomly tu nikiamua sahiz napiga mbili, kesho moja hadi kuna wiki nilihesabu nilikuwa nimekunywa chupa 17 za soda
Hofu ikanijia nikawa nawaza Kisukari kilivyomtesa mzee wangu (ila sasa kimetulia, anaendele vizuri) sasa nikaona isiwe mbaya. Nilipanga kuacha kunywa soda tangu mwezi wa tatu, ila nikawa nakaa siku mbili sijanywa siku ya tatu nakunywa.
Ilipofika June, nikafanikiwa kuacha moja kwa moja. Hapa nina mpango ninywe soda tena mwaka 2027 kipindi cha Afcon πππ