Wanyama na ndege wa Afrika. 3-Kifaru.

Wanyama na ndege wa Afrika. 3-Kifaru.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,680
Reaction score
20,722
KIFARU

10.jpg

KIFARU ni mnyama aliye mkubwa sana na mnene kabisa. Ingawa watu husema kwamba makao yake ni Afrika, wako wengine wa jamii yake Bara Hindi na Java na Sumatra; tena ziko alama za vifaru wa kale karibu kila upande wa Asia. Haya yanaonyesha kwamba zamani vifaru walikuwa wanakaa mahali pengi, walisakwa kuliko wanyama wengine, na leo wanaonekana zaidi Afrika. Ziko namna mbili :-kifaru mweupe, na kifaru mweusi aliye mdogo kuliko mwenzake.

Kifaru mweupe ndiye aliye mnyama mkubwa kuliko wote ila tembo tu. Ni mwenye urefu mabegani kama futi sita; kinywa chake ni kipana sana; pembe yake ya mbele ni yenye urefu kama inchi hamsini hata sitini. Siku hizi (maana yake katika miaka hii hamsini) kifaru mweupe ameangamizwa mpaka sasa haonekani kabisa katika nchi nyingine za Afrika. Katika nchi za South Africa vifaru wanalindwa na serikali wasiuawe lakini ni wachache kabisa ingawa zamani ya miaka mia walikuwapo kwa wingi kwenye nchi za kusini.

Sababu ya kumsaka kifaru mweupe ni kusudi la ngozi yake inayoweza kukaushwa na kutumika kwa kufanya vipande vya juu ya meza au mijeledi na kwa matumizi mengine. Pembe yake pia ina thamani kubwa. Siyo ya yule mweupe tu; vile vile ngozi na pembe za kifaru mweusi zinatumika. Lakini hawa weusi hawakuuawa kama wenzao weupe, maana wameamka kidogo na kuwa na akili kidogo, basi wanajijongeza upesi kidogo. Watu wengi wa Afrika wanakula nyama ya kifaru nao husema kwamba ni chakula kizuri.

Ingawa tunamwita kifaru mweupe hasa si mweupe; rangi yake ni ya majivu meusi. Yule mweusi anatembea pengine pande za mto Limpopo na pengine kaskazini kama Habeshia na nchi ya Somaliland lakini kwake hasa in Kenya na Tanganyika, Angola, Rhodesia na Mozambiki.

Ngozi ya kifaru wa Bara Hindi na Sumatra imepindwapindwa katika makunyanzi makubwa lakini kifaru ya Afrika ana ngozi sawasawa pasipo makunyanzi. Pembe si pembe hasa, maana sizo za mfupa, zinatoka katika ngozi na nyama.

Ungefikiri kama kifaru ni mnyama mkali lakini si mkali zaidi. Masikio yake ni mazuri tena ni mwepesi wa kusikia harufu lakini macho yake hayaoni vizuri. Kwa hiyo ikiwa mtu akikaa kimya kifaru atapita karibu naye asimwone.

Mara nyingi kifaru anaporuka siyo kwa kujaribu kumwuma adui, zaidi anajaribu kumtoroka. Anaposhtushwa au kukasirika anazunguka- zunguka akijaribu kusikia harufu ya adui maana hawezi kuona sawa kuliko yadi arobaini au hamsini.

Ni binadamu aliye adui wake mkuu; maana ni wanyama wachache tu wanaoweza kupigana na kifaru kwa sababu ya ukubwa wake, unene wake na ukali wa pembe yake ndefu. Hata simba hawaendei kifaru na tembo, anawaacha peke yao. Pengine kifaru amemrukia mtu aliyepanda juu ya farasi na kuwapiga mara moja akiwapitisha pembe yake katika farasi na mtu pia. Kwa hiyo amewaangusha wote wawili chini na kuwaua pamoja.

Kama tembo, kifaru hupenda sana kuoga katika matope; basi hapendi kujitenga na maji kwa muda mrefu. Hujifurahisha kwa kugaagaa katika ziwa dogo na kujifunika na matope. Haya yanamsaidia kujifurahisha na pia yanazuia kupe wasiingie katika ngozi yake na kufanya vidondavidonda.

Rafiki wa kifaru ni ndege shasi anayefuatana naye kila aendako. Huchukuliwa mgongoni mwa rafiki yake mkubwa au chini ya tumbo lake akishika kwa miguu, naye huondoa kupe katika ngozi ya kifaru. Shasi anamsaidia kifaru kwa njia nyingine maana anamlinda; akiona kwamba hatari inakaribia anapiga mlio wa kumpasha habari rafiki yake.

Kifaru jike humzaa mtoto mmoja kwa kawaida, isipokuwa mara kwa mara wanazaliwa wawili pamoja. Mtoto anapozaliwa mama anajificha katika chaka msituni, asiwe na haja kwenda mbali kutafuta maji wala chakula. Mtoto akianza kukua hutembea na mama yake na kukaa naye kwa miaka mingi. Kifaru amefanana na tembo kwa kuishi siku nyingi, na kwa hiyo, watoto hukawia kuwa wanyama wazima wenye nguvu nyingi ambao wanajiangalia wenyewe. Ndama wa kifaru anapoacha kunyonya huanza kutumia vitawi vichanga vilivyo chakula cha kifaru mzima.
 
4-Mwanamke mwenye makalio makubwa:
Screenshot_20250417-153233.png


Anapenda pesa na anadharau sana ila kichwani hazimo
 
  • Kicheko
Reactions: rr4
Masahihisho hakuna NCHI duniani inaitwa Tanganyika. Kuna ziwa Tanganyika na wilaya Tanganyika.


Ifike wakati tuseme Kwa pamoja no reform no elections.

Yaaani wenzetu Shule walisomea wapi sijui mpaka wanakera yaani hajui kabisa kabla ya 1840 SEYYID SAID Kuja zanzibar.zanzibar haikuwa state .

Ako kukazana Tu at Zanzibar NCHI , Tanganyika akidhani ndo uzalendo kumbe NI uzwazwa Tu na kujiondolea kizuri nyumbani kwako mwenyewe kisha kuwapa waraabu Koko waliokimbia makwao.(Omani)

Rais WA JMT NI mzanzibar SASA mwambieni apitishe agenda at Zanzibar NI NCHI huru aione cha Moto Kama kilichomkuta Yule WA Korea kusini .
 
Eti kifaru sio mkali, weee hakuna mnyama wa mwituni anayeweza kumletea zengwe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom