Desire Dizaya
JF-Expert Member
- Feb 16, 2015
- 6,476
- 11,673
tatizo hawako fit...mwakani wamweke hassan kazoa waone
Ajira mpyaVijana wawili wakazi wa kijiji cha Mgungira wilaya ya Ikungi mkoani hapa,wamenusurika kifo baada ya kuanza kutapika na kuishiwa nguvu katika shindano la kula chapati 30 pamoja na kunywa vikombe 10 vya chai ya rangi.
Shindano hilo la aina yake hufanyika kijijini hapo ambapo liliandaliwa,vkuratibiwa na kudhaminiwa na Guhumela Lubadila na vigezo vya kuwa mshindi ilitakiwa mshiriki ale chapati zote 30 na anywe vikombe vyote 10 vya chai ya rangi. Vitu vyote hivyo, gharama yake ni shilingi 9,200.
Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Kata ya Mgungira, Hussein Juma Ng’eni, alisema washiriki walikubaliana mshindi asipewe zawadi yoyote, zawadi yake ni chapati 30 na vikombe 10 vya chai atakavyokuwa amekula na kunywa.
Aidha, alisema kuwa endapo vijana hao wakashindwa kufikia lengo la kula chapati 30 na kunywa vikombe vya chai 10, watapaswa wamlipe mmiliki wa mgahawa aliyetambulika kwa jina la mama Benja Mgungira.
Afisa mtendaji kata huyo, alisema endapo mshindi angepatikana, mdhamini wa shindano hilo, Guhumela, angemlipa mmiliki wa wa mgahawa, shilingi 9,200.
Ng’eni alisema vijana hao kama ingekuwa ni shindano la mpira wa miguu, wangekuwa wametoka suluhu ya kufungana magoli sawa kwani wao kila mmoja alikula chapati 19 na vikombe vinne vya chai ya rangi.
“Baada ya kufikia hatua hiyo, kila mmoja alianza kutapika mfululizo huku wakitokwa na jasho jingi na kisha kuishiwa nguvu. Kitendo hicho kilisababisha wakimbizwe katika zahanati ya kijiji, kupatiwa matibabu .Hali zao kwa ujumla,zinaendelea vizuri,” alisema.
Alisema kuwa baada ya kushindwa katika shindano hilo, vijana hao watalazimika kulipa shilingi 9,200 kwa mujibu wa makubaliano ya shindalo hilo.
Chanzo: Dewji blog
Kama unataka tukubebe na ambulanceMimi nakula Vitumbua Ndoo ya Lita 10 iliyojaa
Ati nini? Kwa mwanaume wa Dar labda. Nimetoka kulima na sheli (plau) tangu saa 10 usiku mpaka saa 4 asubuhi ndiyo unaniletea chapati 30 aisee patachimbika. May be nitabakiza mbili hivi za kwenda nazo machungani huko kusukumia masaa.Chapati 30 ni nyingi sana, hata ukipewa siku nzima unaweza usizimalize
Vitu vidogo hivyo....chapati 30 nazo chapati??? Chapati zenyewe nyepesi km karatasi halafu transparent ......Chapati 30 ni nyingi sana, hata ukipewa siku nzima unaweza usizimalize
Natamani nije dar walete shindano la kula hivyo vichips vyao...Naimani kabisa watakimbia...Ati nini? Kwa mwanaume wa Dar labda. Nimetoka kulima na sheli (plau) tangu saa 10 usiku mpaka saa 4 asubuhi ndiyo unaniletea chapati 30 aisee patachimbika. May be nitabakiza mbili hivi za kwenda nazo machungani huko kusukumia masaa.
Mwanaume wa Dar chapati 30 hata mwezi aisee anaweza kumaliza akihangaika nazo hasa kama anaambatanisha na maembe yaliyopakwa pilipili. Na meno yakipata ukakasi basi hata mwaka unakatika [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23]Hao watakuwa watoto walaini laini ndomana wameshindwa kumaliza hizo chapati Mimi leo kuna sehemu walinirundikia misoda ya coca cola nilicho wafanyia hawakuamini na mpunga wao nikabeba![]()
Hao watakuwa watoto walaini laini ndomana wameshindwa kumaliza hizo chapati Mimi leo kuna sehemu walinirundikia misoda ya coca cola nilicho wafanyia hawakuamini na mpunga wao nikabeba![]()