Kuna hili wimbi la wasanii kwenda South Africa kufanya shooting za nyimbo zao,Binafsi sijaona ubora wowote wa video ya Ommy dimpoz na Wanjera yake, nilidhani kufunga safari all the way to South africa tungepata something new, ila sijaona...kwa jinsi ilivyo, nafuu tu hiyo video ingefanyiwa shooting hapa Bongo, angeserve gharama za kusafri hadi huko south Africa.Halafu hata maudhui yake sijaelewa, aliyeelewa anisaidie, may be am a slow observer.
Wimbo wa hovyo, video hovyo hovyo! Wasabi hebu umizeni kichwa! Ommy dimples, Ally kiba nyimbo zenu mbaya kiukweli, Linex kajitahidi
Dah kweli tunatofautiana
mbona me naona iko vizuri tu... na inaburudisha, kwa kweli me naona quality iko poa na idea ya machizi nayo iko fresh tuu
Me nafikiri kinachowapeleka sauzi ni kutafuta kutoboa kimataifa maana video ikitoka ikishaonekana imefanywa na producer fulani tu lazima ichezwe na vituo vya TV vya kimataifa
Sio video zote wanazofanya south zipo poa kivile..nyingine kama za bongo tu..na kuna video nyingi tu za kibongo zina ubora kuliko hizo za south...sema moja ya sababu inayowapeleka huko ni kwamba ma-director wa huko wanakusaidia kuipush video yako kwenye tv za kimataifa..kitu ambacho ma-director wengi wa bongo hawakifanyi
Kuna hili wimbi la wasanii kwenda South Africa kufanya shooting za nyimbo zao,Binafsi sijaona ubora wowote wa video ya Ommy dimpoz na Wanjera yake, nilidhani kufunga safari all the way to South africa tungepata something new, ila sijaona...kwa jinsi ilivyo, nafuu tu hiyo video ingefanyiwa shooting hapa Bongo, angeserve gharama za kusafri hadi huko south Africa.Halafu hata maudhui yake sijaelewa, aliyeelewa anisaidie, may be am a slow observer.
Naomba unitajie directors wachache kati ya hao wengi wanaoweza kufanya video nzuri zaidi au kama ya hizo wanazofanyia SA, na mfano wa moja wa video zao unazoona ni nzuri.Ni kweli kuna directors wakali wengi tu bongo wanaoweza kutengeneza videos nzuri sana
Muziki ni biashara, so watu wanaangalia bizness zaidi. Kinachowapeleka south ni quality ya picha za video. Vituo vikubwa vinazingatia sana quality na idea ya video, wanapocheza video wakianza kupiga video ya Chris brown,wakaja ya rihana,wakaja ya kanye west alafu ikaja ya kiafrica mfano ya p squairw bas kusiwe na tofauti ya kiivo kiasi mtu akakimbilia remote ku change..Pata picha imechezwa we dem boyz ya wiz,ikaja hold u down ya djkhaleed kisha ikaja mama neema ya 20 percent watu wanang'aa km vitumbua.
Hili la kwenda south lisichukuliwe negative kiasi hicho, ishu ni unaenda sauz umejipangaje coz godfather au wengine kazi yao ni kudirect, script na kila kitu unajipanga mwenyewe ukitaka farasi utaletewa ukitaka helkopta utaletewa. Mbona Adam alienda na Mavoko wakakodi izo Led quality zile zile.
Bongo hakuna good video directors, angalia video hzi mbili za madee na chege na temba. Ni good location tu, hakuna story line, watu wanatembea mara wako chumbani. Hapo ndio AJ anapochemsha, hata mm ningekuwa msanii nisingeweza peleka kazi zangu kwake. Angalia video za God father. Kuanzia hii wanjela, mdogo mdogo, nitampata wapi. Unaona kuna extras kama 20 hv, yaani watu professional sio eti unaita masela kwenye kushoot.
Promo moja ya sababu, ila na hata ubora wa kamera wanazotumia na vifaa vingine vya kufanyia na kuhariria video ni moja ya sababu zinazowapeleka SA kwa wasanii wanataka video nzuri. Mfano mzuri tunamuamini sana Adam Juma, ila angalia na linganisha kazi zake alizofanya akiwa SA na zile alizofanyia TZ ubora wake ni tofauti kabisa, ndio tujiulize ni kwa nini ziwe tofauti wakati muongozaji ni huyo huyo mmoja.Hapo kinachofuatwa ni kama baadhi ya wachangiaji walivyosema, ukifanya kazi na directors wa bondeni ni rahisi kazi zako kuonekana kwenye channels kubwa coz mtu kama Godfather ashaaminika huko kwamba kazi zake ni za viwango. Bongo nowdays tunajitahidi pia, tungekuwa na mkono huko kuna baadhi ya kazi zinaviwango kabisa ya kuchezwa kwenye tv kubwa, mfano PACHA WANGU ya MAVOCO iliyotengenezwa na AJ ni video nzuri sana,inastahili kuchezwa tv yoyote