Wangapi watasheherekea Kwanzaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wangapi watasheherekea Kwanzaa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fundi Mchundo, Dec 24, 2008.

 1. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  I like the Nguzo saba principles...

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]NGUZO SABA
  [FONT=Arial, Helvetica, Geneva](The Seven Principles)[/FONT] [​IMG] [FONT=Arial, Helvetica, Geneva]Umoja (Unity)
  To strive for and maintain unity in the family, community, nation and race.
  [/FONT][​IMG] [FONT=Arial, Helvetica, Geneva]Kujichagulia (Self-Determination)
  To define ourselves, name ourselves, create for ourselves and speak for ourselves.
  [/FONT][​IMG] [FONT=Arial, Helvetica, Geneva]Ujima (Collective Work and Responsibility)
  To build and maintain our community together and make our brother's and sister's problems our problems and to solve them together.
  [/FONT][​IMG] [FONT=Arial, Helvetica, Geneva]Ujamaa (Cooperative Economics)
  To build and maintain our own stores, shops and other businesses and to profit from them together.
  [/FONT][​IMG] [FONT=Arial, Helvetica, Geneva]Nia (Purpose)
  To make our collective vocation the building and developing of our community in order to restore our people to their traditional greatness.
  [/FONT][​IMG] [FONT=Arial, Helvetica, Geneva]Kuumba (Creativity)
  To do always as much as we can, in the way we can, in order to leave our community more beautiful and beneficial than we inherited it.
  [/FONT][​IMG] [FONT=Arial, Helvetica, Geneva]Imani (Faith)
  To believe with all our heart in our people, our parents, our teachers, our leaders and the righteousness and victory of our struggle.
  [/FONT] ­ Maulana Karenga
   
 3. M

  Mama JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Leo tunatafakari Umoja!
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yah hii bomba tu
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Leo tunatafakari: Kujichagulia (Self-Determination)
  To define ourselves, name ourselves, create for ourselves and speak for ourselves.

  Sisi kama watu weusi tuna nafasi gani katika kujitambua? Kwa nini mpaka leo tunakubali identity tuliyopewa na wengine? Kukubali huko ndiko kunakotupelekea kuamini kuwa " Miafrika ndivyo tulivyo." Kukubali huko ndiko kunakotufanya tuamini kuwa tuna laana na hakuna anayeweza kutubadili. Kukubali huko ndiko kunatufanya tuwakumbatie wakina Mugabe ambao wamejiteua kuwa ndio wasemaji wetu. Ni lini tutaacha kukumbatia tuliyoletewa na kukumbatia cha kwetu? Sikukuu hii ikiwa ni mojawapo!Ni lini, tutakataa, na kusema kwa nguvu, kwa sauti kubwa " hapana, sivyo tulivyo!"

  Amandla...........
   
 8. M

  Mama JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Lots of thanks FM.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Dec 27, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Actions speak louder than words....I can show you better than I can tell you...your bark is worse than your bite...etc. etc.....

  Mpaka tutakapoanza kuongea kwa vitendo tutabaki kuwa Ndivyo Tulivyo hata mfanyeje. Hata wakiniondolea signature yangu, hata hata nikibaki peke yangu nisemaye ndivyo tulivyo, yaani hata iweje, tusipotenda maneno yetu ya kukataa kuwa ndivyo tulivyo hayatabadilisha ukweli. Kitu kitakachobadilisha ukweli ni vitendo. Maneno hayabadilishi ukweli.
   
 10. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe kwenye hili kuwa ni vitendo vyetu vitakavyoonyesha kuwa "sisi sivyo tulivyo". Ni juu ya kila mmoja wetu kuhakikisha kwa vitendo kuwa hapana, hatuko hivyo. Lakini kabla ya yote tunawajibika kuelewa ni nini tunachokataa na kuweka wazi msimamo wetu. Msimamo ambao hautakuwa wa maneno tu bali utaongozana na vitendo.

  Amandla........
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Leo ni siku ya kutafakari Ujima (Collective Work and Responsibility):
  To build and maintain our community together and make our brother's and sister's problems our problems and to solve them together.


  Ni kwa vipi tunalia na mwenzetu anapopata shida? Mara ngapi tumeangalia na wakati kufurahia matatizo ya wenzetu? Kwa nini imechukua mpaka watu wa magharibi kutusema ndiyo tuone aibu jinsi tunavyowatendea albinos? Aui tunapoagiza magari ya fahari kwa ndege wakati wenzetu hata nauli ya daladala inawashinda! Ni vipi, wewe na mimi, tumekuwa our brother's ( or sister's) keeper? Nani atatupenda kama sisi wenyewe hatupendani?
   
 12. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Leo tunafakari Ujamaa (Cooperative Economics):
  To build and maintain our own stores, shops and other businesses and to profit from them together.

  Wangapi tumeweza kufanya hivi? Au hii sera haina nafasi tena katika jamii ya leo?
   
 13. M

  Mama JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Fundi kwanza asante. Pili, hii itawezekana pale tu tutakapojijengea uaminifu kwa kila mmoja wetu (mtu binafsi) na uaminifu kwa society. Kama mtu anaweza kukikimbia na michango ya harusi aliyochangiwa kwa ajili ya harusi yake mwenyewe, tunaweza kumuamini na kumpa usimamizi wa hizo biashara ?

  Kuna mahali hili somo la kuwafikiria wengine kama tunavyojifikiria wenyewe linatolewa ? May be tutaachana na selfishness leading to the elimination of ufisadi.

  Baada ya hapo FM, hili litawezekana. Kwa sasa hata kukiwa na sera, bado hatutaweza.....ni wizi mtupu.
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mambo ya uaminifu kwa wabongo. Huo ni msamiati wa kichina.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Leo tunatafakari, Nia (Purpose):
  To make our collective vocation the building and developing of our community in order to restore our people to their traditional greatness.


  Hii kwangu mimi ina uzito wa pekee hasa katika wakati huu ambapo kila ukiangalia kuna mifano ya jinsi sisi kama watu weusi tulivyo nyuma kimaendeleo. Ni rahisi sana kutumbukia katika aidha dhana ya kusema " sisi ndivyo tulivyo" au kuwanyoshea vidole wengine na kudai wao ndiyo waliosababisha na ndiyo wanaoendelea kusababisha matatizo yetu! Hivi kweli, tukiamua, hatuwezi kweli kujitoa huku tuliko? Tunahitaji kweli upendeleo au mfadhili wa kutukwamua? Mimi siamini hivyo. Sijui mwenzangu?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Dec 30, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Fundi, tukiamua kufanya kweli tunaweza! Lakini kabla ya kuamua inabidi tukasirike na kusema sasa enough is enough. Nikisema sisi Miafrika Ndivyo Tulivyo watu wananikasirikia mimi. Hiyo ni misplaced outrage. Kinachotakiwa kukasirikiwa ni hali tuliyonayo. Unapomkasirikia Ngabu haisaidii lolote. Ngabu akiacha kusema hivyo ina maana hali yetu itabadilika? Hell no.

  Najua wengi hawanielewi nini maana na dhumuni la kwangu kusema sisi Miafrika Ndivyo Tulivyo. Wanadhani labda mimi kweli naamini hivyo. Hata hivyo hamna neno. Ipo siku nitakuja kuweka bayana nini namaanisha nikisema hivyo.

  Kwa hiyo niko na wewe katika kuamini kuwa tukiamua tutaweza tena bila hata hao wafadhili. Mimi ni mmoja wa wapinga misaada ya kutoka kwa wafadhili wa nguvu sana. Misaada imetudekeza mno. Kuweza tunaweza lakini kabla ya kuweza inabidi tukasirike kwanza. Hayo ndo yangu machache tu kwa leo.....
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nyani Ngabu. Mimi nakuelewa. Na uko sahihi kabisa kusema kuwa ni lazima tukasirishwe na hali tuliyonayo. Bahati mbaya wengi wetu tumeikubali hii hali kuwa ndiyo mapenzi ya Mungu.

  Nimekuelewa sana hata kabla ya kuweka bayana una maana gani. Kwenye hili najua tuko upande mmoja.

  Respect.

  Amandla.....
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Dec 31, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Leo tunatafakari Kuumba (Creativity)
  To do always as much as we can, in the way we can, in order to leave our community more beautiful and beneficial than we inherited it.

  Huu ni wakati wa kuwaenzi wakina Shaaban Robert,Mbaraka Mwinshehe, Juma Kilaza, Robert Nesta Marley, Billie Holiday, Louis Armstrong, Tupac Umar Shakur, Miriam Makeba, Toni Morrison, Zadie Smith, Richard Wright, Walter Mosely, James Baldwin, David Adjaye, Ralph Ellison, Wole Soyinka, Chinua Achebe, Okot p'Bitek, Bi Kidude, Shakila,Dr. Hukwe Zawose, Professor Jengo, R. Ntila, Doreen Mandawa, Mohamed Raza, Morris Nyunyusa, Eduardo Tingatinga na wengine wengi. Unakaribishwa kuongezea unaodhani nao wanastaili kuenziwa.

  Amandla.....
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Dec 31, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Nyani Ngabu, Mwanakijiji, Kelly01......
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Imani (Faith)
  To believe with all our heart in our people, our parents, our teachers, our leaders and the righteousness and victory of our struggle


  Leo ndiyo tunamalizia sherehe zetu za kwanza. Tunawasha mshumaa wetu wa mwisho kwenye KINARA chetu na kuandaa KARAMU kwa wale tuwapendao. Baada ya karamu, tunakaa na kutafakari maana ya neno IMANI katika jamii yetu ya watu weusi. Tunajiuliza tulikotea wapi hadi hapa tulipofika. Tunawazungumzia waliotutangulia, wakina; Kinjikitile "Bokero" Ngwale, Mkwavinjika Munyigumba Mwamuyinga ( Chief Mkwawa), Shaka, Frantz Fanon, Aime Cesaire,Dedan Kimathi Waciuri,Waruhiu Itote (General China), Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, Leopold Senghor, W.E.B. DuBois, Malcolm X, Martin Luther King, Soledad Brothers, Marcus Garvey,Thomas Sankara, Steve Biko, Malkia Nzinga Mbande, Sojourner Truth, Harriet Tubman bila kuwasahau walio bado nasi wakina; Angela Davis, Desmond Tutu, Nelson Mandela n.k. Ni wakati huu ndiyo inabidi tuwaulize babu zetu, bibi zetu, wazazi wetu kuhusu huko walikotoka. Ni wakati huu inabidi tuangalie wenzetu na kujipa moyo kuwa saa ya mapambano ni sasa! Kuwa pamoja na wakina Gabriel Mugabe, tutafika huko tunakoenda na siku moja tutaweza kuamka na kusema bila kusita kuwa " mimi ni mtu mweusi, mwana wa Afrika na utanikubali kama nilivyo maana ndivyo nilivyo na sivyo unavyotaka niwe".

  Baada ya kutafakari hayo, tutazima KINARA chetu na kungoja siku ya kesho na kesho kutwa zitatuletea nini, sisi wana wa Afrika. Tutazisubiri bila kuwa na wasi wasi maana tunajua kuwa hatuko peke yetu kwenye mapambano haya maana tumetoka mbali, na waliotutangulia wako nasi, na iko siku tutafika mwisho wa safari yetu!

  Amandla...........Wana wa Afrika! Amandla.......
   
Loading...