Wangapi mlishawahi kutumia hii kitu?

NI KULE KUPITWA NA WAKATUI TU, LKN VYA KALE NI DHAHABU, ubora wa kanda ktk uimara, ni mara mia zaidi kuliko cd
 
Mimi mpaka imenibidi ninunue converter kabisa ili nihamishe nyimbo zote na kuziweka katika .mp3 format. Kuna kwaya za zamani wakati ule uimbaji wa injili haujawa biashara nyimbo zake ni safi mno kiasi kwamba sitaki kuzipoteza.
 
Mi natumia saa hizi kwenye gari. Nainjoi nyimbo mpya za Brenda Fassie na Mbaraka Mwishehe. Pia kuna Album mpya katoa Hemed Maneti na Lucky Dube
***
-->Ikigoma itoe ipigepige kiganjani/
pia usisahau pen aina ya bic / ikikataa kabisa unazungusha mpaka ilainike then una play tena.
 
Iilifikia mahali tunaringishiana,mwenye tape ya 'crome dioxide au ferro' ndio anaonekana kidume,wewe mwenye ki-'type one' chako cha 'normal position' unaonekana umepitwa na wakati.Nadhani wapo ambao wanakumbuka haya ma terminology kwenye aina na ubora wa kanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…