Wanene wasiopungua na wembamba wasionenepa, hii iko vipi?

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,963
NATUMAI MU WAZIMA.

Ndugu zangu ma dokta na manesi na wote wenye uelewa wa mambo ya afya naomba mnijuze hili swali linalonitatiza kwa muda mrefu sasa.
Kama habari inavyosema, wanene wasiokonda na wembamba wasionenepa, ngoja niwafafanulie kidogo, unamkuta mtu ni mnene iwe wa kuzidi au wa wastani lakini yeye anataka kupungua japo hana nafasi ya mazoezi,lakini anafuata kanuni zote za kupungua. Kwa mfano baadhi ya watu wakifanya yafuatayo lazima wakonde sana tena sana, lakini si kwa huyu/hawa

1. Atapunguza kula kwa 50%
2.Hatokula vyakula vya mafuta.
3.Atafunga ( kwa wale wafungaji)
4.Anafanya mazoezi

Lakini yote ni bure hapungui wala nini, hii inakuwaje wakuu ????

Kundi la pili hili ni la wembamba yaani ni ule wembamba wa kukera,japo inaelezwa unene si mzuri lakini si kwa wembamba wa watu hawa na unakuta na mwenyewe anataka anenepe japo kidogo lakini wapi,na anafanya yafuatayo ktk hali ya kawaida wengine wangenenepa lakini kwa hawa hola.

1. Anaongeza ulaji wa chakula.
2.Anaongeza ulaji wa mafuta.
3.Hafanyi mazoezi.
4.Kazi zake si za shuruba. (kazini kwa gari,ofisini kiyoyozi na nyumbani ni mboga 10)

Haya swali inakuwaje huyu/hawa watu wasinenepe wakati watu wengine wakiwa ktk maisha hayo mbona atakuwa kama kawekwa hamira jinsi wanavyoumuka hii inakuwaje ?????

Karibuni wakuu.
 
Mkuu kunenepa ama kukonda ni suala la afya ya akili tu, unaweza kuwa unakula sana na vyote ulivyovitaja ila kama akili haijakubali kuyapokea mabadiliko mwili hauwezi kuiendesha.
 
kunenepa ni kuridika mkuu kuna ambaye anakula maini but hanenepi ila mwngine ugali mlenda na amenenepa so ts only about kuridhka mkuu....***brain***
 
Mkuu kunenepa ama kukonda ni suala la afya ya akili tu, unaweza kuwa unakula sana na vyote ulivyovitaja ila kama akili haijakubali kuyapokea mabadiliko mwili hauwezi kuiendesha.
Sawa mkuu,lakini wewe hujakutana na watu huko mitaani wakimuona mtu mnene basi watasema HAFANYI MAZOEZI AU ANAKULA SANA, na wakimuona mwembamba wanamuona NI WAMAZOEZI ANA DHIKI NA HAENDEKEZI KULA.
 
Pole sana ndugu,unavyohisi una mawazo au unakosea wapi ??
 
Mimi kama ni kula nimekula sana lkn wapi siongezeki hata kilo moja wakuu nahisi labda mwili wangu una upungufu wa virutubisho hembu nisaidieni ni virutubisho gani nitumie?? huu wembamba siyo kabisa
 
kuna kitu knaitwa body type endomorph,mesomorph na moja nimesahau...kila body ina style yake ya kuchoma mafuta mwilini kwa mfano mesomorph ni mtu mwenye uwezo wa kuchoma mafuta faster na ana musles nyingi ni type za watu ambao gym kdg tu mwili unakua mkubwa wengine unaweza sema mbeba vyuma wkt anashinda kwenye tv...kwahy google upate mwanga kdg khs ilo swali lako
 
Back
Top Bottom