tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,076
- 20,617
Hukumu ya kifungo cha maisha kwa wahuni waliotumwa na afande kumbaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya ni kiinimacho ambacho kimetumiwa na Serikali kuwapiga changa wananchi baada ya suala hilo kwenda viral. Ndivyo inavyoonekana dhahiri shahiri!
Nasema hivi kwa sababu ukiangalia majibu yanayotolewa na viongozi wa serikali baada ya hukumu hii ya mchongo yanaashiria kuwa hukumu hii ni kiinimacho tu. Sababu zipo nyingi sana lakini nitazitaja chache kama mfano.
Mosi, Afande aliyehusika kuwatuma hawa wahuni kumbaka na kumlawiti binti wa watu bila huruma ameponyokaje? Binti aliyetakiwa kumuomba radhi Afande yupo. Kwanini asingetoa ushahidi kumtia hatiani afande? Je, akiletwa mbele ya binti aliyefanyiwa ukatili, hawezi kumtambua? Anaweza. Sasa mzunguko huu wote na danadana za hapa na pale zinatoka wapi? Aidha, wale wahuni wangeminywa pu**mbu lazima wangesema ukweli na kesi ingeisha. Kwanini sasa kesi hii ya Afande inakuwa na mzunguko mrefu hivi?
Pili, kiasi cha pesa cha Tsh 1 million ambacho wamepigwa faini ni upuuzi mtupu. Mtu kafanyiwa ukatili na wanaume 5 halafu unakuja kuwatoza Tsh 1 million ni upumbavu. Mahakama zetu zina mambo ya kipimbi sana.
Tatu, wahuni waliomfanyia ukatili binti wa watu walikuwa 6. Je, kwanini wahuni wawili waliosalia wanafichwa hadi sasa na hawatajwi? Wana ukubwa kiasi gani hadi wafichwe?.
Nne, majibu ya kejeli yaliyotolewa na waziri Gwajima mitanfaoni baada ya kuulizwa na wananchi, yanaonesha kuna kitu kinafichwa. Waziri aliulizwa kuhusu suala la Afande, badala ya kuweka msimamo wa kitaalamu akaishia kumtetea na kuwakejeli waliomuuliza swali. This is rubbish.
Tano, kuna uwezekano hawa wafungwa wakaja kutolewa jela kwa msamaha wa rais baada ya kutumikia kifungo chao kwa miezi kadhaa. Au wanaweza kuja kuachiwa huru kimizengwe. Ushahidi wa hili ni kitendo cha serikali kuchelea kuwataja wahuni hawa kwa vyeo vyao vya kijeshi wakati walipokamatwa licha ya wananchi kupiga kelele.
Aidha, kuna uwezekano hawa jamaa ni members wa kikundi cha utekaji. Kwamba kama taarifa zao zisinge-leak (vuja) mapema huenda wangemuua binti wa Dovya baada ya kumaliza kumbaka na kumlawiti.
MAONI YANGU
Nchi hii ina mambo ya kijinga sana. Yaani raia wasiokuwa na hatia wanadhulumiwa haki zao za msingi, halafu wao wanaleta maigizo kwa kuwafunga wahalifu kifungo cha mchongo. Ndio maana nchi haipati maendeleo kwa sababu imelaaniwa na Mungu.