Wanawake wenye sura ya aina hii hawajiamini……!

Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000

Hiyo hapo juu ni sura ya mwanamke. Ni sura ambayo pengine umeshakutana nayo mahali au ambayo unaijua vizuri. Kama kuna mwanamke mwenye sura ya aina hiyo, ambaye unamjua vizuri au ambaye uko karibu naye, msome tabia zake, halafu uniambie ulichogundua. Ni wazi utagundua kile nitakachoeleza humu kuhusu tabia za wanawake wenye sura za aina hiyo.

Angalia mdomo, pua, macho na paji la uso. Hayo ndiyo maeneo ambayo yanakupa sura. Bila shaka ukiangalia kwa makini, sura hiyo ni nzuri kwa mujibu wa mazoea yetu katika kutazama tulichofundishwa kwamba ni kizuri au kibaya. Wanawake wenye sura hiyo, kwa kawaida ni wenye aibu zinazotokana na kutojiamini. Kwa sababu ya kutojiamini, kuna wakati hujaribu kufanya mambo kwa kupita kiwango chake na kutafsiriwa kwamba wanaringa au wana dharau.

Wanawake wenye sura kama hiyo hudanganyika kirahisi kwa wanaume kwa sababu wenyewe ni waaminifu kwa kiasi cha kutosha. Huamini wanaume kirahisi kwa sababu, wanadhani kila mtu ni mwaminifu na mkweli kama wao. Kukuta mwanamke wa sura hiyo akiwa anaendeshwa na mwanaume ni jambo la kawaida.

Lakini kuna wale wenye sura kama hiyo ambao wamjikagua vibaya kwenye kioo au wameambiwa kitu tofauti utotoni, ambao huwa wahuni, yaani wasioaminika. Hata hivyo, ukiwaangalia hao kwa makini, suala linarudi palepale kwenye kutojiamini. Hata hivyo ni wanawake wenye bahati ya kuaminika, ingawa huharibu bahati hiyo wao wenyewe bila kujua. Wanaaminika kwa sababu ni waadilifu na wanaojua kuishi na watu kwa sehemu kubwa.

Wanawake wa sura hiyo hawana makuu, isipokuwa ni wababe sana. Wana aina fulani ya ubabe ambao ukiuangalia sana ni kutokana na kutojiamini kwao. Kwa hiyo wanawake wenye sura hii wanaharibiwa na kukosa kwao kujiamini tu. Kama wakijenga kujiamini, hutokea kuwa watu wenye kuaminika zaidi na kufika mbali sana.

Wanajua kupenda, lakini wanajiachia sana hadi wanajikuta hawana kauli tena kwa wapenzi wao. Ni wagumu kufanya uamuzi wenye kushika kwenye uhusiano. Na wanaweza kuamua kuondoka na kesho wakarudi kubembeleza wenyewe. Wana huruma na wako tayari kushiriki kidogo walicho nacho na wapenzi wao au watu wengine.

Wanapenda sana mzaha ili kuwafanya wengine wajisikie vizuri. Lakini wao wanapotaniwa, mtaniaji ni lazima awe mwangalifu, vinginevyo hakawii kuwaudhi. Hata hivyo upole hutokea kuwaonea pia. Mwanaume akipata mke wa aina hii anaweza kujidai kwamba, ana mke wa maana kwa sababu ya sifa ya uadilifu na upendo wa dhati lakini kama nilivyosema, inabidi mwanaume huyo amsaidie mwanamke huyu kujiamini.

Uzi huu uwafikie kina, gfsonwin, nivea, nyumba kubwa, BADILI TABIA, farkhina, jouneGwalu, charminglady, Ciello, Madame B, MadameX, lara 1, Paloma, NATA, Neylu, Yummy, SnowBall, Mwita Maranya, platozoom, Eiyer, MwanajamiiOne, Angel Msoffe, fabinyo, King'asti, Arushaone, Mungi, Erotica, Natalia, Zinduna, matumbo, Jiwe Linaloishi Mentor, Kijino, Kaunga, BelindaJacob, HorsePower, Kongosho na wengineo nisiowataja........
 
King'asti

King'asti

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
27,687
Points
2,000
King'asti

King'asti

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
27,687 2,000
Mie.umenikonfyuzi mdingi. Sasa ni wazuri ama sio wazuri? Waaminifu halafu tena wanadanganywa na wanaume?

Wapambe wa big brother africa, huyu anafanana na sheila, mshiriki wa kenya?

Well, nashukuru Mungu mie nafanana na jembe la ukweli, king of stories in east and central africa, dingi wa kimataifa, Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,019
Points
2,000
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,019 2,000
Mie.umenikonfyuzi mdingi. Sasa ni wazuri ama sio wazuri? Waaminifu halafu tena wanadanganywa na wanaume?

Wapambe wa big brother africa, huyu anafanana na sheila, mshiriki wa kenya?

Well, nashukuru Mungu mie nafanana na jembe la ukweli, king of stories in east and central africa, dingi wa kimataifa, Mtambuzi
....nasubiri akianza kuweka sura za wanaume.............
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,701
Points
2,000
Age
47
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,701 2,000
Mtambuzi umesema hajiami kwasababu ya sura yake kuwa ndefu ama kwasababu ya pozi lake?? binafsi leo nakupinga hebu fikiri kama aliatega pozi la picha akaonyesha macho ya kujihami kwa tafakuri nyingi je hajiamini??

kuiamini kwa mtu nijuavyo ni zazid ya sura ya mtu ni tabia ambayo iko katika matendo na maongezi zaid, na hii hutokana na ama na maumivu alowahi kuyapata mtu siku za nyuma ama aina ya malezi.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Mtambuzi umesema hajiami kwasababu ya sura yake kuwa ndefu ama kwasababu ya pozi lake?? binafsi leo nakupinga hebu fikiri kama aliatega pozi la picha akaonyesha macho ya kujihami kwa tafakuri nyingi je hajiamini??

kuiamini kwa mtu nijuavyo ni zazid ya sura ya mtu ni tabia ambayo iko katika matendo na maongezi zaid, na hii hutokana na ama na maumivu alowahi kuyapata mtu siku za nyuma ama aina ya malezi.
gfsonwin, mie napenda sana kupingwa.

Mimi nimesema kwama wanawake wenye sura inayofanana na huyo mwanamke kulingana na pozi lake na ndio sababu ya kuelezea muonekano wa sura, na sijasema huyo mwanamke aliyeko hapo kwenye picha.

sasa kama kaweza pozi kama ulivyosema hiyo haihusu, mimi nilikuwa natafuta nsura yenye pozi fulani kwa ajili ya ku support mada yangu.

Hujaona waigizaji wanavyoelekezwa watengeneze sura ili ifanane na mtu mwenye haiba fulani?

Mweh1
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Mie.umenikonfyuzi mdingi. Sasa ni wazuri ama sio wazuri? Waaminifu halafu tena wanadanganywa na wanaume?

Wapambe wa big brother africa, huyu anafanana na sheila, mshiriki wa kenya?

Well, nashukuru Mungu mie nafanana na jembe la ukweli, king of stories in east and central africa, dingi wa kimataifa, Mtambuzi
we nawe naona ushalanduka alfajiri.

Kwani watu waaminifu hawasalitiwi?
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,701
Points
2,000
Age
47
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,701 2,000
gfsonwin, mie napenda sana kupingwa.

Mimi nimesema kwama wanawake wenye sura inayofanana na huyo mwanamke kulingana na pozi lake na ndio sababu ya kuelezea muonekano wa sura, na sijasema huyo mwanamke aliyeko hapo kwenye picha.

sasa kama kaweza pozi kama ulivyosema hiyo haihusu, mimi nilikuwa natafuta nsura yenye pozi fulani kwa ajili ya ku support mada yangu.

Hujaona waigizaji wanavyoelekezwa watengeneze sura ili ifanane na mtu mwenye haiba fulani?

Mweh1
mbona sasa hapa umeeleweka tofauti na ulivyoielezea kwenye topic husika?? kuhusu pozi hilo kuwa na sifa hizo sina hakika so siwez kusema ni kweli ama uongo ngoja niangalie litratures zinasemaje kwanza
 
HorsePower

HorsePower

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2008
Messages
3,613
Points
1,225
HorsePower

HorsePower

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2008
3,613 1,225
Ni ngumu watu kukuelewa Mtambuzi, lakini kuna ukweli ndani ya hii mada ingawa hatuwezi kugeneralize kuwa ni kwa wasichana wote. Sura kama umbile la mtu, saa nyingine hubeba ualisia wa tabia ya mtu. Hamjawahi kusikia baadhi ya watu wenye sura za duara wana tabia hizi au wenye sura ndefu wana tabia hizi au wafupi wengi ni machachari au warefu wengi ni wapole na wataratibu?!
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,295,847
Members 498,410
Posts 31,225,258
Top