Wanawake wenye maradhi ya kuiba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wenye maradhi ya kuiba!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Apr 12, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wataalamu wa saikolojia wanalielezea tatizo hili kama tatizo la kiakili. Mtu mwenye tatizo au ugonjwa huu huwa anashindwa kujizuia au kuzuia kishawishi kitokacho ndani mwake cha kuiba, tatizo hili hufahamika kitaalamu kama Kleptomania. Lakini jambo la ajabu ni kwamba kitu hicho ambacho kinaleta ushawishi kuibwa ni kitu ambacho hakina thamani kifedha wala hakina matumizi yoyote kwa mwibaji.

  Hapa ni vizuri jambo hili nikaliweka wazi, kwamba, ninachozungumzia siyo tabia ya kuchomolea watu mifukoni au kuwapora mikononi. Hapa ninachozungumzia ni kuiba bila mwibaji kupanga kwamba leo au sasa hivi nijiandae kuiba hiki au kile. Baadhi ya wataalamu wa matatizo ya kiakili wanaamini kwamba, kishawishi cha kuiba kinapomjia mgonjwa huwa kinakuwa kama kitu kipya akilini mwake, yaani kinakua kitu ambacho hakitaki lakini hawezi kukiondoa au kukisimamisha.

  Ndipo pale unakuta mtu anafika nyumbani kwako na anajitahidi sana hadi anaiba hata kijiko kidogo cha chai, huku akiwa ni mtu mwenye uwezo wa kutosha. Ndipo pale ambapo unakuta mtu anafika mghahawani na baada kula huiba uma, wakati mtu huyo ana uwezo mkubwa kifedha. Huenda hata wewe umeshawahi kusikia au kumuona mtu mwenye tabia kama hii, ambapo mara nyingi huwa tunamwita mwizi. Kuna wakati unaweza kusikia, "Mwanamke yule ni mwizi kweli, tena anaiba hata vitu visivyo na maana na siyo kwamba ana shida, ila basi tu." Huenda mwanamke huyu anayeongelewa anakabiliwa na tatizo hili la Kleptomania, yaani ugonjwa wa wizi au udokozi.

  Kwa kawaida wanaokabiliwa na maradhi haya kama ambavyo nimebainisha, ni wanawake na hasa kuanzia umri wa miaka 36, na maradhi haya hudumu kwa wastani wa miaka 16. Hata hivyo kuna taarifa za kuwepo kwa wagonjwa kama hawa ambao walianzwa na tatizo hilo wakiwa na umri wa miaka mitano. Hakuna hasa ushahidi tatizo hili husababishwa na nini, lakini wataalamu wengi wanaamini kwamba linatokana na kuwepo kwa hitilafu kwenye kemikali ya ubongo iitwayo serotonin. Hii ni kwa sababu vidonge ambavyo huwa vinatumika katika kuondoa sononi vinavyofahamika kwa jina la Prozac, ambavyo huwa vinaongeza kiwango cha kemikali hii ya serotonin, vilitumika kwa wanawake wenye tatizo hili. Wanawake hao walipata nafuu kubwa.

  Wanawake wenye tatizo hili ni vigumu sana kwao kujenga uhusiano au ndoa imara kwa sababu wanaume wengi huwakwepa kwa kuogopa fedheha watakayoipata katika jamii. Mara nyingi huishia kuzalishwa na kutelekezwa. Ni pale tu watakapokuwa wamepona tatizo hilo ndipo watakaponusurika na adha ya kukimbiwa na wanaume.
   
 2. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Mimi sitachangia coz niko above 36yrs,nawaachia vikongwe mada yao.
   
 3. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Sorry wana JF,Niko BELOW 36YRS.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  is wamme wa mtu included?
  Basi wevi ni wengi zaidi.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mdame B hupo salama, soma hapo kwenye Bold nyekundu
   
 6. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  We acha tu! C unajua m-bongo akipewa mada ndefu huwa anasoma kichwa cha habari na paragraph moja ya kwanza tu.
  Asante mkuu kwa kunijuza!!
   
 7. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  I think hata kwa wanaume BUT Am not sure
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ni Kweli Mtambuzi tunao ushahidi wa Mbunge wa CCM Viti Maalumu ( Mbeya) Aliyekwapua Vijisabuni na Vijidodoki, Vijisoap Dish na Vijishampoo Katika Hotel Moja Arusha
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu, lakini wanawake ndio wahanga wakubwa wa tatizo hilo......................
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  He he he, basi kama hadi vile vidude vya hotelini vinahesabiwa hata wanamme wanao.
  Kuna munene mmoja alibeba visabuni vyote vya chumbani kwake kwenye hii hotel nayofanyia kazi.
   
 11. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Aha wapi! Hata nyie pia ni wahanga.
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  leo napita tu...........
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  This is mostly common to women ha ha ha wakiona vile viungo, vitaulo, vikandambili basi wanavitamaaani wakati viko hata Kariakoo tena kwa bei ya Kutupa
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Vinashawishi sana vile.
  Kuna mmoja mdada alibeba hadi taulo lile kuuubwa kabisa wakati ni mfanya kazi wa benk
  Aliniacha hoi.

   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mie kuna mabinti wawili nawakumbuka (walikuwa na kati ya umri wa miaka 15-20 hivi) miaka ya mwishoni mwa 80, walikuwa hawaishi kukamatwa kwa kuiba chupi za wenzao, yaani mpaka wakawa wanaogopwa mtaani.................... hata hivyo tatizo hilo lilikuja kuisha na sasa wameolewa na wana ndoa imara.
   
 16. b

  bebiwilli Member

  #16
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi na rafiki yangu ambaye ni best,ilikuwa ni siku ya kwanza kwenda naye kwenye harusi,loh 2po njiani kwenye gari 2narudi home si anachojoa uma na vijiko kwenye pochi, baadae namuuliza ananiambia eti kashazoea yeye na dada yake wakienda kwenye party lazima waibe vijiko,umma na glasi za wine,na hm kwao ni watu wenye uwezo kupitiliza.
   
 17. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Sounds like Bishanga alivyokupeleka vekesheni wapi kulee..??? LOL
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hao bila shaka watakuwa wameathirika na huo ugonjwa wa Kleptomania..............wanahitaji tiba na ushauri nasaha
   
 19. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Nnmmh........... niruhusu nidoubt....
   
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  He he he he, umejuaje?
  Yaani Byshernger ni mwizi wa mataulo hadi basi.

   
Loading...