Wanawake wengine wanawanyima waume zao unyumba

Wanawake wengine wanawanyima waume zao unyumba

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,270
Reaction score
29,939
Ijumaa iliyopita rafiki yangu mmoja alikuwa ameishaingia chumbani kulala. Kabla usingizi haujamchukua mkewe akaingia chumbani humokutoka bafuni alikokuwa akioga. Mara tu baadaya kuingia akatupa chini taulo alilokuwa amevaa na kubaki kama alivyozaliwa.

Akachukua losheni yake na kuanza kujipaka huku akiimba (na kukata kiuno taratibu) wimbo wa taarab 'pembe la ng'ombe mpaka hapo rafiki yangu akawa tayari ameshapandisha mzuka vibaya sana. Akavua pajama alilokuwa amevaana kulitupa pembeni.

Mwanamke alipomaliza kujipaka losheni akajitupa kitandani na kugeukia upande wa pili kana kwamba kitandani hapo hakuna mtu mwingine. Jamaa akamgusa kumuashilia mkewe ageuke. Kwaukali mamaa akasema"SIJISIKII" nyie wanaume mnatuona wanawake kama vyombo vya kuwastarehesha tu (sex machine),kwani huwezi kumpenda mtu kwa jinsi alivyo mpaka umbugudhi.

Jamaa kwa kujua hawezi kupata kitu, akajifunika shuka na kulala. Kesho yake (jumamosi) rafiki yangu huyo akamchukua mkewena kumpeleka restaurant maarufu 'fogo de chao' kula chakula. Mkewe akafurahi sana kwa chakula kitamu. Baada ya hapo jamaa akamchukua mkewe hadi mall kwenye duka maarufu la nguo na makolokolo yote (Nordstrom).

Akawa anamsaidia mkewe kuchagua nguo na mara kwa mara kumpeleka fitting room kujaribu. Baada ya muda msichana akawa amepata nguo nne alizozipenda sana. Akamuuliza jamaa nichukue ipi? Jamaa akamwambia "chukua zote nne, pesa sio tatizo" Pia akamshauri achukue pea mbili za viatu na handbag yakumechishia. Baada ya hapo wakaelekea kwenye sehemu ya perfum na vipodozi.

Mama akachagua perfum nzuri anayoipenda sana. Akachagua na hereni nzuri za kisasa ili amechishe na nguo zake. Wakati huo wote msichana alikuwa amefurahi sana. Alikuwa anatabasamu kila wakati na kumkumbatia jamaa hovyo. Hatimae, mamaa akamwambia rafiki yangu "sasa inatosha, lipia twende zetu nyumbani" Jamaa akamjibu " SIJISIKII kulipa.

"Kwa hasira mwanamke akamuuliza, wewe ndio umenileta huku, umeniambie nichague na ukanibebesha mizigo yote hii halafu unaniambia hujisikii kulipa? Kwa upole jamaa akamwambia"Nyie wanawake watu wa ajabu sana, yaani mnatufanya sisi wanaume kama chombo cha kutatua matatizo yenu ya kifedha na kuwanunlia vitu mnavyotaka. Kwani huwezi kumpenda mtu jinsi alivyo" mpakaumbugudhi? Kwa hasira mwanamke akatupa vitu chini na kuondoka.

Tangu siku hiyo neno 'SIJISIKII' likawa halitamkwi tena.
 
nimependa hadithi yako, ila ndo walivyo wenzetu hao
 
Uuuuuu!!!! mweee, Sasa ndio nini kamdhalilisha dada wa watu, na yeye angemjibia chumbani. khaa!
 
Eeeeeh safi sanaaaaaa....
Lesson learned, class dismissed.
 
Rafiki yako kakosea.Jinsi unavyomfurahisha mwanamke,ndivyo atakupa mapenzi vizuri.Yeye angelipia hizo bidhaa,halafu angekubali kurudi nyumbani kama alivyoombwa,angefurahi sana siku hiyo
 
Back
Top Bottom