Wanawake wengine hawajui kusamehe

Daaaa! Nawahurumia watoto hawataishi maisha ambayo baba yao alitamani waishi.
 

Inategemea na makosa ya huyo roby, simlaumu mkewe hata chembe. Kumsamehe mtu haimaanishi kila kitu kinajirudia kama hakijatokea kitu anaweza kuwa amemsamehe lakini hataki tena kujiweka matatizo aliyoyapata ndo maana aligoma kurudi kuishi nae. Naona wanawake wa msimamo hivi ndio tunaowahitaji katika jamii iliyojaa ukimwi na maradhi mengine kama HPV. Ingikuwa ndio mara ya kwanza tungesema hajui kusamehe, alimpa nafasi nyingine nayo akifanya jambo ambalo mwenzie hawezi kuvumilia. Hata siku moja kitu ambacho wewe unaona kidogo na yeye ataona kidogo.
Wanaume mjifunze, sumu ya mapenzi ni maudhi. Mnawaona wanawake mapoyoyo wanapowasamehe, you think they are too weak
 
Ataweweseka maisha yake yote yaliyosalia, mikosi itamuandama mpaka kwenye kucha, alikuwa shujaa kwa wanae lakini sasa ni sawa na jambazi.

Simpendi na afadhali simfahamu

Mi nampenda bureee huyu Mrs. Roby. Ana msimamo.
Inawezekana kwa mawazo yake alipima risk zake kwa kurudiana na roby akilinganisha na asiporudiana nae.
 

Kikubwa haujui chanzo cha mgogoro wao,nakubaliana nawe si kila jambo linaweza sameheka.
 
Marehemu Robison

Apumzike kwa amani lkn mkewe hakumshikia steering wheel wakati anapata ajali. Mkewe asilaumiwe, jamii inaona makosa ya mwanamke hata akikosewa na akiamua kwa ajili yake mwenyewe.
 
Mi nampenda bureee huyu Mrs. Roby. Ana msimamo.
Inawezekana kwa mawazo yake alipima risk zake kwa kurudiana na roby akilinganisha na asiporudiana nae.

Msimamo ungekuwa + hata mimi ningemuunga mkono, kumbuka kuwa msimamo huo unapingana na maelekezo ya muumba wetu. Amewaleta watoto duniani kusota au kunyanyasika kwa kusimamia ushetani.
 
Mwenyezi mungu ampumzishe kwa amani, ukishaingia kwny ndoa uvumilivu, kusamehe ni vitu vya muhimu ukizingatia tayari unawatoto, kina mama tunatakiwa tuwe wavumilivu japo inategemea na kosa lenyewe. Kuna mengine si ya kuvumilia.
 
Msimamo ungekuwa + hata mimi ningemuunga mkono, kumbuka kuwa msimamo huo unapingana na maelekezo ya muumba wetu. Amewaleta watoto duniani kusota au kunyanyasika kwa kusimamia ushetani.

Wewe mkeo akiwa analala na kila anayemuona ukajua akakuomba msamaha ukamsamehe halafu ndani ya mwaka ukamfumania hali ukijua kuna ukimwi utamsamehe na kumrudia na kuwa nae kinyumba? Inawezekana ndo mazingira yaliyomkuta huyo dada, na kuna wanawake wana kinyaa vile vile hawezi kuvumilia zaidi. Utamlaumu wakati ulipewa nafasi, hata maneno ya BIBLIA yanasema watu wasiachane isipokuwa kwa sababu ya uzinzi na hili ndio janga la wanaume wa kizazi hiki.
Ushetani uko wapi hapo? Nani atawanyanyasa watoto mikononi mwanamke mama yao?
 
Toa Mfano wa jambo lisilosameheka......maana hakuna kosa lisilosameheka isipokuwa kumkufuru Roho wa Mungu.

Haya ni anayosamehe Mungu unayoongelea, ya wanadamu kwa wanadamu ukubwa wa kosa unategemea aliyetendewa.
 
PesaNdogo kula likes laki 8! U nailed it! Tunasikia one side story!
Mwanamke ni mstahimilivu na mwenye moyo wa huruma! Ila kwa suala la uzinzi hata mimi ningemsamehe lakini ndiyo ungekuwa mwisho wetu!
Sijawaona mahala mwanaume anaweza samehe mkewe akiwa mzinzi tena wa kijirudiarudia NEVER!
Mjifunze na ninyi kusamehe wake zenu wazinzi ndipo mtunyooshee vidole na sisi tusamehe!
Eti kamgogoro kadogo kapi????? mbona hukasemi???
Hata kama angesamehewa ilikua ni siku yake ya kufa tu! Siioni kipya hapo?
 
Last edited by a moderator:

Thank you! Tena apumzike kunakostahili kutokana na matendo yake!
 
Ni heri kujishusha na kuwa na moyo wa msamaha kuliko kukaa na chuki moyoni.
 
nina tatizo la kutokusamehe
Mungu anisaidie
yaani hata kitu kidogo tu napata wakati mgumu kusamehe,

Aisee tupo pamoja Mungu atusaidie jamani, ila mimi uniache hadi hasira zipungua kama siku 3 au 4 hivi, basi naachilia ila sometime nakumbuka du!
 
Haya ni anayosamehe Mungu unayoongelea, ya wanadamu kwa wanadamu ukubwa wa kosa unategemea aliyetendewa.

Haya haya ya wanadamu hakuna kosa lisilosameheka hata liwe kubwa kama mlima Kilimanjaro nasema hakuna, ni kuutune moyo wako na akili yako tu kwa lile ulilotendewa,kuna Baraka kubwa sana katika kusamehe na ni mateso makubwa sana kuwa na moyo usiosamehe,Siku zote anayeteseka ni yule asiyesamehe kuliko yule anayehitaji kusamehewa,ukishi katika kanuni ya kutangaza msamaha hata kabla hujaombwa msamaha ni nzuri sana Siku zote utakuwa mtu mwenye furaha na amani na utaishi mwenye heri siku zote za maisha yako.

Katika kesi hii Labda kiwatengu tuambie bidada hakusamehe kabisa au alisamehe akakataa kurudiana naye?
 
Last edited by a moderator:
Toa Mfano wa jambo lisilosameheka......maana hakuna kosa lisilosameheka isipokuwa kumkufuru Roho wa Mungu.

Labda niweke vizuri hoja yangu,kwenye ndoa kuna mambo mengine ambayo hata kanisa linatoa baraka za katika kuachana yaani kutoa talaka japo MUNGU anachukia talaka(soma malaki 2:16a) lakini kwa ajili ya uasherati talaka imeruhusiwa kibiblia(soma Mathayo 5:32 na 19:9).Sijajua tatizo la hawa ndugu ila kwa mkutadha huu Dada hasa Kama yeye alishasamehe Mara ya kwanza kisha jamaa akarudia tena yale yale,anaweza kugomea kusamehe.Kupigiwa inauma sema labda haijakukuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…