Wanawake wengi wasomi au wenye kipato kizuri hawadumu kwenye mahusiano!


Wewe naona mbado sana...safari bado ni ndefu ila naamini tutafika tu!


Ni kweli ila hilo linawezekana endapo wanaume wataweza kujihakikishia kuwa wanaju vizuri kile wanachokitaka kwenye mahusiano. Wengine wapo wapo...Models wanawataka, wanyange twende tu...wasomi wenye kazi nao pia....! Katika mazingira kama hayo lazima watakuja na vijisababu vya kipuuzi puuzi kama hivi vinavyotolewa hapa!


Tupe mfano halisi basi wa ndoa yako na kitu gani umefanya kukwepa hizo karaha. Wengine tunasema wazi tu kuwa ndoa inategemea na shopping list yako na kama uliiandaa kwa umakini na kuifanyia kazi!
 
wanasumbuaje?wanakuwaje kama wanaume?..nielimishe kwahili mana napenda niolewe na mtu niliyemzidi kisomo hadi umri...

....BJ.... umemsoma babu DC lakini alivyonitabiria...........
hebu naomba umsome hapa chini labda utabadili mawazo yako kwa paka weusi.


Kama hayo yote yametoka moyoni basi Babu DC anakutabilia kuwa utakuwa mume mwema. Kwa wale wanaotafuta..you are true husband material!

Wengine hayo yote tunayafanya practically na ndio maana tunawashangaa baadhi ya wanaume wanaofikiria kama vile ni mwaka 1960 wakati tunaelekea mwaka 2011!

Mungu atakuwa na nawe na familia yako itakuwa na baraka tele...!!!!!
"WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE....LOOKING BEYOND THE 31 OKTOBA 2010 LANDMARK"

Retired Maj Gen DC (1947)...dc@jamiiforums.com

 
pole anza kujiamini kama mwanaume,na yeye atakuheshimu...
ukiwa hujiamini hata ukipata mwanamke ambaye hajasoma atakuendesha tu...:teeth:

we fab kwa nini umeiba mawazo yangu? mzima lakini
 

Ndo hapo kenye "Nyekundu" (Empty-Tupu) asema, kichwa huvimba!!!!!
 
wasiosoma balaa. Wakisoma balaa. Wakiwa hawana kitu balaa. Wakiwa na fedha balaaaaa. They are complicated like criket and sometimes bitter like osokoni tree


mfamaji umenichekesha mwe JF raha umeongea kwa hisia sana yamekukuta nini baba, jamani tukubaliane tu kwamba ujeuri ni tabia ya mtu na kingine ni tabia ya wanaume kutojiamini jiamini kama mwanaume ucjali usomi wake (ila sio uwe kiburi) hiyo ndio silaha tosha
 

babu that's why i love you mwe
 



ni kazi zipi hizo zinazofanywa na wanaume tu, wanawake hawawezi kuzifanya
 
Twanga kotekote - Mwanamke akikusumbua tafuta "small house" - small house akileta tabu nenda "ohio street" - acha kuumiza kichwa kwa sababu ya mwanamke - there are so many "out there"
meant this one.
 
Hivi kwanini wanawake wengi hasa wa kitanzania waliosoma ni wasumbufu katika ndoa. Wakisha olewa nao wanakuwa kama wanaume!!! Tabutupu hii!!!!
Unamaanisha usumbufu katika ndoa ni tabia ya wanaume? So kina dada wakisoma ndio wanakua kama wanaume? Na wanaume ni tabia yao kwa ujumla au wanaume waliosoma tu?
 
Mtoa mada, naheshimu mawazo yako sana. Hata hivyo naomba nikuulize:
1. Kwani "wanaume" wakoje hadi uone kero kwa wanawake wasomi kujaribu kuwa kama wao?
2. Wewe mwenyewe umeoa? Kama umeoa mkeo ni msomi? Kama ni msomi kakukera kwa sababu ya usomi wake? Je angekuwa hajasoma asingekukera?

Nionavyo mimi umeingia katika mkumbo wa wasioelewa.Kweli mwanamke msomi au mwenye uwezo huwezi kumrusharusha kama kishada. Huwezi kumtishia au kumgandamiza kama ambavyo ungefanya kwa huyu ambaye hajasoma au asiye na uwezo kujimudu hata kwa mahitaji madogomadogo.

Mwanamke tegemezi ( wengi hawajasoma) akipata mwanaume mnyanyasaji ni full mateso na utumwa! Nadhani your ideal woman is the one who is ready to KB you!

Keep looking if you are still "available".
 

WOS,

Mchango wako katika hii issue ni highly valued. Mimi ni mwanamume na nimewambia sana wenzangu kuwa katika hili suala tatizo kubwa ni wanaume wenyeye. Na kikwazo kikubwa na kitu wanachoogopa kama ukoma ni hapo kwenye red (uwezo wa kujikimu kwa kila kitu bila kuomba omba kutoka kwa mume)!
 
Kazi ipo, naona hapa ni mkorogano kabisa. Sio kwamba wanaume wanawanyanyasa wanawake ila inapotokea mwanamke ana rank sawa au kamzidi kidogo ndipo matatizo huanza, wasiwasi, mashaka, nani aogngoze familia, na mkuu etc. lakini kwa mwanamke mwenye busara na mwanaume mwenye busara haya ni mbambo madogo sana na wala hayapaswi kuzungumzwa .
 
Sometimes ni kweli,

Wanawake waliosoma huwa wanasahau majukumu yao muhimu kama mama ndani ya familia na kuanza kujilinganisha na wanaume...! Kuna kusahau kwamba wanaume ndio kichwa cha familia na kiongozi wa nyumba...! Wanawake waliosoma hilo hawalijui...!

Wanwake waliosoma sana huwa ni kero sometimes, hujisahau sana na kusimama kifua mbele au kutunisha kifua sawa na mwanaume...! Matoke ya kudai hiz haki zao huwa ndio chanzo cha kuleta migogoro ndani ya familia...!

Chondechonde dada zetu...! Msijisahau na elimu yenu na vyeo vyenu huko makazini mkasahau kwamba unapokua mama ndani ya nyumba kuna ambaye yupo juu yenu...! Mumeo...!
 
Jamaniiii wana JF, wanaume wengi wanakwepa kuchumbia wanawake wasomi au wenye kipato kikubwa, hata kama wana sifa zote za upendo wa dhati na uaminifu, ni kwanini hasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…