Wanawake wengi wanaponzwa na tamaa.

mr vata

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
465
616
Habari jamani...
Leo nataka kushare nanyi kisa kimoja ambacho kilinitokea jana.

Jana muda wa saa moja au moja na nusu jioni nilikua narudi nyumbani kutoka katika shughuli zangu. Mimi ninafanya biashara kariakoo pia ofic yangu ni ya huduma hivyo mara nyingine nikiwa na kazi huwa naweza kutoka hata saa tatu usiku.

Kwa kawaida huwa napandia gari karume nageuza nalo ili nipate siti, nafikiri hili wengi wanalijua. Nilipopanda gari nikaenda kukaa siti ya upande wa mbele, yaani ukiingia badala ya kurudi nyuma unaenda kule kwa dereva.

Nilikaa siti ya nyuma kutoka mbele pale katikati, mbele yangu alikaa kaka mmoja, upande wa kushoto kwangu (yaan dirishan) nilikuta amekaa mrembo mmoja matata ambapo kwa mbele kabisa kushoto ( dirishani pia) alikaa mwanamke ambae baadae nilikuja kugundua wapo pamoja na huyu mrembo wa nyuma.

Hawa wanawake walikua wanapiga story na kuonyeshana picha kwenye simu muda wote wa safari. Yule mwanamke ambae alikua kando yangu alikua amekaa kihasara flani hivi... Yeye ni mweupe mrefu flani na alivaa gauni jepesi.

Sasa kutokana na kimo chake na vile alikaa kwenye siti fupi kidogo ikasababisha miguu yake inyanyuke flani hivyo lile gauni lake jepesi likawa limepanda juu na kuyaweka nje mapaja yake matamu, hakujali!

Mimi kama mwanaume kiukwel nilihamasika lkn nikajifanya kupotezea kwa kuhofia maringo na nyodo za hawa wadada wazur wazur, maana kwa jinsi ninavyojijua mimi si miongoni mwa wale wanaume wanaoitwa ma handsome na huwa napata wakati mgumu sana kujiweka karibu na warembo kwani nimeshakula za uso mara kadhaa, nikaona isiwe shida nikawa nameza mate tu huku nikiombea tufike upesi .

Gari ilipofika quality centre ( mtava) tukaanza kukutana na adha ya foleni, ukizingatia na ujenzi unaoendelea pale tazara basi na gari ikazimwa kabisa.
Kukata makali ya foleni nami nikatoa simu ili nichat kidogo. Wakati naendelea kuchat nikagundua dada mrembo kando yangu amemakinika na simu yangu, nilikua nina iphone 5s.

Baada ya muda akashindwa kuvumilia na akaniuliza ile simu aina gani nikamtajia, pia akauliza bei yake dukani pia nikamwambia. Yeye alikua anatumia itel moja pana hivi.

Kutokea hapo nikamuona bidada anaanza kujiweka karibu na mimi basi nami sikulaza damu, story zikaanza na ikafika point akaiomba ile simu ili aishike na kuiangalia vzr, nami nikampa. Katika kuzoeana kule kwa ghafla mimi nikajiongeza, nikaomba namba na mrembo akaandika fasta kwenye iphone 5s yangu.

Kimoyo moyo nikafurahia hali ile japo nilijua yule mrembo alivutwa zaidi na simu yangu na sio mimi. Mara foleni ikatembea, tukashukuru. Wakati safari inaendelea mrembo na mwenzake mbele story zikanoga, wakapiga story mbalimbali na ghafla wakawa wanaongea kuhusu watoto wao.

Katika story hizo nikagundua mrembo kando yangu kumbe ana watoto wawili, nikashangaa kidogo lkn umakini wangu ukaongezeka, mara wakahama kutoka kwa watoto wakaanza kuwaongelea waume zao, nikachoka!

Kumbe mwanamke ana mume? Nikawa najiuliza kuja kushituka konda anauliza wakushuka kwenye kituo changu, nikashuka na kumuaga mrembo maana yeye alikua anaendelea.

Kiukweli yule mwanamke ni mzuri na alinivutia sana, lkn nikaamua kufuta ile namba bila kumpigia kwa sababu nilijua ni mke wa mtu!
Mpaka leo najiuliza, hivi wanawake wanaridhika na nini hasa? Sipati jibu.
 
Habari jamani...
Leo nataka ku share nanyi kisa kimoja ambacho kilinitokea jana.

Jana muda wa saa moja au moja na nusu jioni nilikua narudi nyumbani kutoka katika shughuli zangu. Mimi ninafanya biashara kariakoo pia ofic yangu ni ya huduma hivyo mara nyingine nikiwa na kazi huwa naweza kutoka hata saa tatu usiku.
Kwa kawaida huwa napandia gari karume nageuza nalo ili nipate siti, nafikiri hili wengi wanalijua.
Nilipopanda gari nikaenda kukaa siti ya upande wa mbele, yaani ukiingia badala ya kurudi nyuma unaenda kule kwa dereva. Nilikaa siti ya nyuma kutoka mbele pale katikati, mbele yangu alikaa kaka mmoja, upande wa kushoto kwangu (yaan dirishan) nilikuta amekaa mrembo mmoja matata ambapo kwa mbele kabisa kushoto ( dirishani pia) alikaa mwanamke ambae baadae nilikuja kugundua wapo pamoja na huyu mrembo wa nyuma.
Hawa wanawake walikua wanapiga story na kuonyeshana picha kwenye simu muda wote wa safari.
Yule mwanamke ambae alikua kando yangu alikua amekaa kihasara flani hivi... Yeye ni mweupe mrefu flani na alivaa gauni jepesi. Sasa kutokana na kimo chake na vile alikaa kwenye siti fupi kidogo ikasababisha miguu yake inyanyuke flani hivyo lile gauni lake jepesi likawa limepanda juu na kuyaweka nje mapaja yake matamu, hakujali!
Mimi kama mwanaume kiukwel nilihamasika lkn nikajifanya kupotezea kwa kuhofia maringo na nyodo za hawa wadada wazur wazur, maana kwa jinsi ninavyojijua mimi si miongoni mwa wale wanaume wanaoitwa ma handsome na huwa napata wakati mgumu sana kujiweka karibu na warembo kwani nimeshakula za uso mara kadhaa, nikaona isiwe shida nikawa nameza mate tu huku nikiombea tufike upesi .
Gari ilipofika quality centre ( mtava) tukaanza kukutana na adha ya foleni, ukizingatia na ujenzi unaoendelea pale tazara basi na gari ikazimwa kabisa.
Kukata makali ya foleni nami nikatoa simu ili nichat kidogo. Wakati naendelea kuchat nikagundua dada mrembo kando yangu amemakinika na simu yangu, nilikua nina iphone 5s. Baada ya muda akashindwa kuvumilia na akaniuliza ile simu aina gani nikamtajia, pia akauliza bei yake dukani pia nikamwambia. Yeye alikua anatumia itel moja pana hivi.
Kutokea hapo nikamuona bidada anaanza kujiweka karibu na mimi basi nami sikulaza damu, story zikaanza na ikafika point akaiomba ile simu ili aishike na kuiangalia vzr, nami nikampa. Katika kuzoeana kule kwa ghafla mimi nikajiongeza, nikaomba namba na mrembo akaandika fasta kwenye iphone 5s yangu. Kimoyo moyo nikafurahia hali ile japo nilijua yule mrembo alivutwa zaidi na simu yangu na sio mimi.
Mara foleni ikatembea, tukashukuru. Wakati safari inaendelea mrembo na mwenzake mbele story zikanoga, wakapiga story mbalimbali na ghafla wakawa wanaongea kuhusu watoto wao. Katika story hizo nikagundua mrembo kando yangu kumbe ana watoto wawili, nikashangaa kidogo lkn umakini wangu ukaongezeka, mara wakahama kutoka kwa watoto wakaanza kuwaongelea waume zao, nikachoka!
Kumbe mwanamke ana mume? Nikawa najiuliza kuja kushituka konda anauliza wakushuka kwenye kituo changu, nikashuka na kumuaga mrembo maana yeye alikua anaendelea.
Kiukweli yule mwanamke ni mzuri na alinivutia sana, lkn nikaamua kufuta ile namba bila kumpigia kwa sababu nilijua ni mke wa mtu!
Mpaka leo najiuliza, hivi wanawake wanaridhika na nini hasa? Sipati jibu.
We ni fundi wa kuandika, hela hiyo, ipo nje nje. Andika kitabu, utauza sana. Ni ushauri wangu kwako.
 
Ulimtamani,ukamuomba namba akakupa unamuona malaya. Je angekutukana ungemuona ana nyodo. Hivi wanaume huwa mnaridhika na nn hasa?

Tushajua unamiliki iphone hongera.
Kipi bora kwako! Kuonekana Malaya au kuonekana una Nyodo?
 
Back
Top Bottom