Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,938
Wanawake nawasalimu bila kuwasahau Wanaume wenzangu!
Vibinti vingi mjini na baadhi ya wamama ukikutana nao aidha sokoni, kwenye sherehe, chuo au mahali pengine unaweza ukahisi ni matawi ya juu. Anamiliki simu ambayo wewe Mwanaume wa kawaida hujawahi kumiliki. Anajitutumua kula chakula cha hali ya juu zaidi ya uwezo wake n.k.
Mdada mmoja ambaye najua analipwa laki kama 4 hivi nilimshangaa kumwona anamiliki simu ya laki 4.5. Kwakuwa namjua kuwa si kahaba nikamuuliza umepata wapi fedha ya kununulia hii simu akaniambia kuwa alikuwa anatunza fedha kidogokidogo kwa miezi kama 3 ndo akainunua.
Nilimwonea huruma sana. Utunze fedha kwa miezi ili ununue simu ambayo hauitumii kibiashara!!!
Mwingine alipolipwa fedha za upatu(mchezo) kaenda kununua simu karibu fedha yote. Hii ni tamaa.
Samahani kwa dongo hili. Najua mtasema kila mmoja na kipaumbele chake ila lazima tuishi sawasawa na kipato chetu. Unacheza mchezo ili ununue simu!!!!
Mkizoeana kidogo tu anaanza kukuletea shida zake, nani aliowaambia kuwa sisi Wanaume hatuna shida zetu? Tunazo ila tunavumilia na kutazama vipaumbele vyenye tija kwanza.