Wanawake wazuri hawafai kuolewa?

Wanawake wazuri hawafai kuolewa?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,640
MREMBO3-1.jpg

UNA dhana ipo hususan kwa wanaume wengi kwamba, wanawake wengi wazuri hawafai kuolewa.

Wanaishibisha hoja yao kwa kutoa mifano, kwamba wanawake wengi walioolewa na kutulia kwenye ndoa zao ni wale wa daraja la kati. Wanawaita wa kawaida!

Wanaamini kuwa, wanawake wa aina hiyo wana mambo

mengi. Wana dharau, wanaotolewa macho na wengi, wana jeuri kwelikweli.

Katika uhalisia mwingine, wanaume wengi wamekuwa wakiwagwaya wanawake wazuri. Wengine wamekuwa wakiwatumia kama chombo cha starehe.

Utasikia mwanaume akiwaambia wenzake ‘kwa uzuri ule unafikiri yule ni mwanamke wa kuolewa?’

Haamini kwamba mwanamke mwenye figa ya kuwashtua wanaume, anaweza kutulia na kuolewa. Matokeo yake, wanawake hao, hujikuta wakikosa soko la ndoa.

Bahati mbaya sana, kuna baadhi yao wenyewe wamekuwa wakikubaliana na hali hiyo.

Wanaamua kuwa wanawake wa aina hiyo. Waburudishaji au wachangamsha genge kwa lugha rahisi. Wanatumika kulingana na mahitaji ya wanaume.

Leo atakuwa na huyu, kesho atakuwa na mwingine maana ana uhakika. Akiachwa leo, kesho ‘ashamteka’ mwingine. Ni bandika bandua.

Wanafanywa wa maonesho

Wanaume nao wanawatumia huku wakiwa na akili kichwani. Kwamba huyu ni mwanamke wa kutamba naye mtaani. Ni mwanamke wa maonesho.

Mwanamke wa kwenda naye ufukweni au sehemu za starehe. Kigezo kikubwa anachokitaka mwanaume ni kuwatambia wenzake kwamba ana ‘kifaa’.

Anamtumia pale anapokuwa na fedha. Zikikata anarudi kwa mwenzi wake wa siku zote. Yawezekana kabisa akawa na mkewe, anamtumia yule kama sehemu ya burudani. Yupo wake wa maisha.

Utakuta mkewe anamsifu kwamba ni wa kawaida. Hana makuu. Yeye amepata, amekosa, anamshukuru Mungu. Anamheshimu sababu anajua ndiye mstiri wake. Ndiye anayemfaa katika shida na raha.
MREMBO2-1.jpg

Muhimu kujifunza

Mwanamke unapaswa kujitambua. Una kila sababu ya kujichagulia maisha ambayo yatakuwa na manufaa baadaye. Ukiamua kuwa chombo cha starehe, kweli utafanywa chombo cha starehe. Utavuna fedha nyingi kutoka kwa wanaume.

Watakubadilisha, watakupa kila unachotaka kutokana na umbo lako. Watakufurahisha lakini mwisho wa siku, umri nao utakutupa mkono.

Utakuja kushtuka umri umekuacha, unahitaji familia lakini humuoni wa kuzaa naye. Kila mwanaume ameshachukua hamsini zake na wewe mvuto huna tena.

Kuna maradhi. Yawezekana ukatumika na kujikuta umeingia kwenye matatizo makubwa ya afya.

Wakati huo hutamuona wa kukusaidia tena maana kila mmoja atakuwa anapambana na hali yake, kuilisha familia yake.

Ni aibu

Ni aibu mwanamke kufanywa chombo cha starehe. Kila mtu anakutumia halafu mwisho wa siku heshima yako itakuwa wapi? Wewe wanakutumia kisha wanarudi kwenye familia zao, familia yako wewe utaitengeneza lini?

Haohao wenye familia zao, wakishamaliza kukutumia, wataanza kukusema. Watakuona huna thamani. Watakufananisha na tambara la deki.

WAREMBO.jpg
Umbo lisikuzuzue

Mwanamke mzuri anafaa kuolewa. Kikubwa ni kujitambua. Elewa kwamba, kuna maisha nje ya umbo na sura yako.

Kuna kutumika na kuachwa solemba. Jitambue. Jiheshimu na yatafakari maisha baada ya uzuri.

Wapo wazuri wengi tu wameolewa. Wametulia. Wanaheshimu ndoa na maisha yao ni mazuri. Jitathmini, acha kutumia muda wako vibaya. Unaweza ukawa mzuri na ukaolewa.

Maisha yana maana kama utatulia na uzuri wako, ukaijenga familia bora.

Ndoa ni heshima

Unapokuwa kwenye ndoa, mwanamke unaheshimika. Unakuwa na thamani mbele ya jamii inayokuzunguka na hata familia. Jitulize. Vaa mavazi ya staha.

Thamini utu kuliko mali. Thamani ya kuwa mwanamke itaongezeka kama utakuwa mrembo, mzuri lakini unayejiheshimu.

Kataa kufanywa mwanamke wa kiburudisho. Usikubali kutumika kwa namna yoyote.
 
....kutokujiamini kwawanaume ndo tatizo kubwa (mwanaume haamini ka mdada mzuri atakuwa wa kwake mwenyewe....) pia wanaume wengi wanapowatongoza wadada wazuri hawatumii uhalisia wa maisha yaooo.......wanatumia gia namba 6 ili hali uwezo wake ni gia namba 2/3. Baada ya kumfanikiwa kumpata/kufunga pingu za maisha mwanaume hawezi endeleza gia namba 6 anarudi gia namba 2/3...Mdada mzuri matunzo yanakosekana anaanza wazaaa vipoozeoo vya ....
 
wema kaolewa???
 
Wanaolewa ila na watu wenye pesa kama Dr Machache au cheo kama ex minister, mh Nyalandu.
 
Binafsi hilo ulilolisema halipo akilini mwangu.

naamini mwanamke ni mwanamke.

halafu jamii naona kama zinatofautiana...Kwenye jamii zingine uzuri sio kigezo cha mwanamke kuringa. sijui nitumie lugha gani.

mfano. Bongo chura ni habari ya mjini. ila sehemu zingine karibia kila mwanamke anachura..sio ishu...hata hawajui kuzishangaa.
 
mwanamke mzuri ni wa kwako tuu....... wengine ni fahari ya macho.....
 
Hata bure sioi mwanamke kama Uwoya na wengine wa sampuli hiyo. Ya nini kujitafutia magonjwa ya moyo, jaribu kudate na mdada mzuri utaipata habari yake
 
....kutokujiamini kwawanaume ndo tatizo kubwa (mwanaume haamini ka mdada mzuri atakuwa wa kwake mwenyewe....) pia wanaume wengi wanapowatongoza wadada wazuri hawatumii uhalisia wa maisha yaooo.......wanatumia gia namba 6 ili hali uwezo wake ni gia namba 2/3. Baada ya kumfanikiwa kumpata/kufunga pingu za maisha mwanaume hawezi endeleza gia namba 6 anarudi gia namba 2/3...Mdada mzuri matunzo yanakosekana anaanza wazaaa vipoozeoo vya ....
Tatizo la hao wanawake wanaoonmekana wazuri ni kwamba wanaamini uzuri wao
- unapika
- unafua
- unawafanya hata wakiachika wataolewa tena

Kifupi wengi wanaamini unatekeleza majukumu yote ya ndoa
 
Wanasema kuwa na mwanamke mzuri au kumuoa ni sawa na kupanda miwa karibu na shule ya msingi, lazima iliwe tu,

kwa nini tupigishane presha bure, unajua ukishakuwa na mwanamke mzuri, mrembo muda wote unahisi unaibiwa tu.

Mim uwaambia kuwa siyo wazuri ili wasijione wako hvyo, sipendi kabisa kusifia.
 
Back
Top Bottom