mi kiingereza nakifaham kwa mbaal lakin hiki chako mh!!! nadhan hyo sentens i mean heading ina walakin!
aliyekuambia tunafata uhandsam nani????
yanaangaliwa yaliyomo yamo?kama yamo hata ukiwa na sura ya ngamia.......
mi kiingereza nakifaham kwa mbaal lakin hiki chako mh!!! nadhan hyo sentens i mean heading ina walakin!
Bado hujajibu mnataka niniii
Mkuu ukitaka kumulewa mwanamke subiri aje kwako utamjua tu
Naandika hii hoja nikitafuta majibu yakinifu na ya msingi kutoka kwa wanawake pia wanaume wenye majibu sahihi uzi wangu nimeuliza wanawake wanataka nini? Maana nimeangalia katika hili nimeshindwa kupata majibu. Case study yetu ya swali hili itamlenga mke wa pili wa rais wa zamani wa Gabon Judith Lucien Bongo mwanamke huyu alikuwa mtoto wa Rais wa Congo Brazaville Rais Denis Sassou Nguesso akiwa msomi kakobea kwenye taaluma ya udaktari na pia ni mwanamke mzuri kwelikweli aliamua kuolewa na mwanaume anayemzidi takribani miaka 30
Pamoja na kuwa ni mtoto wa Rais Denis Sessou Nguesso kakulia kwenya mali na madaraka pia ana taaluma na ni mzuri anaweza olewa kwa kugombaniwa ukizingatia ni mtoto wa president ambaye hakuwa na ukomo wa kutawala lakini bado aliamua kuolewa na Rais wa nchi jirani ya Gabon akiwa mke wa pili na aliyemuoa akiwa na miaka 8 zaidi ya umri wa baba yake na akimzidi Judith miaka 29 na si kwamba ni handsome bali wa kawaida mwenye kimo cha futi 4 11" hata futi tano hafiki
Kwanini afanye vile? Angekuwa mtoto wa masikini tungeelewa, angekuwa hana taaluma tungeelewa, angekuwa fukara tungeelewa, baba yake asingekuwa rais tungeelewa yaani kwanini aamue kuolewa na mzee vile kwa sababu tu mmewe ni Rais wakati na baba yake ni rais pia na kakulia ikulu? Jamani naomba majibu yasiyo na mzaha nijue psychology ya hili swala ni nini haswa jibuni kwa kadri mjuavyo. Ahsanteni
Kwa hii stori fupi mi.bado jibu nsona ni pesa na cheo kwan huyu mwanamke kamkubar huyo mzee jiri ya pesa na cheo alchonacho ukiachana na cha baba ake.
Angekua kaenda kwa mzee fukara swali lingekua gumu lakn kwa hili jibu tunapata ni pesa na madaraka
Mkuu issue yangu ipo kwenye title ya uzi wako. Sehemu ya kiswahili ipo wazi na inaendana na thread yako vizuri. Sehemu ya pili maana yake ni kwamba wanataka wanawake wa aina gani. Bila shaka uki refer wanaume. Kama hiyo ndiyo ilikuwa maana, basi kwenye thread hujaligusa. Kama ilikuwa msisitizo tu toka kiswahili hadi kiingereza, then ingekuwa What do women want?
Nikirudi kwenye maada, kisaikologia namwelewa huyo dada. Kwa sifa na familia yake angetaka kuwa Rais wa nchi! Labda aliona ingekuwa ngumu. Kitu cha karibu zaidi ilikuwa kuwa mke wa Rais! Labda alikuwa na ndoto za kuurithi urais huo!
mm nataka pesa yaan kila ninachohitaji nipate.security and love.
Wanawake mnataka nini = what women do they want... kwa hisani ya dikshenari ya kipare. Bila kuweka kimombo tungejuaje kaenda shule? ushasoma headings za hadithi za shigongo? unaangalia bongo movies? ndo ujue watanzania tumekuwa watumwa wa lugha ya watu, afu bahati mbaya sana hatuijui kiviiile...
Wanawake mnataka nini? Kwangu mimi nlishaelewa swali, sikuhitaji tafsiri ya kimombo wakati hoja yenyewe imeletwa kwa kiswahili.
Turudi kwenye mada, eti flora, we huwa unataka nini ukiacha mgegedo na mapesa?
mi kiingereza nakifaham kwa mbaal lakin hiki chako mh!!! nadhan hyo sentens i mean heading ina walakin!