Wanawake wanaongoza kwa kuwa na plan B katika mahusiano

Wanawake wanaongoza kwa kuwa na plan B katika mahusiano

Chimps

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
559
Reaction score
356
Nusu ya wanawake huwa na mpango mbadala ama wa kando ambao wanaweza kukimbilia iwapo uhusiano wao utaharibika.Utafiti uliofanywa miongoni mwa wanawake 1000 uligundua kuwa asilimia kubwa imeweza kuwaweka wanaume mbadala pindi tu uhusiano walionao unapoharibika.

Cha kushangaza ni kwamba wanawake waliomo katika ndoa huwa na mpango mbadala ikilinganishwa na wale walio katika uhusiano wa kawaida.Pia imebainika kuwa mpango huo wa kando huenda akawa rafiki wa zamani ambaye amekuwa akimpenda mwanamke huyo.

Wengine huwa wapenzi wa zamani ama hata mume waliyeachana naye,rafiki ama mtu ambaye walikutana katika eneo la mazoezi.Utafiti huo ulifanywa na kampuni ya utafiti wa mtandaoni wa Onepoll.

Je, unakubaliana na utafiti huu

Chanzo: Utafiti:Wanawake huwa na mpango m'badala - BBC Swahili
 
Naanza kumchunguza wakwangu
 
Kwa kiasi kikubwa viwango vya upendo ndani yetu huimarishwa na yale wanayotutendea wale tuwapendao na vile vile mioyo yetu huchoshwa na maudhi kutoka kwa wale tuwapendao popote penye penzi la dhati usaliti ni msamiati mpya kabisa miongoni mwao kwani wenyewe huona raha kuwa pamoja..hujiona kama wapo paradiso na hakuna mwingine atakaye muhitaji zaidi ya yule aliye ndani ya moyo wake.

Lakini hali hubadilika mara tu penzi linapogeuka raha kwa anayetoa na kero kwa anayepewa hali ambayo huambatana na maudhi ndani yake yanayo ambatana na maumivu makali ya moyo ambapo humpelekea mjeruhiwa kutafuta tiba na nafuu na hapo ndipo inapopatikana fikra za plan B kwani muda mwingine penzi huitaji malezi ili liweze kustawi na kunawiri kinyume na hapo penzi hufa kifo cha kushangaza.

TRUE LOVE LAST LONGER.
 
KikulachoChako

Mkuu maudhi ndio yanayoharibu mahusiano,mtu anachoka kuudhiwa kusiko na msingi uvumilivu pia wengine hatujaumbiwa...... hivyo basi akitokea mtu anayekuweka sawa ktk vitu vihusuvyo mapenzi ndio hizi zinazoitwa plan B
 
Last edited by a moderator:
Aiseeeh! Kautafiti haka kanaweza kuwa na kaukweli fulani hivi ila sina uhakika zaidi.
 
MankaM

Lakini mbona hata mkiungana na hizo plan B hamtulii nazo?
Siku zote mtazamaji wa mpira haoni ugumu anaoupata mchezaji yeye anaona kuwa mchezaji hajui kucheza . lakn huyo mtazamaji ukimwingiza ndan ya uwanja ndipo atakapoona kuwa kumpe mpira ni mgumu.
 
Last edited by a moderator:
mkuu maudhi ndio yanayoharibu mahusiano.. mtu anachoka kuudhiwa kusiko na msingi uvumilivu pia wengine hatujaumbiwa...... hivyo basi akitokea mtu anayekuweka sawa ktk vitu vihusuvyo mapenzi ndio hizi zinazoitwa plan B
Hata hili neno nalo , ila kukosa uvumilivu ni excuse ya ki.......
 
Mgirik

Tafakari chukua hatua mkuu jiangalie wewe na mwangalie mwenzako ujue unaishi naye vip ili hizi plan b zisiwepo
 
Last edited by a moderator:
Ila kusemakweli plan B zinasaidiaga kupunguza maumivu...
 
Comments za K tatu nlizozisoma hapo zishaverify utafiti huu.
 
Junior. Cux

Weweeee jiulize kwani refa anaingia uwanjani na na red card
 
Last edited by a moderator:
naanzaje kukuvumilia wakati sipati kile nachotaka??? malumbano hayaishi wanaume mnamasimango kama wewe ndio usiseme
Kama mimi tena?....duh! Aiseeee!
Jitahidini mvitulize, Mwenyezi Mungu kakulinda mpaka hapo na maradhi na majanga mengi sana usitegemee ataendelea kuwa upande wako daily.
 
weweeee jiulize KWANINI REFA ANAINGIA UWANJANI NA RED CARD

Ha ha ha haaa you are very smart Evelynechumvi. True mpira ni burudani na starehe why redcard? Redcard ni preoaredness for any negative suppliese so is plan B
 
Back
Top Bottom