Wanawake wanaochelewa kubeba ujauzito waonywa

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,357
Wanawake wanaochelewa kubeba ujauzito, wameonywa kuwa kuchelewa huko kunawaweka hatarini kuja kupata watoto wenye mtindio wa ubongo.

Mbali na hilo, pia wanaume wanaotafuta watoto wakiwa katika umri mkubwa wa zaidi ya miaka 60, nao wametajwa kuwa hatarini kupata watoto wa aina hiyo na wakiepuka hilo, watakosa uwezo mzuri wa akili darasani.

Taarifa ya daktari mkongwe nchini, Dk Ali Mzige aliyotoa wiki hii, amebainisha kuwa hali ya umri mkubwa wa wazazi wa kike na kiume, ndio chanzo kikubwa cha kuzaliwa kwa watoto wa aina hiyo, na siyo uchawi wala mazingaombwe.

“Naomba niweke wazi kwamba, mama mwenye umri zaidi ya miaka 35 kama ndio anaanza kuzaa kwa mara ya kwanza, Mungu aepushie mbali, lakini ana uwezekano mkubwa wa kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo.

“Mbali na hayo, pia kwa baba mwenye umri mkubwa miaka zaidi ya 60 na ushei, akitaka kutafuta mtoto uwezekano upo wa kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo.

Kwa hiyo ushauri wangu kwa wazee wenzangu tunaostaafu sasa, tulee wajukuu tusianze tena kutotoa vifaranga,” ameeleza Dk Mzige katika taarifa hiyo. Kwa mujibu wa Dk Mzige, kisayansi umri mzuri wa kuoa au kuolewa na kuzaa kupata watoto wenye afya nzuri, ni kati ya miaka 18 na 35 kwa pande zote mbili baba na mama.

Changamoto kijamii

Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo watoto hao, Dk Mzige alisema ni pamoja na unyanyapaa kutoka katika jamii kwa watoto hao pamoja na wazazi wa waliowazaa. Amesema kutokujua chimbuko la mtindio wa ubongo katika jamii, kumekuwa kukihusishwa na imani za kishirikina, kwamba mzazi amefanya kila awezalo, ili mwanawe awe na mtindio wa ubongo, ili apate mali na kutajirika.

Mbali na wazazi kuonekana kusababisha mtoto wao kuwa na hali hiyo kishirikina, Dk Mzige alisema watoto hao pia wamekuwa wakitengwa na jamii na wakikua hasa wanawake, hudhalilishwa kijinsia ikiwemo kubakwa.

“Wengi hunajisiwa na kubakwa na watu wenye akili timamu, kwa imani kuwa kufanya tendo hilo na mtu mwenye ulemavu, utapata utajiri na mafanikio mazuri katika shughuli zako,” alisema.

Changamoto kiakili

Alisema wanaozaliwa wakiwa na mtindio wa ubongo, huchelewa kukua kiakili na kimaumbile, ni wapole sana hawana fujo kama watoto wengine wanaozaliwa kikamilifu. Pia huchelewa kutambaa, kunyanyuka, kuzungumza na wanakuwa na misuli ambayo ni dhaifu haina nguvu ya kusukuma na kupiga mateke kama watoto wengine.

“Uelewa wao kiakili uko katika asilimia 50 (IQ), ukilinganishwa na watoto wa kawaida ambao wana uelewa na ufahamu wa asilima 100,” alisema Dk Mzige.

Dk Mzige pia alifafanua kuwa kama baba atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 60, kama mtoto hatazaliwa na mtindio wa ubongo, mtoto huyo kiakili atakuwa na kasoro endapo umri wa baba utakuwa umesogea na yeye bado anaendelea kupata watoto.

Aidha wanaozaliwa na tatizo hilo, magonjwa makuu yanayosababisha vifo kwao ni saratani ya damu (leukemia) na magonjwa ya moyo na wengi hawafikishi umri wa kuishi wa miaka 40.

Chanzo: http://www.habarileo.co.tz/index.ph...wanawake-wanaochelewa-kubeba-ujauzito-waonywa
 
Wait, sasa huyu daktari mbona ni kama anakinzana na ile imani ya kwamba watoto hurithi akili kutoka kwa mama zao?

Sasa kama ni hivyo (mimi sikubaliani na hiyo dhana kwani naamini mtoto anaweza kurithi kutoka kwa mzazi yoyote yule na hata vizazi vilivyopita), kama mama bado ni kijana hiyo hatari inatokea wapi wakati watoto hawarithi akili toka kwa baba?
 
mkuu katika Elimu ya Saikolojia, hususani tabia na akili.
Vitu hivyo viwili sio vya kurithi..
 
Well, kuna watu hapa wanadi intelligence ya mtoto inarithiwa kutoka kwa mama.

Inawezekana labda mtu mwenye mtindio wa ubongo anaweza pia kuwa intelligence.
 
Mtoto anarithi akili kwa mama...
Na hili la kuzaa na umri mkubwa kuwa na effect kwa mtoto si news...
Nimeshasoma article huko UK watoto wengi these days wanazaliwa na utindio wa ubongo sababu wamama wanazaa umri umeshaenda tokana na majukumu ya kikazi...

La baba eti mzee nae ana athiri mtoto ndo nasikia leo...
 
Una maana kuwa baba hawezi kuchangia katika kuzaliwa kwa mtoto mwenye mtindio wa ubongo?

Kwa watoto wote wenye mtindo wa ubongo watakuwa wameridhi kutoka kwa mama zao?

Tukienda mbali zaidi kama baba ni HIV positive na mama ni HIV negative wakijahimiana na mama kupata ujauzito, mtoto atakayezaliwa atakuwa na uhakika wa 100% wa kutokuwa HIV positive?
 
Baba akiwa HIV +Ve,Mama HIV -ve mtoto hawezi kuzaliwa na VVU labda kama mama alipima akiwa yupo kwenye window period na mtoto akapata michubuko ya kugusana na damu ya mama.
Otherwise yupo salama.

Na hata mama akiwa HIV +Ve bado kuna uwezekano mkubwa tu mtoto akazaliwa bila maambukizi
 
Right. So, can HIV positive man donate sperms?

Kama ungekuwa ni mwanamke au assuming wewe ni mwanamke ungekubali kuwekewa sperms ambazo zimekuwa donated by HIV positive man?
 
HIV ina uhusiano gani na akili?
Unless unataka kusema akili iko kwenye damu...lol

Una maana kuwa baba hawezi kuchangia katika kuzaliwa kwa mtoto mwenye mtindio wa ubongo?

Kwa watoto wote wenye mtindo wa ubongo watakuwa wameridhi kutoka kwa mama zao?

Tukienda mbali zaidi kama baba ni HIV positive na mama ni HIV negative wakijahimiana na mama kupata ujauzito, mtoto atakayezaliwa atakuwa na uhakika wa 100% wa kutokuwa HIV positive?
 
Baba akiwa HIV +Ve,Mama HIV -ve mtoto hawezi kuzaliwa na VVU labda kama mama alipima akiwa yupo kwenye window period na mtoto akapata michubuko ya kugusana na damu ya mama.
Otherwise yupo salama.

Na hata mama akiwa HIV +Ve bado kuna uwezekano mkubwa tu mtoto akazaliwa bila maambukizi
hili linategemea kama mama anaattend clinic mara kwa mara kwa ushauri na pia anameza dawa za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwend akwa mtoto
 
Fertility ni uwezo wa kumpa mwanamke mimba...si quality ya mtoto...(mwenye utindio wa akili or not)

au unataka kusema mbegu weak (za mzee) zikitungisha mimba mtoto anakuwa hana akili...

Exactly!, fertility ni uwezo wa kumpa mimba mwanamke, ukisoma vizuri post wanaeleza kuhusu huo uwezo wa mwanaume at a certain age, unavyoanza kupungua kumpa mimba mwanamke, mwanaume wa hiyo age anachukua muda mrefu kumpa mimba mwanamke kuliko someone younger than them, I think wamesema it can take years for them to get someone pregnant na mtoto atazaliwa but most likely anaweza awe na down syndrome
 
Wanawake wanaochelewa kubeba ujauzito, wameonywa kuwa kuchelewa huko kunawaweka hatarini kuja kupata watoto wenye mtindio wa ubongo.

Mbali na hilo, pia wanaume wanaotafuta watoto wakiwa katika umri mkubwa wa zaidi ya miaka 60, nao wametajwa kuwa hatarini kupata watoto wa aina hiyo na wakiepuka hilo, watakosa uwezo mzuri wa akili darasani.

Taarifa ya daktari mkongwe nchini, Dk Ali Mzige aliyotoa wiki hii, amebainisha kuwa hali ya umri mkubwa wa wazazi wa kike na kiume, ndio chanzo kikubwa cha kuzaliwa kwa watoto wa aina hiyo, na siyo uchawi wala mazingaombwe.

“Naomba niweke wazi kwamba, mama mwenye umri zaidi ya miaka 35 kama ndio anaanza kuzaa kwa mara ya kwanza, Mungu aepushie mbali, lakini ana uwezekano mkubwa wa kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo.

“Mbali na hayo, pia kwa baba mwenye umri mkubwa miaka zaidi ya 60 na ushei, akitaka kutafuta mtoto uwezekano upo wa kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo.

Kwa hiyo ushauri wangu kwa wazee wenzangu tunaostaafu sasa, tulee wajukuu tusianze tena kutotoa vifaranga,” ameeleza Dk Mzige katika taarifa hiyo. Kwa mujibu wa Dk Mzige, kisayansi umri mzuri wa kuoa au kuolewa na kuzaa kupata watoto wenye afya nzuri, ni kati ya miaka 18 na 35 kwa pande zote mbili baba na mama.

Changamoto kijamii

Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo watoto hao, Dk Mzige alisema ni pamoja na unyanyapaa kutoka katika jamii kwa watoto hao pamoja na wazazi wa waliowazaa. Amesema kutokujua chimbuko la mtindio wa ubongo katika jamii, kumekuwa kukihusishwa na imani za kishirikina, kwamba mzazi amefanya kila awezalo, ili mwanawe awe na mtindio wa ubongo, ili apate mali na kutajirika.

Mbali na wazazi kuonekana kusababisha mtoto wao kuwa na hali hiyo kishirikina, Dk Mzige alisema watoto hao pia wamekuwa wakitengwa na jamii na wakikua hasa wanawake, hudhalilishwa kijinsia ikiwemo kubakwa.

“Wengi hunajisiwa na kubakwa na watu wenye akili timamu, kwa imani kuwa kufanya tendo hilo na mtu mwenye ulemavu, utapata utajiri na mafanikio mazuri katika shughuli zako,” alisema.

Changamoto kiakili

Alisema wanaozaliwa wakiwa na mtindio wa ubongo, huchelewa kukua kiakili na kimaumbile, ni wapole sana hawana fujo kama watoto wengine wanaozaliwa kikamilifu. Pia huchelewa kutambaa, kunyanyuka, kuzungumza na wanakuwa na misuli ambayo ni dhaifu haina nguvu ya kusukuma na kupiga mateke kama watoto wengine.

“Uelewa wao kiakili uko katika asilimia 50 (IQ), ukilinganishwa na watoto wa kawaida ambao wana uelewa na ufahamu wa asilima 100,” alisema Dk Mzige.

Dk Mzige pia alifafanua kuwa kama baba atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 60, kama mtoto hatazaliwa na mtindio wa ubongo, mtoto huyo kiakili atakuwa na kasoro endapo umri wa baba utakuwa umesogea na yeye bado anaendelea kupata watoto.

Aidha wanaozaliwa na tatizo hilo, magonjwa makuu yanayosababisha vifo kwao ni saratani ya damu (leukemia) na magonjwa ya moyo na wengi hawafikishi umri wa kuishi wa miaka 40.

Chanzo: http://www.habarileo.co.tz/index.ph...wanawake-wanaochelewa-kubeba-ujauzito-waonywa

Uuuuuwiiiii!!!
 
Back
Top Bottom