Wanawake wanaitwa laini laini kimakosa…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443

Huweza kuanguka mahali hata usipotarajia......

Kama hujawahi kusikia au kama hujui, naomba nikwambie kwamba, wanawake wanaumia zaidi au ni rahisi kwao kuumia wakiwa kwenye mzunguko wa siku zao (Hedhi). Naomba ujaribu kumfanyia utafiti mtu wako wa karibu ambaye unaweza kujua kwamba, hivi sasa yuko kwenye mzunguko wa siku zake, au kama ni wewe mwenyewe mwanamke, hebu jichunguze.

Kama ni kuumia mara nyingi hutokea ukiwa kwenye mzunguko wa siku zako. Je ni kwa nini?

Ni kwa sababu, wakati wa mzunguko huo wa siku kuna mabadiliko kadhaa ya kihomoni mwilini mwa mwanamke. Mabadiliko haya huwa ni ya kupwa na kujaa, yaani hayakai kwa muda mrefu, hubadilika kila baada ya muda mfupi.

Kwa mabadiliko haya, musuli wa nyama nyingine za mwili huathiriwa kwa njia moja ama nyingine. Katikati ya mzunguko wa siku, musuli na nyama za mwili huwa rahisi kuathirika. Katika kipindi hiki, homoni ya kike ya oestrogen, ambayo moja ya kazi yake ni kutoa nguvu kwa musuli wa mwili, hushuka sana. Kushuka kwa kiwango cha homoni hii, hufanya mwili kuwa dhaifu. Ni udhaifu wa ghafla wa mwili.

Mwishoni mwa mzunguko wa siku, homoni nyingine ya relaxin huongezeka. Kuongezeka huku ni kuruhusu nyonga kujifungua, ili hedhi itokee. Lakini kuongezeka kwa homoni hii hufanya nyama za mwili kuwa tepetepe, kinyume na zinavyotakiwa kuwa imara. Kwa hiyo muda mfupi kabla mwanamke hajaziona siku zake ama pale anapoanza kuzioana, yupo kwenye hatari ya kuumia kirahisi. Wakati huu kuteleza au hata kujikata ni rahisi zaidi.

Dk. Stephen Sandler anasema kuna uhusiano wa karibu kati ya kiwango cha homoni kwenye mwili wa mwanamke wakati wa mzunguko wa siku zake na uimara wa mwili wake. Anasema uhusiano huo uko wazi na hauna mjadala. Kwa sehemu kubwa, wanawake wakiwa kwenye mzunguko huu, maeneo ya viungo kama magotini, viungo vya vidole na miguu huwa na udhaifu.

Kwa hiyo kitendo cha kuvuka mahali pafupi tu, kinaweza kumsababishia mwanamke maumivu. Kuinama na kuokota kitu kunaweza pia kumsababishia maumivu. Wataalamu wamekuwa wakijiuliza kwa muda mrefu ni kwa nini wale wanawake wanamichezo, huwa wanaumia kirahisi wakati fulani, kuliko wakati mwingine. Hivi sasa wamepata jibu, kwamba ni kutokana na mzunguko wa siku…..

Naomba Mods wasipeleke huu uzi Jukwaa la JF Doctor maana unahusika sana hapa MMU...

Copy to: Kaunga, Madame B, lara 1, Lisa, nivea, MadameX, BADILI TABIA, AshaDii, marejesho, Zinduna, Preta, Zion Daughter, Remmy, mwaJ, Asnam, Kipipi, snowhite, cacico, Paloma, Mamndenyi, vivian, King'asti, amu
 
Last edited by a moderator:
Yawezekana ni kweli. mimi dalili kubwa ya kwanza ni miguu kukosa nguvu,ila na stress zinakuja kwa urahisi,huwa nakuwa mkali.
 
Hii sredi inanisaidia sana kwenye utafiti wangu. BADILI TABIA na cacico hebu kujeni pande hii....

Asprin hubby nimekuja.....

Kuumia sijui ila najua nakuwa careless flani hivi ndo kipindi nikishika hata glss navunja (ndo maana kila mara nakuomba hela ya kununua glass)

zamani nilikuwa na kisirani siku hizi kimeisha.....ila kipindi hicho nikisikia aina fulani ya mziki nakasirika hadi nazima redio (sijui ndo kudata huku) yaani huwa sitaki makelel kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ole wako garini unifungulie bolingo zako utajuta
 
Last edited by a moderator:
Sasa ndio najua ni kwanini mke wangu huwa ni careless sometimes than other times na pia huwa too emotional.
Thanks Mtambuzi 4 this educdtive thread.
 

hapo kwenye red,, dawa yko ni ku2mia vikombe vya plastic tu,,
 
kuna kichaa pia kinachokuja na hedhi-menstrual psychosis............tulikuwa zamani tunaita kichaa cha mwezi au wenye nacho wakiugua tunasema mwezi umeandama lol
 
aisee hizi days ni vizuri kuwa mbali na mimi
hasira, jamani ,ila nina tatizo lingine sugu siwezi kulisema hapa

acha kabisa.......mie ndo nakuwa mbogo alojeruhiwa!!! mkaliiiii......kama pilipili zote uzichanganye pamoja!!!
 
kuna kichaa pia kinachokuja na hedhi-menstrual psychosis............tulikuwa zamani tunaita kichaa cha mwezi au wenye nacho wakiugua tunasema mwezi umeandama lol
Mh, mkuu si kwamba umechanganya mada kweli.....!!!!
Hii ya kichaa cha mwezi si kile wanaita mwezi mchanga? hicho nadhani kinatofautiana na hiki kichaa cha hedhi.... Ngoja nifanye utafiti nitakuja na majibu baadaye
 
acha kabisa.......mie ndo nakuwa mbogo alojeruhiwa!!! mkaliiiii......kama pilipili zote uzichanganye pamoja!!!
Kumbeeee, nilikuwa nahisi hivyo siku nyingi kila nisoamapo post zako humu ukichangia baadhi ya mada.....LOL
 
aisee hizi days ni vizuri kuwa mbali na mimi
hasira, jamani ,ila nina tatizo lingine sugu siwezi kulisema hapa
Nishalijua na wiki ijayo nitakuja na uzi kuhusu tatizo lako hilo.....LOL
 
Mh, mkuu si kwamba umechanganya mada kweli.....!!!!
Hii ya kichaa cha mwezi si kile wanaita mwezi mchanga? hicho nadhani kinatofautiana na hiki kichaa cha hedhi.... Ngoja nifanye utafiti nitakuja na majibu baadaye


nitakuwa labda nimechanganya kutokana na wenye kichaa cha mwezi wengi ni wanawake,ila pia kuna kichaa kinachokuja na hedhi mtu anakuwa kichaa kabisa..lol
 
acha kabisa.......mie ndo nakuwa mbogo alojeruhiwa!!! mkaliiiii......kama pilipili zote uzichanganye pamoja!!!
yaani nakuwa moodless hata unipe nini,kuna siku nilikuwa nasafiri kuna jamaa nilikaa nae sasa akawa ananipa story zake za fix na mimi nilikuwa nimetoka msibani sijalala siku nyingi plan yangu ilikuwa kulala kwenye gari maana kesho yake job ,sasa mimi nikilala ile usingizi unataka kunijia ananishtua eti anataka nimuongeleshe khaaa nilimmaindi nikahama na seat! ila naenjoy sana siku hizo sometimes kuna kitu huwa kinanijia najifeel mwanamke wa ukweeeeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…