Wanawake wana Uwezo wa kushangaza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wana Uwezo wa kushangaza!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Jul 16, 2012.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mtu mwenye nguvu kuliko watu wote katika historia ya dunia alikuwa Samson, kama ingekuwa leo basi Samson angeitwa John Cena n.k
  Kama ni masumbwi basi Samson angebeba mikanda yote ya World Boxing Association (WBA) au World Boxing Council (WBC) au World Boxing Federation (WBF) au World Boxing Organization (WBO).
  Hakuna cha akina Tyson wala Evander Holyfield au Wladimir Klitschko wote wangedundwa sekunde chache tu baada ya pambano kuanza.
  Samson alikuwa shujaa (hero) kwa taifa la Israel, aliweza kuua simba kwa mikono mitupu, maelfu ya watu mikono mitupu pia na hata mageti ya vyuma yalishindwa kumfungia kwani aliyavunja bila huruma.
  Samson alikuwa na ugonjwa na mabinti wa kifilisti (aliwapenda sana ingawa alionywa na kwake ikawa sikio lisiosikia...)
  Mara ya kwanza alioana binti ambaye Biblia haimtaji jina na wengi huhisi hii ilikuwa ni Sababu tosha kwa Samsoni kuanzisha vita na wafilisti, ndoa haikudumu ilivurugika siku ya harusi hata hivyo Samson akampata mrembo mwingine kutoka kwa wafilisti, Delila ambaye hata hivyo wafilisti walimrubuni atafute siri ya nguvu za Samson.
  Hata hivyo mke wa Samson yaani Delila alikuwa na nguvu kuliko Samson kama huamini subiri!
  Huyu mwanamke alimaliza historia ya Samson na Samson akatoboa siri ya nguvu zake baada ya kuwekwa kufuani kwa Delila na matokeo yake akatobolewa macho na jina la kumchezea kama mdoli na kumpa kazi ngumu.
  Habari hii inatuelimisha au kutukumbusha kwamba uwezo alionao mwanamke kwa mume wake ni mkubwa ajabu na anaweza kufanya lolote anataka akijua jinsi ya kuchezesha kalata zake hasa kwa kujua mume wake udhaifu wake upo wapi.
  Wanawake wote wanauwezo mkubwa sana juu ya wanaume tatizo kubwa wanawake wengi wameshindwa kutumia uwezo wao, ushawishi wao kuhakikisha mume anamuweka sawa au kufanya vile anapenda kwa sababu hawajajifahamu.
  Hapa ninazungumzia kufanya yale ambayo mwanaume anaamini mume wake anazembea kama vile kuiweka ndoa katika mstari sahihi.
  Ni kawaida kuwa na Generals, au Governors au Rais au mawaziri wanaume hata hivyo wengi wao hujikuta wake zao wakiwa chimbuko la uongozi wao na kwamba huwa wanawasaidia kutoa maamuzi ya mambo mengi.
  Kuna usemi kwamba:
  “A man’s wife has more power over him than the state”
  Hata binadamu wa kwanza pale katika Bustani ya Eden alianguka baada ya shetani kumtumia Eva (mwanamke) kwa kumdanganya kula matunda na hatimaye amshawishi mume wake naye ale kwani alijua angemtumia mume ingekuwa ngumu sana mume kumshawishi mke akubali badala yake aliona mwanamke ni rahisi kumshawishi mume na akakubali.
  Bottom line ni kwamba mwanamke anao uwezo mkubwa sana katika kuvumbua kile kilichomo ndani ya mume wake na kwamba mwanamke akitumia uwezo wake ambao Mungu amempa kuhusu mume basi anaweza kujenga mahusiano na ndoa imara na inayoridhisha.
  Wapo wanawake kila kukicha ni kulalamika tu kwamba mume wangu mume wangu, acha kulalamika tumia uwezo wako wa kuwa mwanamke kumsaidia mume kuwa mume bora katika ndoa kwani Mungu amekupa uwezo wa ajabu ndani yako kiasi kwamba mume yeyote anaweza kumkubali kile mke anasema pale mke akitumia uwezo wake sawa na Mungu alivyompa Adam bustani yake akaikana.Mungu wake likatukanwa.
  Delila alitumia uwezo wake kama mwanamke kumshawishi Samson atoboe siri ya nguvu zake ambayo ilikuwa ni nywele zake kutonyolewa tangu utoto wake.
  Baada ya kutoboa siri tu wafilisti wakamshika, wakamtesa na wakamtoboa macho.

  AMEN.......................
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  wafilist ni watu gani?

  Samson wa siku hizi sio wa siku za mwanzo, huyo samson alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mkewe ndio maana akatoa siri zake na kuamini kuwa ni mwenzake. Samson wa siku hizi siri zake anaweka na kimada au kifuani kwake sasa hapo unategemea mwanamke anakuwa na uwezo gani wa kumdhibiti mumewe ikiwa anaishi nae na huku hajui his inout.
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kumbuka delila alihangaika sana mpaka kuja kujua siri ya mumewe
  Wanawake siku hizi hawajui kubembeleza mmewe mpaka ampe yaliyo sirini
  Wanaume na wanawake wa siku hizi wakifuata nyayo za wa kale hawatakuwa tofauti na wa zamani,......
   
 4. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mungu alimpa mwanaume matamano juu ya mwanamke na kutufanya tuwe dhaifu kwao. dada mrembo akikushikashika kidogo tu wengine tunaadhirika mbele ya kadamnasi. kuna watu wanawatoa wapenzi zao shopping za nguvu na kula lunch kempinski wakati wao wanashindia chipsi dume lol
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Cha ajabu bible hiyo hiyo anasema aliye dhaifu ni mwanamke.......
   
 6. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  lol, udhaifu wa mwanamke ni kwamba hawezi kufanya chochote bila mwanaume. udhaifu wa mwanaume ni kwamba hawezi kujizuia mbele ya mwanamke
   
 7. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kaka kazi ya uchungaji umeanza lini..??Back to the topic,usifanye mchezo na kiumbe jike bana ukionyesha udhaifu anaweza hata kukuambia umhonge roho yako,lakini huwa anafanya hayo akishajua udhaifu wako kwa sisi wenye mioyo kama chuma cha pua hata huwa hawajaribu,nilishatishiwa na binti eti nitajiua hapahapa nyumbani kwako usiponitekelezea ombi langu,nikamwambia tena utakuwa umenipunguzia matatizo kweli ebu ngoja nikuletee sumu ya panya, akaniuliza hivi wewe ni mzima kweli..??
   
 8. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Subutu umwambia Tonga eti sasa nna m100 uone moto wake! Mmba ya mawee! Kabati ya mbeo! Sinema ya mmba! Ngumbe ya malela! Kutiri stauti? We! utatangulia mela za haki kabla ya siku! Ndo maana wazee wa kichagga hawakubali kuwaambia wake zao ukweli wa mali walizonazo!
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Chorus x2
  Kama ni demu sikiliza(nisikize me),kama una swali uliza(niulize me)

  Verse I
  Mwanamme kwa demu ni sawa na mfupa kwa fisi,mademu wana nguvu zaidi ya sisi sema wengi hawajiamin au msemo ule wa mwanamke kipofu nao ndio wanauamini,msichimbe madini(sawa) ila sio lazima muwe wafanyakazi wa ndani,big up to my gyal,au hawaoni stara,beyonce au hawataki kuendesha murrano kama lady jaydee?

  Kwa hisani ya mnyama aka mimi aka 120 nge aka Ngwair
   
 10. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kwakweli mimi simjui delila bado hujanijibu wafilist ni nani?
   
 11. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Hili halina pingamizi, wanawake wana nguvu sana na ushawishi mkubwa kuliko wanaume.
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hahahaha umenichekesha, sijawa mchungaji bhana....
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wafilisti ni Taifa lililokuwa linapigana na waisrael.......embu soma hapa chini kidogo:


  WAFILISTI
  Kwa miaka arobaini Waisraeli walitaabishwa na Wafilisti, walioishi katika ukanda wa
  nchi iliyo pwani ya Kusini mwa Kanaani. Walikuwa ni watu wenye nguvu, waliopenda
  vita ambao hawakushindwa wakati Waisraeli walipoingia na kuimilki Kanaani chini ya
  uongozi wa Yoshua. Miji yao mikubwa ilikuwa Gaza, Gathi, Ashkeloni, Ashidodi na
  Ekroni. Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na mtawala wake na hawa waliitwa Mabwana
  watano wa Wafilisti, wakati walipokuwa chini ya ukandamizaji wa Wafilisti, Waisraeli
  hawakuweza kuunda mapanga au mikuki (1 Samweli 13:19-20).Hivyo bila ya
  msaada wa Mungu hawakuwa sawa na madui zao waliowajia wakiwa na silaha hizi.
   
 14. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145


  Wafilisti ni hawa jamaa wanaojulikana leo kama wapalestina,ila ukianza mambo ya kuulizana source ndio hutaniona tena kwenye mada hii..
   
 15. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hapo penye nyeusi ni vzr wadada kupazingatia, niliwahi kusoma andiko moja mahali fulani; sijui kitabu gani vile ..... maana sisi wapagani tuna shida sana .... ila iliandikwa kuwa "mwanamke mwenye hekima ataijenga nyumba yake, bali yule mpumbavu huivunja nyumba yake mwenyewe". Naona kama andiko hili linaendana na mawazo yako!
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,744
  Likes Received: 12,820
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa!
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tulishajifunza kwa makosa ya Samson, ndo maana hatutoi siri kabsaa! Ila wanawake mnanguvu sana hamjui tu.
   
 18. Rapunzel

  Rapunzel JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,089
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  chezeaaa mwanamke weye? utalowaaa
   
 19. MARILYN

  MARILYN Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wafilisti ndo wapelestina wa sasa
   
 20. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Jukwaa la dini lina kazi gani?
   
Loading...