Wanawake waliozoea kuachwa na wapenzi

Wanawake waliozoea kuachwa na wapenzi

ZING SOKONI

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,512
Reaction score
57,115
Wanawake wa namna hii unaweza kuwa na nia ya dhati kabisa ya kuwanasua katika matatizo ya kimahusiano ambayo yanawasumbua lakini kule kutokujiamini kwao mwisho wa siku kunasababisha kuvuruga kabisa mahusiano. Hii inatokana na kwamba wameteseka kwa muda mrefu hali ambayo inapelekea kutokumwamini mwanaume ambaye anaweza kuwa anampenda kwa dhati kabisa.

Wanawake wa dizaini hii ni ngumu kwao kukuamini pale unapokuwa unawaelezea malengo ambayo unayo juu yao hivyo kupelekea mifarakano au matatizo kwenye mahusiano na mwisho mwanaume huishia kubwaga manyanga na kutafuta ustaarabu mwingine.

Sijajua kwa upande wa wanaume kama hiki kitu kipo, ila nafikiri ni muhimu kujua historia ya mapenzi ya mwenzi wako kwasababu wapenzi walioumizwa kwa muda mrefu ni vigumu sana kudumu nao katika mahusiano kwa muda mrefu.
d768d0cb65951f4ad04ac9fc2c7fffb3.jpg
 
Ukikanyaga nyoka lazima ukiona mjusi ushtuke
Kwa Hiyo wanajihisi mnoo....

Ila nawahurumia wadada flani hivi wanakuwaga na mapenzi ya dhat hujitoa kwa hali na na Mali kuhudumia penzi lakini mwisho Wa Siku huachwa solemba......!
Sad::::
Unajua kuna wanawake ambao ni wife material na wengine "sex" material kwahiyo muda mwingine mwanaume humpenda msicha kama sex material hivyo akianza kuchuja anapiga chini
 
Ni kweli kabisa...mimi hapa juzi tu nimeachana na demu kisa mambo ya kunihisia vibaya sababu eti aliyepita kabla yangu kamtenda....inakuwa kero maana nikikosea kidogo tu utasikia ''Ndo kawaida yenu hiyo''..nikaona cha kufia nini..nduki
 
Naona idadi ya wanaume inapungua na wavulana kuongezeka, muda wote ni kulalama tu hii siyo tabia ya mwanaume, mwanaume akiudhiwa anaguna tu halafu anaondoka akirudi yameisha anapata kimoja cha faster cha raha basi vikojoleo vikuungana tena hapo kuna ugomvi utoke wapi? Huu ndo uanaume siyo haya mnayoyafanya nyie
 
Bro nadhani unaongea kuhusu mtu usiyemjua....sababu zingine hazisemeki mkuu......mimi ni mvumilivu sana ila kwa hapa nimeshindwa..kidogo tu utasikia ''KAMA VIPI NAWEWE NIACHE KWANZA ROHO YA MAPENZI SINA BASI TU.''
 
Watu Walioumizwa Sana Kwenye Mapenzi Ni Wachache Sana Wanaofanikiwa Kupata Watu Wa Kudumu Nao. Hii Hutokana Na Ukweli Kwamba, Wengi Wao Huwa Na Fikra Hasi Linapokuja Swala Zima La Mapenzi. Matokeo Yake, Fikra Hasi Hizi Huendelea Kuvuta Watu Ambao Sio Sahihi Kwao Na Hivyo Kuendeleza Utamaduni Waliouzoea Wa Kuumizwa.
Swala La Msingi Kwa Watu Wa Namna Hii Ni Kubadili Namna Yao Ya Kufikiri Na Kuishi Sasa Badala Ya Wakati Uliopita.
 
Ni kweli kabisa...mimi hapa juzi tu nimeachana na demu kisa mambo ya kunihisia vibaya sababu eti aliyepita kabla yangu kamtenda....inakuwa kero maana nikikosea kidogo tu utasikia ''Ndo kawaida yenu hiyo''..nikaona cha kufia nini..nduki
au ni mimi nini maana mimi ndo zangu sio kwamba sitongozwi ila siwezi kabisa akikosea tu kidogo nasepa yaani mimi kunitongoza na kukukubali leo na kuachana na wewe asubuhi ni kawaida siamini mtu
 
Kitakacho fanya udumu na mwanamke yeyote yule, iwe aliyeumizwa au asiye umizwa kimapenzi adumu kwenye mahusiano ni wallet!

So long as wallet inadumu basi naye ni lazima adumu.
Wallet Inakupa Uhakika Wa Kungonoika Tu, Mapenzi Ni Zaidi Ya Ngono Bro'. Pesa Haikupi Mapenzi Ya Kweli, Isipokuwa Inaboresha Penzi Tu.
 
au ni mimi nini maana mimi ndo zangu sio kwamba sitongozwi ila siwezi kabisa akikosea tu kidogo nasepa yaani mimi kunitongoza na kukukubali leo na kuachana na wewe asubuhi ni kawaida siamini mtu
Usisahau Hata Wewe Ni Mtu Pia.
 
Back
Top Bottom