Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,951
Nawasalimia wana JF
Niko na rafiki yangu wa karibu sana amenisimulia historia yake ya uhusiano na wanawake (sasa hivi ameoa na anawatoto wawili mapacha).
Alinieleza wanawake wote walio muacha kwa vituko wote hawajaolewa. Kanitajia kweli wote wapo wapo tu na umri wao sasa unaenda, na ukiwatazama wanahitaji sana japo wapate wenzi wao.
Sikuelewa sababu gani au imetokea tu. Jamaa kusema kweli huwa anajari, lakini katika maisha yake wanawake zaidi ya watatu walimwacha kwa visingizio eti kwamba hana mkwanja wakutosha.
Japo kuwa rafiki yangu wakati ule alikuwa na kazi ndogo iliyokuwa inamwingizia kipato.
Nimejaribu kuongea naye kuwa hiyo huenda ni jambo la kiroho zaidi, inabidi aende akaongee nao na awasamehe na kuwaachilia.
Yeye kasema alishawasamehe. Lakini nikamsisitiza awatafute aongee nao ili waeze kufunguliwa. Maana kinachoonekana kile walichokuwa wanakihitaji mpaka leo hii hawajakipata. Na wanahaha sasa na sura zao zinaanza kupoteza mvuto.
Mwana JF hebu toa nawewe ushauri hivi hii ni kweli inaweza kutokea?
Nawasilisha hoja.