Wanawake waajabu sana

floow

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Posts
411
Reaction score
858
Nina mpenzi wangu huwa anajifanya ana ana akili sana, yeye anafahamu kushona nguo, hivi juzi ameomba nimnunilie cherehani ya kushonea pia nimpatie pesa kwa ajili ya kufungua ofisi yake, hayo yote nimeahidi kumfanyia mwisho wa mwezi huu.

Kinacho nishangaza juzi nilipokutana nae, akaomba tupige picha za pamoja kupitia simu yangu kisha nimtumie (yeye simu yake haina camera nzuri) kweli tulipiga picha na nikamtumia.

Cha ajabu ninachokiona zile picha anapost mtandaoni ila amekata vipande ambavyo mimi nipo. Pia kaviweka ukungu vipande ambavyo mimi nimetokea sana ili tuu nisionekane.

Jamani hapo mnamtafsiri vipi huyu mwanamke mimi nimeshaanza kumuona mchawi tuu.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
 

Attachments

  • FB_IMG_1500012887693.jpg
    40.4 KB · Views: 32
hahaha power of women kuna kitu umemnyima ndo maana. ivi hamuelewagi lugha zao wew unadhani yeye hapendi simu yenye camera nzuri kama yako? muwe mnajiongeza
 

Dah, mapenzi yanalemaza uwezo wa kufikiri kwa kweli

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Duh paka utimize ahadi ndio utawekwa mtandaoni.

Is that a bid deal??? Kuwekwa mtandaoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…