Wanawake wa Tarime: Inatia huruma... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wa Tarime: Inatia huruma...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tuko, May 31, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nilihudhuria harusi moja, wakati naingia nikakuta upande wa familia ya mwanaharusi mmoja wanacheza ngoma ya kikwao.. Japo walionekana kujitutumua na kuonyesha furaha, niliweza kusoma sense ya kutojiamini, uoga na huzuni miongoni mwa wanawake hali iliyojijumlisha ikaleta mwonekano wa kukata tamaa ya maisha.

  Nikauliza ngoma ya wapi hii, nikaambiwa ya Kikurya, nikadhani labda maudhui yake yalikuwa ya huzuni. Ghafla ikaunganishwa na wimbo utamu wa yesu, still nikaona sura za huzuni zinatawala wanawake wale...

  Baada ya mjadala mfupi na wenzangu, tukagundua kuwa majority yao walitokea kijijini huko Tarime, na wanawake kupigwa na kunyanyaswa imewafanya waonekane watu wa huzuni na unfriendly...

  Hivi wanaume wa Musoma na wengine wote mnaopiga wake zenu, can't you just BOLD your arguments na mkapata kuheshimiwa bila kuwapiga wanawake??!!!

  Hili jambo unaweza kulichukulia simple kama hauexperience, but kwa wale wanaoona ndugu zao, marafiki zao, mashemeji zao wanavyonyanyaswa au hata wao wenyewe wataungana nami kutetea sana haki za wanawake hawa...
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  nenda png utabadili mtazamo, survival of the fittest
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  naogopa hadi kukoment.....hawachelewi 'kukugecha'....

  But seriously, inasikitisha
   
 4. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Hata wewe umenisktisha! Una siku mbili , umepiga kambi huku! Looh BT Hata Hi ?
  Vibaya ivoo !
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu, ni utamaduni wa watu. Huko wanawake wenyewe wasipopigwa wanakuona wewe mume mtu wa ajabu. Unaweza achika kwa sababu ya upole/wema wako. Huko kinachotawala ni sadism - masochism.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani huko tarime sheria zimeenda likizo? Ama serikali haijafika huko bado!
   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nasoma paper moja ya jamaa anaitwa Fleisher ni Anthropologist, anasema Kuria wana culture ya violence si kwa wake zao na watoto tu bali hata wao kwa wao alikuwa anaongelea cattle raiding na interclan war. Akawa ame mquote mkuu wa wilaya wa Tarime anasema Tarime ni the most difficult district to administer in Tanzania. Hao watu hawajuhi wala hawatambuhi sheria. Serikali yenyewe inawaogopa.


  Kuna baba alikuwa jirani yetu tulikuwa tunamhita mwanasheria mimi nikiwa bado mtoto, sikuwa naelewa kwa nini anaitwa mwanasheria. Ila miaka ya nyuma kidogo aliteuliwa kuwa jaji na mimi nilikuwa nimeshakuwa mkubwa ndo nikajua kumbe alikuwa lawyer. Lakini huyu baba nakwambia hana hata sifa ya kuwa jaji. Alimkata jirani yetu mwingine panga akatoa mkono kisa alisikia anatembea na mke wake mdogo; wote ni watu Wakurya, sijuhi kilichoendelea baada ya hapo. Ila naona alokatwa mkono hakushtaki kwani jamaa kibarua kingeota nyasi na asingekuwa Jaji leo hii. Hawa watu ni tit for tat hakuna kwenda kushtaki; ushtaki wewe mwanamke??? Pona ya jamaa nadhani ni kwa kuwa alikata mkono wa mkurya mwenzie ambaye wala hakwenda kushtaki.

  Si unajua mambo ya panga jamaa kakinga mkono lisipige kichwa. Tena ni Dar wala tukio hilo alikutokea Tarime ila wote wakurya.

   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hahahahahaaaa huku nimeingia bahati mbaya tu........

  Ila serious kama wanapigwa its sad maana mwili unauma asikwambie mtu, ingawa sidhani kama wakurya wote wanapiga....maana nina ndugu yangu kaolewa na mkurya sijawahi ona wakigechana.... (unless kama wanazidunda kimya kimya)
   
 9. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Kuna best friend wa dada yangu aliolewa na professor mmoja mkurya. Alikuwa ni dada ambaye ukiona life anayoishi unasema na mimi nikue niolewe. Jamaa alikuwa anampa kila kitu kuanzia yeye na familia nzima anatunza (mashemeji wote kapeleka ng'ambo kusoma) maana jamaa alikuwa na chenji si za kitoto alikuwa na projects kubwa kubwa. Dada kila mwaka shopping majuu.

  Walikaa kwenye ndoa miaka 11 (kama niko sahihi) bila hata huyo mwanaume kuinua mkono. Nikasema kumbe waliosoma wako tofauti. We! Siku aliyomkung'uta yule dada alilazwa ICU 5 days hajitambuhi. Alichanika uso wote na alikuwa mzuri kishezi. Na ndoa ikaishia hapo. Yaani mdada alitoka hospitali na kuchanja mbuga kwao. Toka hapo ninasema hakuna cha msomi wala wa mjini.
  Maana yule baba nilikuwa namwona mstaharabu sana.

  Ila ni watu wazuri sana kama marafiki si mume kwa kuwa wako open na si wanafiki.


   
 10. M

  Mundu JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu Tuko nadhani umeingia mlango wa kutokea... wenzako wanakwambia wasipotandikwa na waume zao wanalalamika kwa wakubwa kuwa kuna walakin...mapenzi yamepungua. Iweje wewe unasema ile mila ni mbaya?

  Au wewe ndo umeandika lile tangazo "pata ridhaa yake, bila mabavu"?
   
Loading...