Wanawake wa Somalia mashakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wa Somalia mashakani

Discussion in 'International Forum' started by Saint Ivuga, Jan 25, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  Wanawake wa Somalia mashakani

  [​IMG] Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Msemaji wa Al Shabbaab, Sheik Ali Mohamud Rage

  Wanawake wa Kisomali wanaoishi katika maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo Al-Shabbaab, wanajikuta katika wakati mgumu kwa sababu ya kuongezeka kwa sheria kali zinazowekwa na wanamgambo hao na kulazimishwa wazifuate.

  Hivi karibuni, Al-Shabbaab walitoa agizo kwa wanawake wanaoshi katika mji wa Kismayu kutofanya biashara za kubadilishana na wanaume wanaofanya kazi kwenye meli zinazotia nanga katika bandari ya pwani ya mji huo.
  Wamewakataza pia kushikana mikono na wanaume mbele za watu, wamewaka kusafiri peke yao, na hawawaruhusu kufanya biashara yoyote wala kufanya kazi ofisini.
  Kiongozi wa juu wa Al-Shabbaab amesema kuwa mwanamke hatakiwi kuonekana yupo na mwanaume kutoka nchi nyingine katika eneo la bandari, na yeyote atakayekwenda kinyume na agizo hili, atakamatwa.
  Al-Shabbaab wapiga marufuku muziki, sinema
  [​IMG]Bildunterschrift: Wanajeshi wa Kisomali wakiwa mafunzoni nchini UgandaNeno Al-Shabbaab lina maana ya kijana katika lugha ya Kiarabu, lakini kundi hili limepiga marufuku mambo yote yanayopendelewa na vijana. Kwa mfano, limepiga marufuku kuangalia sinema, miziki inayosikika katika milio ya simu, kucheza ngoma kwenye sherehe za harusi na kuangilia mpira kwenye televesheni.
  Wanawake wengi katika mji wa Kismayu ni wajane, kwa ama kuachika au kufiliwa na waume zao. Wameishi kwa miaka kadhaa kwa kutegemea biashara ya kubadilisha mboga za majani na matunda, na kupewa mafuta na bidhaa zingine kutoka kwa wafanyakazi melini.
  Akiongea kwa simu na Shirika la Habari la Reuters, Hawa Olow, alisema kuwa, yeye ana watoto watatu na amewakuza kwa hicho kidogo anachokipata kupitia biashara ya kubadilishana bidhaa bandarini, lakini kwa sasa hawezi tena kufanya biashara hiyo.
  Al-Shabbaab wameamuru wanawake lazima wanunue na wavae vazi maalum refu na pana, ambao kundi hilo linatengeneza.
  Vile vile, wanamgambo hawa wamepiga pia marufuku biashara ya mirungi inayotafunwa sana na wanaume na kulewesha kiasi. Mirungi maarufu sana katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika. Wanawake wengi katika mji wa Kismayu hujishughulisha pia na biashara hii kwa magendo, lakini wakikamatwa wanafungwa jela siku 20 na kulipa faini ya shilingi milioni moja za Kisomali.
  Mwanamke mwengine, ambaye hufanya biasahra hiyo, ameimbia Reuters kuwa, wakati wa vita walikuwa na maisha mazuri na amani kidogo, lakini sasa hali ya maisha ni ngumu kwa kuwa utawala wa Al-Shabbaab unatoa adhabu kali hata kwa vitu vidogo vidogo.
  Mwanamke huyo amesema Al-Shabbaab wamewaambia wanawake hawatakiwi kufanya shughuli yoyote ile.
  "Kwa kuwa wengi wa wanawake hawana waume, wameachika au waume zao wamekufa kutokana na mapigano, maisha kwa ujumla yamevurugika." Anasema mwanamke huyo.
  Mwanamke haruhusiwi kukaa karibu na mwanamme katika basi na akisafiri lazima asindikizwe na mwanaume mwenye undugu naye.
  Profesa wa Historia katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, Abdiwahab Abdi-Samad, anasema katika familia yake wamezaliwa na kukua wakiwa Waislamu na haoni mahala palipoandikwa katika Uislamu mwanamke asifanye kazi. Anasema wanachofanya Al- Shabbaab ni kuchukua nadharia hizo kutoka kwa kundi la Taliban la nchini Afghanistan na wanamgambo wengine wenye itikadi kali.
  "Ikiwa Al-Shabbaab hawataki wanawake wafanye kazi, basi lazima wawape pesa ili familia zinazowategemea ziweze kuishi." Anasema Profesa Abdi-Samad.
  Katika mji wa Afgoye, uliopo kusini mwa mji mkuu wa Mogadishu, ambako Bibi Fatuma Ahmed anaishi, amesema yeye mwenyewe alichapwa bakora mbele za watu na kijana mdogo anayelingana na mjukuu wake kwa kutovaa vazi lililoamriwa na Al-Shabbaab.
  Bibi Fatuma ameambiwa asivae nguo zake za zamani, lakini anasema yeye ni mzee wa zaidi ya miaka 60, hivyo hakuna hata mwanamme anayemtupia macho.
  "Kwa nini wananilazimisha nivae nguo hizi nzito?" Anauliza kwa uchungu Bi Fatma.
  Mwandishi: Fatuma Matulanga/Reuters
  Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hivi hawa watu hawana kazi nyingine???
  Shariaaa shariaa....waitumie kumaliza mapigano badala ya kukandamiza wanawake!
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mimi nafikiri hii Somalia ingeunganishwa na Sudan ikawa nchi moja
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nafikiri Lizzy hawa jaama hawana kazi nyingine zaidi ya hiyo this is utterly ridiculous kabisa
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kumbe kwenye uislamu mwanamke haruhusiwi kufanya kazi
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ili iweje Mkuu!
   
 7. e

  elburliz Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanawake wa kiislam...je hii ni sawa?? oppression and violation of women?? be their mouth piece and save the world!!!
   
 8. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Pia AL SHABBAAB wampiga marufuku kwa wanawke kuvaa Bra na pia kama mwanamke alikuwa amekaa kwenye kiti ndani ya Bus akiondoka lazima mwanaume usubiri dakika kumi kabla ya kukalia kitin hicho ili joto la mwanamke liwe limetoweka kinyume cha hapo ni viboko
   
 9. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Samahani Source ni REUTERS
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hivi wapi imeandikwa kwenye Uislam kuwa mwanamke hatakiwi kufanya kazi?
   
 11. n

  ngoko JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lizzy, hawa watu wanajaribu kurejesha maadili yaliyopotea katika jamii hiyo ili pale yatakapokuwa aligned na matakwa ya sharia basi kila mmoja atajikita kujenga taifa kwa kufuata hayo maadili .Kumbuka mmomonyoko wa maadili pia unalitumbukiza tz kwenye huo mwelekeo , maana kila maovu yanayotokea ni wazi ni kutokana na kukosa maadili ..., rejea maneno ya Mzee Kaduma kwenye Kongamano la I la Katiba UDSM .
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  ndiyo shariah hiyo, kwa haraka haraka ni kama zaidi ya 50% ya shariah law ni za kumkandamiza mwanamke. KADHIA court.
   
 13. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Ebo!
   
 14. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  That's sharia kudadadeki!!!!:shock:
   
 15. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Eee Mungu kisikie kilio cha akina mama hawa!

  Wakomboe katika shida hii Baba!

  Amen!
   
 16. d

  damn JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hivi wanawake wanaojifunika gubigubi, baibui huwa wanavaa bara?
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  hawavai..wanafuata sharia vilivyo
   
 18. BOLT

  BOLT Member

  #18
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi wanaiuwa kila siku
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani wanashangaza kweli!Badala ya kuwatumia wanawake kufanya kazi nyepesi waendelee wanakaa kuwapangia nini wavae ndani ya nguo zao!
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kitendo cha kumchapa mtu mzima viboko tu sio maadili na sidhani kama italeta maadili zaidi ya kusambaza woga!
   
Loading...