JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,967
Wiki iliyopita nikiangalia kipindi cha Television na mama yangu, Mtangazaji akawa anasimilia kisa cha dada mmoja kumwacha mume wake na kurudi kwao kwa kisa cha kukuta meseji ya mapenzi kwenye Simu ya mumewe.
Haya ndio maneno alosema mama, kwanza aliguna kwa masikitiko makubwa kisha akasema meseji tu! huku akishangaa, akaongeza enzi zetu tulikuwa tunaletewa ndani hata wanawake wanne na hatukuthubutu kurudi, wa siku hizi wana bahati kubwa.