Wanawake wa siku hizi hawataki kero, ukimkera tu umeachwa

Ushauri wa kipumbavu kabisa huu, hivi unaandika haya ukiwa kwako au kwa shemeji yako?
 
Habari zenu wakuu,

Nawakumbusha wanaume kwamba wasiishi kwa mazoea. Siku hizi hakuna Wanawake wanaopenda tabu au kutesa moyo. Ndo maana unaona ndoa nyingi hazidumu.

Mwanamke wa siku hizi akisikia kwamba una mchepuko anakuacha, yaani hajaona just tu kusikia..

Mwanamke wa siku hizi ukimletea mapombepombe yako wakati yeye hanywi na akikukataza ukakataa unaachwa, bora uoe mnywaji.

Mwanamke akiongea muache aongee hadi hasira ziishe, huwezi mshinda kwenye kuongea hata ukimeza spika. Mwanamke akiongea ukamjibu utaishia kugombana naye halafu kesho anakuacha anarudi kwako anasema ulimpiga hata kama umemfinya tu.

Usitake kushindana na mwanamke, ukiona umeanza kushindana na mwanamke, jijue ndoa yako imeanza kuteteleka kesho yake anakuacha unabaki unashindana na baridi usiku na akiondoka unabaki unashindana na kubadilisha wasichana.

Mkeo mheshimu na umnyenyekee vinginevyo utaachwa.

Watoto wadogo watabisha lakini huu ni ushauri nawapa kutokana na experience.

Usiguse simu ya mkeo, bila ruhusa yake ukiigusa utaipasua then mtagombana atakuacha.

Umeoa mwanamke mwenye mtoto au watoto ukataka kumfuatilia anapompeleka mtoto kwa baba yake jua utakufa kwa presha kukonda kwa wivu maana yake utaachwa. Siku ukiwafumania utaambiwa alikutangulia kuniona then unaachwa.

Kama unamhitaji mkeo au unampenda na unataka kufanya naye maisha usimfuatilie.. Muache Mungu amuongoze, wewe Mwanaume dumu magotini mwa Mungu akiomba akusaidie, hakika utashinda.

Walioshindwa na ndoa au walioachika wataanza kusema amekupa limbwata.. Usijali maneno yao sababu ukiachwa watajisifia sana.

Usipofuata huu ushauri jua kesho unaachwa.

Kama huogopi kuachwa jua hujawa tayari kuwa na familia. Usoe na endelea na ubazazi, kama umeoa acha kumtesa mtoto wa watu.

Kama unaogopa kuachwa basi oa na tembea katika misingi hii upate wa kukuzika na kukulilia siku ukifa.
Dah Umenisikitisha sana huwezi kuwa mwanaume pambafu¡!!!!
 
Mwanaume ukimuacha si umempa fursa baba au nakosea. mwafrica haaachwagi? wadanganye haohao!

Mahusiano anagharamia nani kwa maana kodi ya meza? mimi au yeye?

umetumika weee! kukugeuzageuza mpaka akajipatia mitoto dahari, mali, jumba zuri, af niache aje kukaa jackline marioere! adui yangu mkubwa weeee! umerogwa au! leo unatudanganya humu? mfyuuuu!

yaani nikaanze moja kutafuta au. tuseme huo ni uchoyo sababu umejifikiria wewe wewe tu, fikiria huyu unaye muacha pia kiutu zaidi. fikiria ndg zako na shemeji zako waliokupenda, rafiki zenu wakiwatembelea, wakala na kunywa meza inavopendezaga, machopochopo, vinywaji, maongezi vicheko, wachungaji, wanakwaya nk, watajisikiaje kuacha mji wako ambako walikuwa wanapata hayo yooote! wakipita zao. eti leo haupo? unaenda kudanga! au kutafuta stress!

siku huzi ukiondoka ndo imetoka baba, mme hawazi kuangukia, hata kwenu hapitiiii! atajidai amesahau njia!

Mbaya zaidi fikiria watoto, wazuri unao waacha kirahisi rahisi tu.
 
Sawa umerudi kwenu, kuishi kwenye ugali wa shikamoo tena? unapenda hii raha wewe! na utaahira wako..

Ukiwa doororo kichwani hakuna ilimu Dunia ndo nitoleee! umekuwa maskini kabisaa! Utaumizwa kisaikolojia na wanafamila weeeee! tena hata wao wamekosa offer za dezo kwa mkwe! si unajua wanaume wanavyojipendekezaga kwa wakwe!

usiombee ukosee kitu hapo kwenu ukikosea kidogo tu, utasikia vijilaana vya hapa na pale ''ndo maana umeachwa'' kwa sababu ya huu huu ujinga wako, yule kijana mpole vile jamani utampata nani sasa mwanangu? Dunia hii ya Mungu? haya twende shamba tukalime! utalimishwa weye mpaka uchakae, mme haji kuangukia. umeacha self container maridadi kabisa na chemchem za mjini ziko mpaka ndani. unaenda changanywa chumba kimoja na wadogo zako? shwaini mafuta.

Utajenga tabia km hivi kila ukisikia wageni ''Hodi Hodi humu ndani'' unakimbia km huna akili nzuri kufungua milango,ukidhania amekuja kupiga goti kumbee! ni majirani tu! wakati wakufanya kazi hiyo ya kufungua milango ni ya wadogo zako!

Labda kidoogo! uwe na kajikazi, utaishi salama japo miaka 10 hivi.
 
Tatzo hapo linakuja mentality, mie naona kwa uzi wapo wanafikiria upande mmoja wa mahusiano ndio unaotakiwa ufanye kila linalowezekana kudumisha uhusiano, wakat upande mmoja uwe huru kuumiza, kisa unajua kuacha. Haya,
Sema mie pamenifurahisha pale panaposema anakuacha unaanza kubadili waschana. Hahahah., ambao n wanawake hao hao. So Wanaume msijali wapo wakubadili hamtapigana na baridi, kuliko fedheha moyon.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom