Wanawake wa kabila la wazinza

Wanawake wa kabila la wazinza

Status
Not open for further replies.

tatanca

New Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
3
Reaction score
1
Hii! kwa wote,

Nimepata mchumba wa kabila la wazinza,
Nawaombeni kwa wale wanao lifahamu kabila hili la wazinza, je wanawake wa kizinza
mila zao zikoje? tabia zao kijami na pia kiunyumba zimeka vipi? wanapendelea nini?
pia naombeni ushauri wenu,
 
Ndıyo mara yangu ya kwanza kulısıkıa hılı kabıla. Lınatokea mkoa ganı?. Wanaolıjua watakueleza tabıa zao ıngawa nafıkırı ımeshaelezwa mara nyıngı na zaıdı watu wengı wamekuwa wakıkosoa tabıa ya kutaka kuelezwa sıfa za mtu kwa kuegemea kabıla.
 
Unaandika kama umekurupushwa usingizini? Manawake ndio nini?

Alafu siku hizi mambo ya ukabila bado tu mnayo?
 
Ukipenda, hata chongo utaita kengeza. Mapenzi hayaangalii kabila, mapenzi ni kipofu, kama umempenda kweli kabila lake si kitu, wewe ulichagua kuzaliwa kwenye kabila lako?
Vingenevyo hujapenda, unafanya maigizo tu.
 
kwa kuwa ni mpenzi wako......kwa nini usimuulize yeye mwenyewe....?
kwanza ni watu wa mkoa gani....?
 
Mmh! Hao ni watu wawapi? Kwani Huyo unaetaka kuanae hajakwambia nn anapenda eeeh! Mie naona bora ungeanza na Huyo utakae ishinae kwanza mengine ndio ukamalizia hapa...
 
wazinza wanatokea mkoa wa mwanza kwenye visiwa vya nkome n.k.

Ila wewe mtoa mada unaoa kabila? Unaoa huyo uliyempenda?
 
Hii! kwa wote,

Nimepata mchumba wa kabila la wazinza,
Nawaombeni kwa wale wanao lifahamu kabila hili la wazinza, je wanawake wa kizinza
mila zao zikoje? tabia zao kijami na pia kiunyumba zimeka vipi? wanapendelea nini?
pia naombeni ushauri wenu,

Mchumba au mpenzi,????mimi ninavyojua mchumba tayari umeshapeleka barua ya uchumba na wazazi wamekubali tena wanakueleza taratibu, mila na tamaduni zote za kwao kuanzia mahari hadi ndoa ....Acha ukabila kijana.
 
Jaribu kumchunguza huyo binti tabia, mwenendo na kila kitu. Kuhusu mila zao jaribu kutafuta wazee wa kabila hilo watakueleza mila na desturi zao. Kwa kuchunguza kabila hutopata majibu sahihi/
 
Nashkuru kwa maoni yenu yote ni katika kujifunza, lakini kumbukeni aulizae si mjinga ila anataka kujua haijalishi swali limekaaje ilimradi lime eleweka, nikweli kwamba nimekwisha muliza lakini nae hajui chimbuko lake latoka wapi, anacho jua ni kwamba babu zake walitokeaga mwanza na aliambiwa yeye ni mzinza, cha zaid hakuna,

Halafu kua na uchumba haimanishi yakua lazima muwe mmeisha tambulishana kwa wazazi yaweza kua ni wachumba na ndo mko kwenye harakati za kwenda kutambulishana, ko naweza nkawa nauliza npate kujua nijiandae vipi nisti aibu, maana makabila mengine unaweza ukapeleka zawdi ikawa ni dhihaka ao ukase manono ao ishara ambazo ni matukano kwao,

Lakini pia kunawengine washa owana na washa zaa ndo kwanza wana enda kwa wazazi kutambulishana,

kuuliza kwangu kumetokana na kwamba huyu mpenzi wangu sio mtu anae penda kusimulia sana mambo yake anakotoka mila zao nikimuliza annjibu kiufupi ufupi yameisha,

na pia nimeuliza hivyo nipate jua namna walivyo kitu ambacho kinaweza kunisaidia kuepusha mitafaruku mbalimbali, kwasabu kuna mwengine anaweza fanya kitu ukamwonya mara moja mbili na bado akakirudia kumbe ni asili yao, unapo mjua mtu kiundani si rahisi kumfanyia makosa ao kumwekea hisia mbaya kwasbu tayari unamjua,

Ko wenye moyo wa kunipa mawazo karibu, we unae ona naku boa acha tu,
 
Aulizae ataka kujwa. Kuuliza si ujinga. Kama vile walivyo madam wa visiwa vya Honolulu. Loving, caring, submissive,sexy and obedient. Kuhusu trust, sijui. Nilikaa nae for a short stunt nilipokuwa Nansio Ukerewe. Lakini aliifanya 1 year kuwa kama 1 day. Unfortunately I was transfered to Dar and she couldnot follow. By the way I was still eligible then. Give her a try.
 
wanatoka karibu na kisiwa cha ukerewe,ni wapole sana ata wakikasirika huwezi kujua ila ni wagumu kusamehe na wepesi kulipiza kisasa ata baada ya miaka mingi,wanafanana tabia na wafipa kutoka mkoa rukwa.

Wafipa hatupo hivyo wewe.....
 
Hii! kwa wote,

Nimepata mchumba wa kabila la wazinza,
Nawaombeni kwa wale wanao lifahamu kabila hili la wazinza, je wanawake wa kizinza
mila zao zikoje? tabia zao kijami na pia kiunyumba zimeka vipi? wanapendelea nini?
pia naombeni ushauri wenu,

Huku JF si google jamani..........................!
 
Ni wastaarabu ana ingawa watu wengi wa visiwani huwa ni wachawi sana. Hasa visiwa vya ziwa victoria
 
wazinza wanatokea mkoa wa mwanza kwenye visiwa vya nkome n.k.

Ila wewe mtoa mada unaoa kabila? Unaoa huyo uliyempenda?

Samahani. Kwa taarifa tu, wanatoka katika kisiwa cha Kome sio Nkome. Nkome si kisiwa iko nchi kavu. Kisiwa cha kome kipo ktk wilaya ya Sengerema
 
Ngugu mtoa mada, Wazinza wana tabia fulani (japo si sana) ya ubinafsi na dharau kidogo. Sio wataalamu sana wa kupika hivo km amekulia ktk mazingira ya kijijini mapishi yapo pembeni, na wewe km ni mtu uliezoea mapishi ya Pwani utakutana na mapishi ambayo ambayo si mazuri sana
Kuhusu utamaduni ni watu ambao kitoweo cha heshima ni Sato. Kama wewe ni mkwe watakuandalia sato kama kitoweo cha heshima sana. Inabidi ujiandae siku utakapokwenda kuwatembelea wakwe kijijini wakati wa chakula. huwa wanakula kwa pamoja yaani mnakaa wote chini au kwenye mkeka mnaanza kula. sahani/bakuli la mboga/kitoweo ni moja na mnashare. Mchuzi huwa ni mwingi sana, Ktk eneo lao viazi hustawi sana hivo unaweza kukuta chakula kikuu cha mchana ni viazi na Sato waliopikwa chukuchuku na mchuzi mwaingi. Nimesema ujiandae kwa sababu ulaji wao utakushangaza. wanatumia bakuli moja kwa ajili ya mchuzi na kwa sababu ni mwingi kila mtu akitaka anachukua bakuli hilo anatia mdomoni na kunywa mchuzi ili kushushia kiazi alichokula, so ninyi nyote mnatumia mfumo huo wa kushushia mchuzi ulioko kwenye bakuli moja. Hapo km roho yako ni nyepesi unaweza kutapika au ukaacha kula ila ndivyo wanavyokula.
Naomba leo niishie hapa. nikikumbuka nyingine nitakuambia coz niwahi kuishi huko for about 3 yrs and my parent are living there japokuwa sisi si wazinza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom