Wanawake: Ukimpenda mwanaume mtongoze

Aisee...
 
Hahahah kweli vyuma vimekaza yaan wanaume nanyi mnataka tuwatongoze? bado tu kusema tuwahudumie.
 
Familia nyingi za kawaida zina hudumiwa na akina mama
Huu ndio ukweli hata kama mchungu....familia nyingi hasa hizi za akina sie zinakula kwa akili ya mama
 
ebwana jamaa hyo 'Movie' yako na mkeo jinsi mlivyoakutana na kujuana mpaka mlipofikia nimeipenda mno.
mnastahili pongezi.
Mungu azid ijaalia familia yenu furaha na amani


Doswe Dossena we acha tu, kuna mapenzi ya kweli dunia hii asikudanganye mtu.....ila bahati mbaya tu kuna wengine wanajiingiza kwenye mapenzi yasiyoendana na ndiyo maana mara nyingi utaona wanashindwa hata kuongozana kwa kuoneana haibu kuwa watachekwa. Mume hana muda na mkewe na mkewe kuona mume ni mzigo. Tuache utani, kuna mengi mema mke wangu ananifanyia na ndiyo maana hata wazo la kutoka nje ya ndoa naona ni dhambi, haswa nikikumbuka jinsi alivyo tayari kufa juu yangu, yaani inatisha. Kweli penzi ndiyo uchawi wa kipekee dunia hii ya Mungu, hakuna zaidi yake..... mshana jr nadanganya hapa?
 
Wengi mkitongozwa mnaringa na kuanza kusema sisi Malaya akati ni hisia
 
Nimeipenda hii uliweza kusoma alama za mrembo kukuzimia kila alipokuona.

 
It seems psychology has to be introduced into our schools curricula.

Hapa ni kama tunataka kulazimisha maji yapite ambako siyo mkondo wake!

Haiwezekani, so men has to fulfil their duty as usual. Signal ni attracting factors kwa mwanaume kuchukua hatua.

This is common in African cultural societies, unlike abroad ambako girls wapo conscious japo hata kwa vitendo ku expose direct feelings na hata ku seduce kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…