Wanawake, twawapenda sana, ila...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake, twawapenda sana, ila...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ligogoma, Apr 7, 2011.

 1. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,142
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Jamaa yangu hapa ana mke mrembo haswa na jamaa linampenda kweli kweli mkewe. Tatizo ni kuwa mke ana vijitabia ambavyo jamaa vinamkera saaaana.

  Huyu mwanamke anapenda hela huyu balaa, anafanya kazi ya ualimu na jamaa anakwambia hajawahi kuuona mshahara wake kipindi chote walichoishi mpaka leo first born wao yupo form 2. Hiyo haimjalishi jamaa but kinachomuuma ni pale anapoacha hela ya matumizi shilingi 15,000 kwa siku ili watoto wale vizuri then anakuta chakula ni mboga za majani ambazo hata 1000 hazifiki labda na wali pekee, bila tunda wala nini!!

  Alijaribu kumuacha hivyo kwa muda wa mwezi mzima na mwendo ukawa ndo hivyo na kila akimuonya habadiliki na mbaya zaidi hata hela zinazobaki hazijulikani zinakoenda!!

  Jamaa ili familia yake ile vizuri inambidi awe akitoka job jioni apitie sokoni kununua mahitaji ya home ya kesho yake la sivyo akiacha hela ni maumivu!!

  Sasa jamaa anajiuliza, mshahara wake unaenda wapi achilia mbali mahitaji ya kike. Pia na hela ya nyumbani nayo ndo achakachue jamani? Hata pamoja ya kumjazia gari full tank kila week na service zote za gari?

  Mpendejwe ninyi wanawake jamani!!!
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Tupendeni tu. Mtafanyaje sasa!
  Mkituchukia mtakufa kabla ya siku zenu kwa mawazo
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  najua kinywaji unachokunywa.....naleta
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Mtuvumilie jamani, sisi ndio maua ya ulimwengu. Tunataka usawa, kipaumbele na kipau nyuma kwa wakati mmoja, ili mradi vinilinde mimi na mslahi yangu kwanza.
   
 5. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  I feel you mkuu...si utani hii issue, its exactly what is happening to me. For the sake of being responsible father and husband, unajikuta tu unaamua kunyamaza na kupigana vikumbo na kina mama/dada sokoni ukichagua nyaya na vitu vingine. halafu inauma basi huko sokoni unakutana na wamama/dada wakoresponsible na makapu/mifuko kununua mahanjumati kwa ajili ya familia zao..
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  afadhali maana nina kiu hiyo..
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  wanaume lazima tuelewa wanawake ni wa aina3 ...[1] walioradhi kuolewa (maisha yao yote), [2] wanaoolewa shingo upande/ ili waonekane wako kwenye ndoa (hili ni kundi kubwa) na [3]. wasiotaka kusikia neno ndoa/kuolewa (maisha yao yote) ...kazi ni kwetu waoaji wa kundi la [2]
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  umenikumbusha mbali sana mkuu kwa hii mada.....yaani basi tu... iliwahi kumkuta ndugu yangu mmoja hakika huyu jamaa tumekua wote na tangu chekechea hadi chuo.... kwao amezaliwa peke yake....baada ya kuoa baada kama ya mwaka mama akasafiri toka mwanza hadi arusha kwa mwanae (ndiko anakofanya kazi)...kufika huko jamaa akitoka asubuhi kwenda kazini mama huku nyumbani anakunywa chai na viazi mviringo ndo imetoka hadi usiku......mume akitoka kazini jioni kinaandaliwa chakula kizur kweli ...hapo jama yangu anadhni hata mchana ni hivyo...kumbe sivyo......

  mama akakaa kimya wala hakumwambia mwanae hayo...akapata matibabu ya ugonjwa wake....siku moja mama kaamka asubuhi kafanya usafi wa nyumba wakati huo mke wa ndugu yangu akiwa amelala.....mama akapika ndizi kwa ajili ya chai......basi yule mke wan ndugu yangu akaamka kama saa nne hivi akakuta mama mkwe wake amepiga deki nyumba....ameosha vyombo....na kupika chai na alikuwa amekunywa chai tayari na ndizi...
  yule mke wa ndugu yangu alipoamka akaoga (chumba ni self) then akaja sebuleni na kumkuta mama mkwe amakaa sebuleni anaangalia magic africa..binti akapitiliza hadi jikoni akanywa chai huko na baada ya hapo akarudi sebuleni na kumwambia mama mkwe kuwa aoshe vyombo vya chai......yule mama akasema sawa.....then binti amwambia kwa nini amemenya ndizi na maganda ya ndizi hajatupa jalalani...akaanza kumtukana mama mkwe wake

  Mungu sio Ivuga basi ndugu yangu akapata dhalula kule ofisini na kurudi nyumbani alisahau flashi na ilikuw na document muhumu sana..ile kufika nyumba akakuta mama yake analia na alipouliza mama hakusema kitu na mke wakti huo amejifungia chumbani...sasa mama wakati analia akawa anataja maneno flani flani kama vile ..mwanangu nimekulea kwa shida lakini mke huyu atakuua mapema...sasa ndugu yangu akahamaki na kumkurupusha mke wake chumbani na kumuuliza umemfanya nini mama....yule mke nae bilaakili akahamaki na kusema muulize yeye nini kinamliza.....

  baada ya mda mama akasimulia kila kitu A to Z......ndugu yangu alilia sana na kusema mama mbona hujaniambia kama ulikuwa huli mchana?...nilipigiwa simu na ndugu yangu a kuniomba niende nikasafiri na nilipofika huko nikapewa hii habari na ndugu yangu na ndugu wa mke walikuwepo.....jamaa alichofanya siku ile ni kuongea kwa kifupi sana kuwa mama ni kila kitu kwake...ameteseka kumsomesha....ametembea bila viatu.....na mama yake amemsomesha kwa shida then leo mke anakuja anamtesa mam yake?? akasema nimewaita hapa kuwa mashahidi na muujue ukweli sitaki uzee wangu uwe wa manungu'niko...mama hakutaka kuniambia na nisingerudi nyumban siku ile na kukuta mama analia nisingejua, .....

  yule dada aliachwa na ndoa ikaishia hapo.....alilia na kuomba msaada lakini haikusaidia......nakumbuka alikuwepo mjomba wake alimpiga makof yule binti pale hadi tukamshikilia....... kuanza upya sio ujinga ndugu yangu hajaoa mpaka leo


  kisa kirefu ( sorry 4 this)
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  nimekugongea thanks mkuu..........umenena vema
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  Edson huyo bi dada kwenye hii story yako alizidisha....khaaa....hata kama ni utu ulimtoka....kama yupo hivyo si angevumilia tu kwa muda mpaka huyo mama aondoke.....wa aina hiyo hafai kuwa mke
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hao wanawake wa hivo nao wamezidi, hata chakula mtu ananyimwa, tena aliyekuzalia mume? na huyo anayewanyima wanae chakula bora anaficha pesa nae mmmh, what kind of a mother is that? Maana i would wish for the best food for my kids hata kama iweje.
   
 12. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  This is so sad really, imagine sio tu mama mkwe, kuna wanawake wanaowatesa mahousegirls wao mpaka unashangaa...hivi ukinyanyaswa na bosi wako kazini unajisikia inavyouma ....kuna baadhi ya wanawake wanakosa hekima kabisa...

  This reminds me of my weekly market shopping...lakini si vibaya wanaume kununua chakula sokoni au supermarket na inapendeza zaidi mkiwa the whole crew! Kids included :)
  Mhandisi
   
 13. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #13
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Sio vizuri kufanya generalization ya wadada. I know there are wonderful women out there ambao wanaweza kumtreat mama mkwe mpaka ukadhani ni mama yake mzazi. Lakini to be honest: I think kwa swala la mama yangu..my wife should never push that envelope beyond the point. Kwa kweli fanya mengine usimfanyie kitu mbaya mama yangu. Maana what this woman did in my life..she is my world on this planet....Mungu ndo anajua. Leo nioe mke afanye ujinga wa huyo dada hapo juu? I am sorry, you will have crossed the line and that will be the end of the story between us. Mara mia unifanyie kitu kibaya mimi mume wako kuliko mama yangu.. Ofcourse..all factors constant (maana kuna mama wakwe wengine nao wana visa vyao).
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huyu dada hafai, ana roho mbaya kupta maelezo! Utamnyanyasaje mama wa mwenzio hvyo? Bora alvyoachka manake anaweza mpa m2 sumu. Nmecktka sn. Kn mama wakwe wana vsa ila ucmtende vbya hv jaman! Alaaniwe huyu mdada. Pole ma mkwe kwa kushndshwa njaa!
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wanawake wa aina hii wapo,wengne hawatak ndugu wa mume na hata ndugu zai wenyewe
   
 16. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,142
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, sijajua wanakuwa na matatizo gani ingawa wanadai kuwa wao ndo maua ya dunia hii!!!
   
 17. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #17
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hii ni post ya mwaka kha Husninyo wewe bana nimecheka kweli
   
 18. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #18
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160

  Hii ni post ya mwaka namba mbili.........
   
 19. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanawake wa aina hii huwa wanawavunja sana moyo waume zao, yaani hata watoto wake hawaonei huruma sababu ya tamaa zake tu zisizo na mbele wala nyuma
   
 20. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #20
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  wallah tena ukimpelekea mtitu n bonge la movie
   
Loading...