Wanawake tukumbushane wajibu wetu

maliyamtu

JF-Expert Member
Nov 29, 2017
2,135
3,866
Salam sana jamvini

Jamani napenda niende moja kwa moja kwenye mada.

Kumekuwa na wimbi kubwa la wanawake wanaolalamika kuhusu mahusiano ama ndoa zao kukosa mwelekeo mzuri na zingine nyingi kuvunjika kutokana na sababu mbalimbali. Hatahumu jukwaani kumekua na nyuzi nyingi mno za wanamama wakizungumzia changamoto za ndani ya ndoa au mahusiano yao.

Katika zama hizi tulimo sasa wanawake wengi tumekua tukisahau kutimiza wajibu wetu kama wake na badala yake tunaingilia majukumu ya wanaume zetu,tumesahau kabisa kwamba tunatakiwa tufanye nini na nini tusifanye kwa waume zetu.

Napenda kuongelea kuhusu kupenda na kupendwa,wanawake wengi wa sasahivi tunataka tuanze sisi kuwapenda wanaume kitu ambacho ndio chanzo cha mahusiano au ndoa nyingi kuvunjika kwa maana mwanaume anakua hajampenda mwanamke sawasawa hivyo baadae mambo yanakwenda fyongo.

Wanawake wenzangu tujifunze kuwaacha wanaume watupende wao kwanza ndipo nasi tuwapende,,upendo huo utadumu kwa muda mrefu maana hata maandiko matakatifu yametuasa kwa kusema "Enyi wake watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu" hivyo basi wanawake wajibu wetu ni kuwatii waume zetu kwanza hayo mambo ya kupenda tuwaachie wao wanaume. Maana nao maandiko yamewaambia hivi "Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa".

Tukirejea kwenye zama za nyuma kidogo zama ambazo vijana walikua wakitafutiwa wake na wazazi wao tutaona familia ya mwanaume ndo ilikua ikitafuta mke kutoka familia jirani zenye watoto wazuri na walio na tabia njema za kutii na kuheshim,hiyo ni sababu tosha ya kusema kwamba tusiangalie tunapenda wapi bali tuangalie tunapendwa wapi na tuonyeshe utii na heshima pale tunapopendwa.
 
Vise versa is true. Kudumu kwa mahusiano kunategemea na wahusika ambao wamo wana azma gani.. mwanamke ana operate katika emotional state while mwanaume ana operate in logic. Siku zote haitawezekana mwanamke na mwanaume kuwa sawa.. kwenye mahusiano yoyote yale mmoja wao lazima awe na power juu ya mwenzake other wise mahusiano hayata dumu. And that is the truth
 
Back
Top Bottom