Wanawake Togo wasusia ngono kudai Mageuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake Togo wasusia ngono kudai Mageuzi

Discussion in 'International Forum' started by MAKOLE, Aug 29, 2012.

 1. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  Wanawake nchini Togo, wametakiwa kususia kitendo cha ndoa kuanzia Jumatatu wiki hii kama njia ya kushinikiza serikali kuleta mageuzi.
  Kampeini hiyo yenye kauli mbiu ''Juhudi za kuokoa Togo'' imeanzishwa kwa ushirikiano na mashirika tisa ya kijamii pamoja na vyama saba vya upinzani pamoja na vyama vingine vya kijamii.
  Kiongozi wa upinzani, Isabelle Ameganvi alisema kuwa kususia ngono huenda ndio itakuwa silaha inayofaa kuweza kuleta mageuzi ya kisiasa.
  Muungano wa vyama hivyo pamoja na mashirika yasiyo ya kijamii unataka rais Faure Gnassingbe, ambaye familia yake imeshikilia madaraka kwa miaka mingi waweze kuondoka mamlakani.
  "tuna njia nyingi za kuwashinikiza wanaume kuelewa tunachotaka sisi wanawake'' alisema bi Ameganvi, kiongozi wa tawi la wanawake la muungano huo.
  Alisema kuwa yeye ameweza kushawishiwa na mgomo sawa na huo nchini Liberia mwaka 2003,ambao walitumia njia ya kususia ngono kushinikiza amani.
  "ikiwa wanaume watakataa kusikia kilio chetu, tutalazimika kufanya maandamano ambayo yatakuwa makali zaidi kuliko mbinu hii ya kususia ngono.'' aliongeza bi Ameganvi
  Togo imekuwa ikiongozwa na familia moja kwa zaidi ya miaka arobaini.
  Je, njia hii huenda ikawa silaha madhubuti kwa hali ya kusuasua kwa utawala hapa Tz? Tafakari....
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kama sofia simba vile. hahaaa!
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  wakisusia kwa hapa TZ zitakuwa habari njema sana kwa machangu na nyumba ndogo!!
   
 4. princeamos

  princeamos Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DUH! hii nilaana
   
 5. a

  afwe JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ingependeza kama ungetoa preamble kidogo! Imekuwakuwaje mpaka wakasusia
   
 6. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Done, limetekelezwa
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  hata togo wapo
   
 8. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hao machangu na nyumba ndogo sio wanawake?
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  wapo kikazi zaidi sio kisiasa!!
   
 10. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kwani wamama wote walioolewa wa Togo ni wanasiasa?
   
 11. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  sijawahi kufika Togo kwa hiyo sijui hilo muulize aliyeanzisha thread! iam sorry!!
   
 12. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
Loading...