Wanawake stress nyingine tunazitafuta

Ukumbuke wewe ni mke sio kiranja wala hakimu. Ukiyazingatia haya utaishi kwa amani tele ndoani
Duuh kwahiyo ukiwa mume ndo yakupasa kufanya makosa kwa makusudi ukitegemra mkeo akusamehe na akuvumilie kila kitu na siku? Kwa hali hii wanawake mbona tuna kazi kwenye ndoa

Kwa kweli mimi ndoa zinisubiri tu hizi za kutaka mwanamke peke yake ndo ajicommit? Labda zikija za aina nyingine ndo nitaolewa hata kesho ila kama ni hizi basi Mungu anichukue nikiwa single tu maana hata yeye hakuumba ndoa za aina hii
 
dada una roho ngumu sana,,,, na unavumilia mengi....ni wachache sana wenye moyo chuma kama wewe......wao kila sms wanataka wajue ni nani.......tena siku hizi hawaziosomi,,,, wanajitumia screen shot....hongera zako
 
Shida sio makosa, usikae hapo nyuma kufuatilia hatua za mume. Umeagwa kwa amani mtu kaenda job, katoka lunch mmebonga. Yuko kijiwe na wana umeagwa na unahudumiwa freshi.

Sasa kazi ya kuanza kufukunyua simu ya mume bila ridhaa yake au kwa kificho ndio linalosemwa hapa ni kujitaftia matatizo bila sababu.

Na labda nikusaidie mume wa kukusujudia kama mtoto hayupo. Labda awe hajiwezi kiuchumi na hana nguvu za kiume sawasawa. Otherwise tafta hela ukamate boya umhudumie.
 
Kufukunyua mara moja moja sio mbaya
 
Sometimes humu kuna wanawake mna mawazo kuntu sana
 
Kwa hilo wanawake wengi sana tunafeli,binafsi sihangaikagi na simu ya Mpenzi wangu, aongee wapi achati sijui afanye nini wala sijipi presha, maisha mafupi kwann niteseke kwa vitua ambavyo naweza kuvihandle???Unakuta wamama wanafundishana kuhack simu za wanaume wao, nawaangaliaga nawaona wajinga fulani hivi, unahack unapata presha unakufa unamuacha anaendelea na maisha, ya nini bwana, mie nnachojali ananipa haki yangu vzr ananitimiza vyote nnavyopata basiiii,nampa uhuru wake na maisha yanasonga,na hatujawahi gombana eti kisa simu
 
Mimi nadhani bado hatujaelewana hakuna anayetaka mume wa kumsujudia bali ninachojaribu kusema ni kwamba kama wewe mume kufuatiliwa na mkeo hautaki kwanini na wewe umfuatile mkeo? Kama wewe hautaki mkeo akufuatilie halafu wewe unamfuatilia mkeo hiyo ina maana gani?

Ina maana hayo makosa unayotaka kuyakuta kwenye simu yake unataka uyafanye wewe tu ila yeye asiyafanye? Unajua wanaume mnashindwa kukikubali hiki kitu kimoja kinaitwa KARMA yaani 'what goes around comes around' kila unalolifanya haijalishi liwe ni zuri au baya lazima likurudie kwa namna yoyote ile na wakati wowote ule hauwezi kuizuia hiyo hali

Yaani ukichapa wake au watoto wa kike wa wenzio na wewe wako lazima watachapwa tu sasa hauwezi kulazimisha wewe uwe malaya halafu upate mwanamke muaminifu wapo wanaopata wake wa hivyo lakini wajuvi wa mambo wanasemaga "in every general rule there is always an exception"

Kwahiyo katika hiyo general rule ya KARMA hao ambao wanayofanya hayawarudii basi ndo exception yenyewe lakini ni asilimia chache sana sasa nyie wanaume mnataka mfanye hayo kwa wanawake wengine halafu yasijirudie kwa wake zenu na yakijirudia ndo mnaanza kusema wanawake tunafanya makusudi ili kuwalipizia sijui tunashindana na nyie hizo kauli mnatoa wapi jamani?

Halafu kwani shetani huwaga anawatendesha dhambi wanaume tu? Yaani hiyo dunia mnayoitaka ambayo wanaume wanafanya makosa halafu wanawake hawafanyi makosa haipo haijawahi kuwepo na haitakuja kuwepo mtu akipata mke au mume pasua kichwa ndo wake huyo

Anatakiwa akumbuke tu mambo aliyofanya kwa wenzie huko nyuma halafu Mungu alivyo wa ajabu sasa mara nyingi watu wanapata wenza wa kufanana nao tabia with the the exception ya baadhi ya watu sasa whether you are among or not among the exceptions wewe shukuru tu Mungu yaani shukuru kwa yote
 
Na katika huo uhuru ndiyo anapata na dili ya buashara na wewe na watoto mkapelekwa Zanzibar weekend
 
Ndo hivyo mkuu.. mpaka sasa nshamtoa marks za kutosha, ndoa haiwezi.
Naona mnataka muachwe mchepuke kwa uhuru na mkipata wanawake wanaowaacha mchepuke kwa uhuru ndo mnaona wanafaa kuolewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…