Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,233
- 113,610
Ni kweli NN, ukaribu wa baba kwa mtoto ndio kinga pekee inayoweza kumwepusha mtoto na manyanyaso/vipigo kutoka kwa mama wa kambo...
Taire! Taire!
Ila cha kushangaza kuna wanaume wajinga sana, eti libaba linahama upande wa mwanae na kuwa upande wa mkewe, kila anachoambiwa na mtoto ni uongo na kila anachoambiwa na mkewe ni ukweli, mtoto anabaki peke yake, hana wa kumsapoti wala kumweleza shida zake...hapa atanyanyasika mpaka apate akili ya kiutu uzima aweze kujiokoa peke yake.
Mijanaume kama hiyo inahitaji kwenda kusafishwa nyota.
Mama wa kambo huwa wanapima upepo wa baba akikuta libaba lege lege basi huyo mtoto cha moto atakiona, ila kama baba anamsimamo na yuko upande wa mtoto kamwe hatathubutu kumnyanyasa... Mtoto anajenga kujiamini na ataishi kwa amani...
Ni kweli kabisa. Wakishakusoma tu na kuona huna msimamo wala kanuni mtoto anaweza kupata shida sana. Ila wakijua kuwa una msimamo thabiti watajiuliza mara mbilimbili kuleta sokomoko kwa sababu wanajua lazima patachimbika bila jembe wala shoka.