WANAWAKE roho mbaya namna hii mnaitoa wapi mnapokua MAMA WA KAMBO? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WANAWAKE roho mbaya namna hii mnaitoa wapi mnapokua MAMA WA KAMBO?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BAGAH, Mar 22, 2012.

 1. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  huwa sielewi mwanamke anapopewa jukumu la kulea mtoto ambaye si wake (namaanisha mama wa kambo) anakua na roho ya tofauti (mbaya)....
  ni mara chache unasikia mtoto anaelelewa na mama wa kambo akawa na raha katika maisha!...

  huwa ni fujo mvutano mafarakano kusingiziana,ili mtadi tu kupanda na kushuka kwa majambo!...
  je haiwezekani mtoto na mama wa kambo kuishi pasi majungu na mivutano???

  je baba wa mtoto nae ana nafasi gani katika hili sekeseke?

  GTs your highness!.
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Napita hapa,...maake sijalelewa na mama wa kambo.
   
 3. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Igwee!..ila waweza kua na machache juu ya hili!
   
 4. S

  Skype JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Halafu nimegundua mtoto anayekulia kwenye misukosuko kama ya kina mama wa kambo hua anakua imara sana kifikra awapo mtu mzima. Pamoja na hayo mimi napingana sana na unyanyasaji unaofanywa na BAADHI ya mama wa kambo, chondechonde kinamama na kinababa, inapaswa kutambua kua mtoto wa mwenzio ni wako pia.
   
 5. Zabibu

  Zabibu JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mimi nimelelewa na mama wa kambo karibia maisha yangu yote maana mama yangu alifariki tangu nikiwa darasa la kwanza lakini sijawahi kunyayasika kwa njia yoyote ile huyu mama amekuwa mtu mwenye upendo sana na nimejifunza mengi kutoka kwake na nitaendelea kumshukuru sana maisha yangu yote.

  SIO MAMA WA KAMBO WOTE WANA ROHO MBAYA .
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ingawa sio wote wenye ukatili ila wapo na ni wengi kuliko wenye wema kwa watoto wa wenzao.
  Mimi ni mhanga so najua ubaya wa hawa watu dingi akirudi huwa anajikomba ili tusianike maovu yake dingi akiwa hayupo.
  Mbaya zaidi wengine ni waumini wa mstari wa mbele wa madhehu tena ni viongozi
   
 7. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Zay nimekukubalia vyema!...mshike sana huyo mama wako wachache!..
   
 8. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  tena usiombe ukute dingi nae amekua zoba kwa uyo mama...lolote analoambiwa na mama anaamini na kukufokea ww!!
   
 9. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inategema na wanawake sio wote, kuna mwanamke mimi namjua analea mtoto wa mme wake kwa mapenzi zaidi, kuliko watoto zake wenyewe wa kuzaa na huyo mme wake.

  Sio wanawake wote wana roho mbaya, matatizo sisi wanaume tunatazama upande mmoja tu, hatutazami upande wetu pia.


  Usisahau kuna parcentage kubwa ya wanaume wana roho mbaya kuliko wanawake :cool2:
   
 10. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  huwezi umiza kichwa sana kuwaza roho mbaya ya baba kama ile ya mama!..kumbuka mama ana muda mwingi wa kulea/kukaa na mtoto kuliko baba...so ni rahisi kuona effects zake (good/bad)
   
 11. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,128
  Likes Received: 942
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Zabibu sio mama wakambo wote wana roho mbaya. Hapa ile methali ya samaki mmoja akioza wote wameoza ndo inafanya kazi kwa mama wa kambo. Naijua familia moja ambayo mama alifariki. Mtoto wa mwisho wa huyu marehemu alikuwa darasa la sita. Baba( mume wa marehemu) alioa mke mwingine. Mama huyu mpya aliwajali sana watoto aliowakuta, ila watoto kwa kusikia kwamba wamama wakambo ni wabaya, wakawa hawamjali wala kumheshimu huyu mama mpya. Lakini mama huyu akaendeleza upendo wake na kupuuza visa anavyofanyiwa na watoto. Yule aliyekuwa darasa la sita akachipuka na kufaulu kwenda sekondari ambako alifaulu division I form four na kuendelea form five na hatimaye Chuo kikuu. Keshamaliza na amepata kazi nzuuri.

  Pointi hapa ni kwamba kama yule mama aliyeolewa kwenye hii nyumba angekuwa na roho mbaya basi huyu mtoto aliyekuwa darasa la sita angenyanyasika na asingeenda kokote. Pia mara nyingi watoto ndo huanza chokochoko na mama wa kambo ambaye naye hurudisha mapigo. Inapotokea hivyo watu bila kujua chanzo huanza: 'Ooh! Mama mbaya, anatesa watoto'.
  Kwenye mahusiano ya watoto na mama wa kambo yawapasa watoto wamheshimu kama mama yao, wasichukulie kwamba kwa kuwa ni mama wa kambo basi ni mtu mbaya.
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sio wamama wote Bagah ila asilimia kubwa roho zao ni mbaya sana...

  Ukichukua wamama wa kambo 10 wawili kati yao ndio wana roho nzuri..
   
 13. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  habari yako shem wa ukweh!..
  nakubaliana na ww kwa asilimia zote SL
   
 14. Kayla

  Kayla JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ubaya mdogo hufuta wema uliokithiri..ni kawaida kwa binadamu kulaumu pale mambo yanapokwenda kombo au anapotendewa ndivyosivyo hata kama ni haki yake kutendewa hivyo...hivyo basi hata mtoto akilelewa na mama wa kambo akatendewa wema lakini ikitokea akafanyiwa sivyo wema woote husahaulika...
   
 15. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kwakweli msitukumbushe sie tulioteseka jamani,huwa sielewi ni nn hasa inakua ivo mana hatukuwa wakorofi wala nini
  ila Mungu hulipa hapahapa duniani,now tuko ngangari kama "skype avosema"
   
 16. S

  Skype JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kumbe tupo wengi tuliokulia ktk mikono ya chuma! Tujipe pole kwa mateso ila tujipongeze kwa kufuzu maana haikua kazi ndogo kuvumilia kichapo, matusi, kejeli, kulala au kushinda njaa, nk.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Baba wa mtoto akiwa karibu na mtoto wake na kumpenda kwa dhati atahakikisha huyo mama wa kambo hamnyanyasi mwanae.

  Kwangu mtoto anatangulia kabla hata ya maslahi yangu. Asilani siwezi kuruhusu mtoto wangu kukosa furaha na amani kisa mama yake wa kambo.

  Ndiyo maana ni vyema wazazi wakawafundisha watoto wao kutokukubali kunyanyaswa na yeyote yule. Mimi sioni ubaya wowote ule kumfundisha mtoto wako kuwa hakuna mwenye haki ya kumpiga, kwa mfano.

  Na ikitokea kapigwa basi naye apigane. Heshima wakati mwingine ni lazima mtu uitafute la sivyo utafanywa mkeka.
   
 18. S

  Skype JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Ngoja niyapitie haya mafundisho huenda yakanisaidia mbeleni ktk kulea watoto, I highly appreciated this useful piece of advice.
   
 19. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli NN, ukaribu wa baba kwa mtoto ndio kinga pekee inayoweza kumwepusha mtoto na manyanyaso/vipigo kutoka kwa mama wa kambo...


  Ila cha kushangaza kuna wanaume wajinga sana, eti libaba linahama upande wa mwanae na kuwa upande wa mkewe, kila anachoambiwa na mtoto ni uongo na kila anachoambiwa na mkewe ni ukweli, mtoto anabaki peke yake, hana wa kumsapoti wala kumweleza shida zake...hapa atanyanyasika mpaka apate akili ya kiutu uzima aweze kujiokoa peke yake.


  Mama wa kambo huwa wanapima upepo wa baba akikuta libaba lege lege basi huyo mtoto cha moto atakiona, ila kama baba anamsimamo na yuko upande wa mtoto kamwe hatathubutu kumnyanyasa... Mtoto anajenga kujiamini na ataishi kwa amani...
   
 20. father-xmas

  father-xmas JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  inasikikitisha kuwa ulichokisema ni kweli kwa asilimia nyingi..........................!
  ila wapo mama wa kambo wazuri sana tu...................hata hivyo huwa najiuliza.............mtoto ni mtoto lakini kinachomshinda mama kumpenda mtoto ambaye hajamzaa ni kitu gani.............!......ingekua vizuri kama tungepata wamama wakambo tukawasikia maelezo yao...................labda tungeelewa kiini cha roho zao mbaya...................!
   
Loading...