Wanawake, Perfect Guy (Man) wako ana sifa na vigezo vipi?

Wanawake, Perfect Guy (Man) wako ana sifa na vigezo vipi?

Thread Starter

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2017
Posts
1,392
Reaction score
1,070
Habari zenu wadau, wakubwa kwa wadogo... Natumai mko poa na mnaoumwa Mungu awajalie unafuu ikawe heri

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada

Nina swali ambalo nahitaji majibu na ufafanuzi kutoka kwa watoto wa kike sanasana (wajuba wa kiume sio mbaya pia).

Hii ishu imenitokea mimi kabisa, Kuna msichana mmoja nilianzisha mahusiano nae mwaka jana kwenye mwezi wa pili anaitwa Anita (sio jina rasmi), nilimjua kupitia mfanyakazi mwenzetu tunaefanya nae kazi ambae ni kama kaka wa mbali

Kaka yake alinipa sifa zote kuhusu huyo mdogo mtu na nikamuelewa kwa kuwa nilikuwa na hisia za kumpenda, basi akanipa namba tukaanza mawasiliano. Pia aliniunganisha na Aunt yao kwa kuwa kuna muda alikuwa akiongea nae kwa Simu.... Aunt alinihusia endapo labda nitaonesha interest kwa mtoto wao niwe makini na nimtunze kwa kuwa mtoto wao amelelewa kwa miiko na maadili, kwa hiyo hatapenda nimzingue(nimsumbue) na alifurahi kusikia sifa zangu kutoka kwa Kaka yake na huyo Anita

Siku ya kwanza kuwasiliana nae Anita

Kwa kweli sikuamini kwani nilikuwa nawaza maswali yao kama kawaida Umetolea wapi namba yangu, Wewe nani, Mara tusijuane sikujui n.k... Msichana yule alinipokea vizuri na nikaanza kujitambulisha taratibu, maswali ya umetoa wapi namba yangu na nani wewe niliyapangua kwani nilimwambia ni yule Bro wake ndio kanipa halafu ukizingatia Bro aliwahi kuniconnect na Aunt yake mmoja hivi katika kudodosa A B C's za yule msichana...

Basi siku zikaenda wewe miezi ikakata tukawa tunawasiliana, ikafika kwenye mwezi wa 5, Anita akataka kuniona mimi mubashara and not through calls or whatsapp...

Nakumbuka tulikutana mitaa ya Manzese kwenye hotel moja hivi ipo mitaa ya Manzese, inaitwa Gold sijui silver paradise?

Siku ya kukutana mimi ndio nilimtangulia kwa kuwa ndio nilisuggest hapo na yeye kumuonesha aliridhia kwa sababu alitaka sehemu iliyotulia na penye upepo... Basi tukaonana nikamkaribisha, tukala, tukanywa, tukaongea na tukayajenga... Nikamuelezea nia yangu ya kutaka kuwa nae but siku hiyo hakueleweka moja kwa moja...

Basi mida ya usiku saa 3 tukaagana kwa kuwa yeye anakaa Kinyerezi ikabidi nimtangulize hadi Tabata mi nikarudi zangu Ubungo nikapanda Mwendokasi hadi Kimara Korogwe nyumbani...

Basi tukawa tunawasiliana kawaida na mambo mengine yanaendelea..

Sasa tuje kwenye kiini cha mada

Katika kumchunguza yule msichana, niligundua kuwa anaishi kwake amepanga na pia ni Single (though alinambia alikuwaga na mahusiano huko nyuma akaachana na msela kwa sababu ya kucheat kwa jamaa), ana kazi yake ya maana inamuweka mjini... Ana umri wa miaka 25, mwaka huu mwezi ujao hapo anasogeza +1 na kuwa 26.. Msichana mmoja hivi mpole, mstaarabu anajiheshimu na ni mcheshi sana... Elimu ipo sio haba

Sasa katika ongea ongea zetu hizi (huwa anapenda kupiga story sana, hasa za maisha ya kawaida, mahusiano na utani wa hapa na pale) ikaja ishu yangu ile niliyomtongoza na kumwambia kuwa nataka awe my wife tujenge maisha... Akawa anasema;

Nanukuu " Jay sio kwamba sikupendi hapana ni kwamba Nahofia kukurupuka nisije nikakukubalia halafu ukawa sio sahihi kwangu halafu you know sisi Catholics tukishafunga ndoa ndio kifungo cha maisha, sitaki kufanya maamuzi yaje kunigharimu..kwa hiyo hapa nawaza Mungu anisaidie" mwisho wa kunukuu

Nikamuuliza Who is the Perfect guy/man ambae unamtaka? akawa hanipi jibu la kueleweka ila alichosisitiza anataka Real love, upendo wa dhati kutoka moyoni...hivyo vingine tutarekebisha

Mimi kama mimi Jay nikajiangalia huku na huku nikajisemea Kama kazi ipo tena ya kudumu, Pesa sio shida ya kuhudumia familia ipo na biashara pembeni na Ajira rasmi nnayo...nikawa najiuliza sasa anakwama wapi huyu msichana au anahisi akinipa nitamkimbia na wakati angejua akinikubalia Penzi lake nitalienzi na nilijiapia huu "ujana ujana" nitauacha pindi nitakapokuwa nae... Najiuliza kitu gani kwenye mapenzi nitashindwa kuprovide (Care, Attention, Affection, Love,Sex, Money) nakosa jibu hadi leo kwa msichana huyu ambae Moyo wangu umetokea kumpenda...

Au anataka mwenye magari, majumba, mapesa mengi na luxuries za kumwaga ambazo mimi sina au? Au labda ana mtu mwingine hataki kuniambia na anatuweka kwenye mizania kutupima? Aaaaaah nachoka mimi 😖😩

Ingawa kuna kipindi naongea inaonekana kama ana nia ya kuwa na mimi na siku zingine haeleweki ( Yaani Chemical Equation kuna muda inabalance na kuna muda haibalance kabisa)

Sasa swali langu kwenu wanawake na wadau wengine... Perfect guy kwenu ni yupi?

Excuse me kwa Bandiko refu 🙌🏽
 
Japo Uzi kama gazeti ila sikiliza

[emoji23][emoji23]Bro Jo wajina pole sana, huyo mwanamke inaonyesha anacheza na akili yako...

Siku ukipata muda Kaa nae chini mtulize mwambie kwa msisitizo "NO BODY IS PERFECT" hakuna aliye mkamilifu, aliyekamilika duniani hayupo, watu wanavumiliana madhaifu yao wanaoana

Akimtaka huyo Perfect guy mwambie akamchongeshe VETA au SIDO

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Halafu kumbuka wanawake hawajawahi kueleweka wanataka nini!
 
[emoji871]
IMG_20200613_162848.jpg
 
ila unaona huyo anita wake Kama anakuja hivi halafu anakataa, yaani wanawake aisee[emoji23][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom