Wanawake njooni mseme ukweli

Wanawake njooni mseme ukweli

sheremaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Posts
4,452
Reaction score
10,930
Nawasalimu wote kwa upendo na hekima pia hongereni kwa majukumu yenu ya kila siku...twende kwenye mada sasa

1. Wanaume wengi tunahangaika kujua/kufahamu hasa kwenye swala la mapenzi nyie wanawake mnapenda kitu gani kutoka kwetu..?

2. Naomba wanawake mseme ukweli mnapenda nini hasa kwa wanaume

3. Mnapenda wanaume wa aina gani,wakorofi,wapole,walokole,wasumbufu,wakatili..

4. Mnapenda mwanaume akutreat vipi?

5. Mfano mkiwa mnaishi mbali mnapenda mawasiliano yenu yawaje hasa kwenye simu??kuongea sana au kidogo tu..
Mana kuna wanaume wanasema usizoee kuongea na mkewako kwenye simu zaidi ya nusu saa!???

6. Mnapenda mwanaume awe na muonekano upi hasa uvaaji na muonekano wa mwili wake uweje yani.

7. Mnapenda kuskia kuwa mwanaume wako anamwanamke mwingine zaidi yako??mnajiskiaje mkiskia hivyo???

8. Mnapenda mwanaume ambaye haeleweki eleweki kama anakupenda au hakupendi!?yani asiyeonesha mapenzi kwa 100% kwako..

9. Mfano ukiwa mbali na mpenzi wako nini kitasababisha uchepuke?tamaa ya ngono au vishawishi na ukichepuka unajiskiaje

10. Mfano ukiwa unaishi na mume wako nini kinasababisha uchepuke ?? kama huyo mwanaume anakutumizia mahitaji kwa kadri alivyojaaliwa

11 UKIWA MBALI NA MUME WAKO UNAWEZA KUKAA MUDA GANI BILA KUFANYA MAPENZI

Kwa hayo maswali machache nawaombeni mnijibu kwa upendo na ukweli kabisa..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maswali kweli yako targeted kwa wanawake maana sijaelewa kabisa. Ila ngoja nibaki humu niwapigie kelele.

Tuwapigie kelele waje waseme japo kidogo..
Maana maswali mengie ambayo ni elekezi kwa wanawake huwa tunajijibu sisi wanaume
 
Unataka kujua mawazo ya wanawake wote ili iweje, wewe kama umepata manzi muulize maswali akujibu kulingana na yeye.

Be crazy, Be Weird, Be whatever coz life is too short to be anything but HAPPY.
 
1: Tunapenda kufahau suala lake la kiuchumi.

2: Ucheshi, kiasi na busara.

3: Wapole

4:like a queen

5: kuongea kiasi ila kuchat kila wakati.

6: Avae apendeze yaani awe mtanashati.Asivae hovyo hovyo. Mavazi yawe yenye hadhi na itategemea sehemu anapoenda. Na awe msafi.

7: Hamna mwanamke anayependa kusikia
mwanaume wake ana mwanamke mwingine. Inaumiza na kutia kichefuchefu kwa pamoja.

8: tunapenda wanaoonyesha wanatupenda kwa vitendo. Hata kama hawasemi.

9: Hatuchepuki.

10: Hamna jibu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
1: Tunapenda kufahau suala lake la kiuchumi.

2: Ucheshi, kiasi na busara.

3: Wapole

4:like a queen

5: kuongea kiasi ila kuchat kila wakati.

6: Avae apendeze yaani awe mtanashati.Asivae hovyo hovyo. Mavazi yawe yenye hadhi na itategemea sehemu anapoenda. Na awe msafi.

7: Hamna mwanamke anayependa kusikia
mwanaume wake ana mwanamke mwingine. Inaumiza na kutia kichefuchefu kwa pamoja.

8: tunapenda wanaoonyesha wanatupenda kwa vitendo. Hata kama hawasemi.

9: Hatuchepuki.

10: Hamna jibu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Umejibu vyema, ila number 9 ingefaa ujibu kwa niaba yako.
Kuna wake za watu nawafaham lakini wanachepuka ilihali familia zao zipo vizuri kiuchumi pamoja na mahitaji yote.

Au ni kutoridhishwa kitandani?
 
Namba 9 imekaa vyema.
Mtoa mada yeye anafanya kitu kama research , mwisho wa siku atafanya evaluation apate jibu mkuu
Umejibu vyema, ila number 9 ingefaa ujibu kwa niaba yako.
Kuna wake za watu nawafaham lakini wanachepuka ilihali familia zao zipo vizuri kiuchumi pamoja na mahitaji yote.

Au ni kutoridhishwa kitandani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliandika kujibu yote ndefu ilikuwa napost siioni.

Aisee kuandika tena ni ishu mkuu wangu.
 
Tatizo mnatuchukuliaga kwamba tupo very complicated wakati sivyo.

Mwanamme asimame kama mwanamme, abebe majukumu ya familia kwa maana ya kutimiza mahitaji ya familia.

Amheshimu na kumjali mke wake kwa hali na mali. Kumpa company na sio ya kumchungulia kyupi tuuu. Na aiangalie familia ya wakwe kama anavyoangalia ya wazazi wake pia. Kushauriqna katika masuala ya kifamilia.

Kuwa mwalimu ama kiongozi wa mke wake pale anapoona amekosea step. Kumfundisha mambo mapya mfano siasa, ama kukaa nae kuangalia mpira kumfundisha rules etc.

Kumpiga turumba. Hili neno turumba mara ya kwanza na mwisho nililisikia kwa baba yangu fundi magari wakati navunja ungo. Hakukaa akaremba maneno yake. Alituambia tu pigweni turumba weee mpaka ifuke moshi. Nilipokuwa ndo nilielewa. So ndugu msomaji, mpige mkeo turumba weeeee ndo miongoni mwa yanayotakiwa katika ndoa.
 
Wanawake wanataka ela !!! ukiwa na ela mwanamke automatic tu anatulia

Narudia tena tafuta elaaaa
Oya we tafuta ela kwanza
 
Back
Top Bottom