Wanawake ni vipande vipande, wanangoja kukamilishwa...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Kwa mujibu wa kitabu cha Biblia, ni kuwa Mungu alichukua ubavu wa mwanaume aitwae Adam na kumtengeneza mwanamke aitwae Eva. Hiyo ni dhana tosha kwa mtu wa kawaida kuamini kuwa mwanamke aliumbwa akiwa kipande kidogo kilichotoka kwenye umbo kamilifu la mwanaume. Hiyo ni sababu ya kinasaba kuwa; mwanamke humpenda mwanaume katika ukamili wake kwanza na kumtii halafu ndipo anaweza kudai vitu vingine vya nje ya maumbile ya mwanaume. Kwa sababu mwanaume anajua kuwa mwanamke ni kipande tu au sehemu ndogo kutoka sehemu kubwa ya mwanaume hivyo humpenda vipande vipande na kumhurumia.

Na hivyo ndivyo mwanamke anavyojifahamu na kujitambua. Na mwanamke yeyote ambaye hajipendi vipande vipande hata wanawake wenzie lazima wamseme, wamponde na kumsimanga. Ushahidi uliopo, unaonesha kwamba mwanamke yuko tayari kupoteza pesa nyingi sana muda na rasilimali nyinginezo katika harakati za kuboresha au kukarabati sehemu au vipande vya mwili wake. Inaweza ikawa ni uso, nywele, kucha, nguo za kuonesha kitovu, matiti, kiuno nakadhalika…… Linapokuja suala la kutengeneza vipande huwa hawajali madhara au matokeo ya baadae ya kile wanachokifanya. Kwa mtazamo wa haraka haraka inaweza kudhaniwa kuwa wanatangaza bidhaa zao. La hasha. Ukweli ni kwamba kwa asili wao ni kipande tu cha ukamilifu wa utu, linapokuja suala la mwili, sio akili na hisia.

Katika uhusiano na jamii kwa ujumla mwanmke hupenda kusifiwa vipande vipande. Kwa mfano ukimwambia mwanamke kwa ujumla wake kuwa yeye ni mzuri na amependeza; haoneshi kufurahi, bali ataishia tu kusema ‘ahsante.' Lakini ukimwambia kuwa sehemu au kipande fulani cha mwili wake ni kizuri, mfano macho, nywele, kiuno, nk. Hapo atafurahi sana na kutoa kicheko cha aina fulani kuashiria kuwa sasa karidhika, hatimaye jamii imemtambua kuwa yeye ni mwenye kitu fulani bora kuliko wanawake wenzake.
 
Mtambuzi wewe ni mchambuzi pia! Ni kweli kuwa kwa baadhi ya imani na maandiko yanasema kuwa mwanamke ni sehemu ya mwanaume.

Ukiacha haya, nauungana na wewe ktk tafiti zako kwa asilimia 100 kuwa ukamilifu wa mwanamke upo kwenye mkusanyiko wa vipande vipande na ndiyo maana hupenda kusifiwa kwa kutajiwa sehemu tu za mwili wake. Niliwahi kusoma andiko fulani mahali fulani kuwa ukamilifu wa mwanamke uko kwa mumewe -That is, how mume anavyohandle vipande vipande vya mkewe kumfanya awe mkamilifu!
 
Mtambuzi :i beg to differ....Mungu aliona Adam hajakamilika ndio maana akachomoa kambavu kamoja ili kufanya msaidizi aliona Adam yu mpweke mno...sababu ya kuchomoa mbavu ni simple ili wafanane na ndio maana wanandoa wakikaa sana kwenye mahusiano mwishowe watu huona wamefanana ...so mwanamke ndiye anayemkamilisha mwanaume na c vipande kama unavyodai.
 
Kazi kweli kweli, mpambano maridadi kati ya KE na ME. Mpaka dunia inaisha naona watu watakuwa hawjapata majibu.
 
Mtambuzi :i beg to differ....Mungu aliona Adam hajakamilika ndio maana akachomoa kambavu kamoja ili kufanya msaidizi aliona Adam yu mpweke mno...sababu ya kuchomoa mbavu ni simple ili wafanane na ndio maana wanandoa wakikaa sana kwenye mahusiano mwishowe watu huona wamefanana ...so mwanamke ndiye anayemkamilisha mwanaume na c vipande kama unavyodai.
lolyz ... nakubali kutofautiana kimtazamo na yeyote yule...... Sitaki kuigeuza mada hii kuwa ya kidini, kwani itapoteza uhalisia......
Kuhusu wanandoa kufanana, naomba usome zaidi link hii hapa chini, niliwahi kuzungumzia jambo hilo wakati fulani.....

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/160484-mabinti-hawa-huolewa-na-baba-zao.html
 
Last edited by a moderator:
na ndiyo maana usipopata mwanaume mzuri hapa sizungumzii uzuri wa sura bali namaanisha real men nawe maisha yako hayatakuwa mazuri mana atashindwa kuunganisha vipande vilivyopo kwa mwanamke na kuwa mwanamke mkamilifu.
 
Mtambuzi :i beg to differ....Mungu aliona Adam hajakamilika ndio maana akachomoa kambavu kamoja ili kufanya msaidizi aliona Adam yu mpweke mno...sababu ya kuchomoa mbavu ni simple ili wafanane na ndio maana wanandoa wakikaa sana kwenye mahusiano mwishowe watu huona wamefanana ...so mwanamke ndiye anayemkamilisha mwanaume na c vipande kama unavyodai.

Wao wamekamilika bwana ndio maana siku hizi wanaoana wenyewe kwa wenyewe! They real dont need us at all; go guys Cameroon ameshawapa go ahead na wala si MUNGU.
 
Wao wamekamilika bwana ndio maana siku hizi wanaoana wenyewe kwa wenyewe! They real dont need us at all; go guys Cameroon ameshawapa go ahead na wala si MUNGU.

Kaunga mbona kama unatutusi tena wakaka? Ishu hapa siyo hoja ya ukamilifu wa wanaume na mambo ya ki-cameroon, uzi unazungumzia namna Mungu alivyoumba mwanamke na mwanaume na namna gani tafiti zinaonyesha jinsi ambavyo mwanamke anamtegemea mwanaume ktk ukamilifu wake! Mtambuzi amemention maeneo kadhaa ikiwemo namna ambavyo mwanamke anapenda kusifiwa kivipande vipande hoja ambayo ina ukweli ndani yake.

Tutake radhi aisee!
 
unajaribu kusema nini?
kuwa sisi ambao hatujirembi kucha na kadhalika ni nini?
BADILI TABIA ....Swala hapa si kujiremba, swala ni wanawake kutaka kusifiwa eneo ambalo wanahisi ni zuri na linavutia kuangaliwa, kinachofanyika ni kuboresha eneo hilo kwa kujiremba au kwa mavazi.............

Rejea makala yangu kuhusu jambo hilo kwa kubofya hapa chini:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/188688-wanaotembea-nusu-uchi-wana-lao-jambo%85%85%85.html
 
Last edited by a moderator:
Kaunga mbona kama unatutusi tena wakaka? Ishu hapa siyo hoja ya ukamilifu wa wanaume na mambo ya ki-cameroon, uzi unazungumzia namna Mungu alivyoumba mwanamke na mwanaume na namna gani tafiti zinaonyesha jinsi ambavyo mwanamke anamtegemea mwanaume ktk ukamilifu wake! Mtambuzi amemention maeneo kadhaa ikiwemo namna ambavyo mwanamke anapenda kusifiwa kivipande vipande hoja ambayo ina ukweli ndani yake.

Tutake radhi aisee!
Horse power huo ukweli ndio upi kwa mfano? kujipodoa ni jadi ya mwanamke maana aliumbwa awe kama ua la dunia...kama ni kusifiwa hakuna asiyependa sifa Mungu mwenyewe anapenda sifa sembuse mimi mwanamke? Ukweli utabakia kuwa MWANAUME HAWEZI KUKAMILIKA BILA MWANAMKE hiyo ni nature,creator angekuwa wa kike amini usiamin angetengenezwa ke(she) wa kwanza.we cant change nature
 
ni kweli hata biblia hutumia neno wao kuw a n dhaifu so wanahtaji msaada,tunaona wao pia huhitaji msaada zaid zaidi katk mazngra ya kila siku ni wagumu kutoa maamuz magumu hutegemea zaid wanaume kwl wao ni vpand .
 
Kaunga mbona kama unatutusi tena wakaka? Ishu hapa siyo hoja ya ukamilifu wa wanaume na mambo ya ki-cameroon, uzi unazungumzia namna Mungu alivyoumba mwanamke na mwanaume na namna gani tafiti zinaonyesha jinsi ambavyo mwanamke anamtegemea mwanaume ktk ukamilifu wake! Mtambuzi amemention maeneo kadhaa ikiwemo namna ambavyo mwanamke anapenda kusifiwa kivipande vipande hoja ambayo ina ukweli ndani yake.

Tutake radhi aisee!

Not this time broda; kama kupenda kusifiwa ndio ukipande pande then hata wanaume ni vipande pande pia.

na hata kama huyo ya uumbaji kuwa sijui ubavu ulinyofolewa kwa mwanamume (which can be just a metaphor), then mwanamume naye hajakamilika coz he is less one ubavu (kama ulinyofolewa just one).
 
Back
Top Bottom