Wanawake na msamiati mpya dhidi ya wanaume………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake na msamiati mpya dhidi ya wanaume………!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mtambuzi, Jul 16, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Saloon hizi zina mambo............................!

  Jana nilikwenda kunyoa hizi mvi zangu, nilikuta kuna wateja wananyolewa katika saloon hiyo, hivyo ilibidi nikae nje kusubiri huku nikisoma gazeti langu. Pembeni ya hiyo saloon kulikuwa na saloon nyingine ya kike na hapo nje walikaa kina dada wakisukana. Mara akapita kijana mmoja wa pale mtaani ambaye ninafahamiana naye, tulisalimiana kisha akapita na hamsini zake wale kina dada walianza kumjadili……………

  "Shoga unamuona yule kaka alivyo mzuri, yaani ana sura nzuri utadhani mwanamke." Alisema dada mmoja kati ya wale kina dada.

  "Mwenzangu hayo macho je? Mwanaume ana macho mazuri kama nini, na kifua chake mmekiona? Na huo ndio ugonjwa wangu….." Alidakia mwenzake.

  Mwenzao mmoja ambaye alikaa kimya akiwasikiliza alidakia...... "Ni mzuri ndio, lakini kizuri hakikikosi kasoro?"

  Wale wenzie wakamuuliza ana kasoro gani?

  "Hana kazi mwenzangu..........Yuko mtaani tu na anashinda vijiweni na jioni utamkuta uwanjani anajifanya kocha anafundisha mpira timu ya watoto wa hapa mtaani........... " Alijibu yule dada.

  "sasa hiyo ndio kasoro?" Mwenzake mmoja alidadisi........

  "Hee, mwanaume asiye na kazi atamtaka nani? Nani atamtaka mwanaume suruale........" Yule dada alijibu kisha wote wakacheka kwa pamoja kwa kebehi................

  Duh, mazungumzo yale yalinifanya nitafakari.... Hivi siku hizi mwanaume asiye na kazi huchukuliwa kwamba ana kasoro!

  Nilibaki mdomo wazi.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,111
  Likes Received: 3,031
  Trophy Points: 280
  mmmmh.....kusema kweli mna majina mengi.....
   
 3. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160

  Saloon hizi zina mambo............................

  “Shoga unamuona yule kaka alivyo mzuri, yaani ana sura nzuri utadhani mwanamke.” Alisema cacico -Hapa alimsema X HB wake

  “Mwenzangu hayo macho je? Mwanaume ana macho mazuri kama nini, na kifua chake mmekiona? Na huo ndio ugonjwa wangu…..” Alidakia BADILI TABIA

  @Remmy alidakia...... “Ni mzuri ndio, lakini kizuri hakikikosi kasoro?” Hapa wanamsema Bishanga )

  Wale wenzie wakamuuliza ana kasoro gani?

  “Hana kazi mwenzangu..........Yuko mtaani tu na anashinda vijiweni na jioni utamkuta uwanjani anajifanya kocha anafundisha mpira timu ya watoto wa hapa mtaani........... “ Alijibu yule dada.

  “sasa hiyo ndio kasoro?” Yummy alidadisi........

  “Hee, mwanaume asiye na kazi atamtaka nani? Nani atamtaka mwanaume suruale........” sweetlady alijibu kisha wote wakacheka kwa pamoja kwa kebehi................

  Duh, mazungumzo yale yalinifanya nitafakari.... Hivi siku hizi mwanaume asiye na kazi huchukuliwa kwamba ana kasoro!

  Nilibaki mdomo wazi.[/QUOTE]
  Lol mi sina neno
  Nimeamini wanamke Umbea
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Sasa kukosa kazi ndio iitwe kasoro!
  Mimi najua mtu kuwa na kasoro ni kuwa na upungufu wa viungo...........
  Mna visa nyie
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama ulikuwepo, maana hiyo timu uliyoishirikisha katika huu mjadala, kama kweli vileeee......................LOL
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika
   
 7. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hahahaaa hiyo timu iko nusu lol
  Ungemkuta Zinduna hapo na Erotica ndio ungeshangaa maaana wangeanza hadi kuchambua wanavyokuwa chumbani na haoo wenye vifua lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kama huna kazi mkuu, basi wewe una kasoro..................!
   
 9. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Heheheee umeibuka bro?
  Karibu sana
   
 10. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hahahaaaa na wanajua kuchambua aisee lol
  Kumbe ukiwa na kazi unawadaka kirahisi lol
  Sasa Bishanga muuzandizi inakuwaje?
  Ile sio kazi au?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kujua vifua vya wanawake basi jibanze kwenye Saloon.
  Nasikia walituma maombi ya kutaka kuwekewa jukwaa lao la Urembo, Mods wakashitukia litakuwa ni la kuchapa umbea wakawatolea nje......... walikasirikaje!
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ngoja waje wenyewe, utasikia watakavyosema................
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Inawezekana hii imemgusa Kaizer...........
  Nahisi na yeye hana kazi, anaugulia kuambiwa ana kasoro...........LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hahahaaaa na watutolee maumbea yao lol
  Salamu hizi na ujumbe uwafikie wale vinara wa Umbea BADILI TABIA Yummy cacico Remmy sweetlady Yummy Catherine Erotica na wenzao wanaokaaga salun za JF
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hahahaa huyu anayo ndio maana CUTE na Catherine hawataki kumwachia hata sekunde lol utadhani wamelogwa nae kumbe ni kikazi alichonacho
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hebu ngoja niende kwenye lile jukwaa la matangazo ya kazi niangelie ni wanaume wangapi wanaotafuta kazi kisha niunganishe dot (Wana kasoro)
   
 17. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hehehee watakuwa wakali hao lol
  Ngoja wanamalizia kupika watakuja muda si mrefu
   
 18. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Teh hivi lile jukwaa huwa lina Mod?
  Lol kama yuo muulize yeye atakusaidia kukupa list haraka
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nikiwajua nitawaanika hapa kwamba wana kasoro...................................

  Kwa mujibu wa dada zetu
   
Loading...