Bob12
JF-Expert Member
- Feb 27, 2017
- 11,422
- 58,788
Habari wana jamvi,
Kuna watu wanaamini unaweza ukamtumia mwanamke Milion 1 kushinda vita ya dunia, ikiaminika kwamba mwanamke ana mbinu za ajabu sana ktk kufanikisha jambo.
Kuna vijistori nilivyobahatika kuvisoma kama Samson mwanaume wa shoka mwenye miraba minne na aliyesumbua sana maelfu ya watu katika vita lakini maadui wakamtumia mwanamke wa kawaida sana kiumbo lakini mwenye mbinu za ushawishi zilizotumika kumfanya Samson kutaja asili ya nguvu zake.
Sulemani alikuwa mcha Mungu na mwenye wingi wa hekima lakini hekima zake hazikufua dafu kwa mwanamke mpaka mwanamke anamfanya sulemani kuabudu miungu.
Ukija kwenye maisha halisi hata mtoto anaposhindwa kuzungumza na baba kwa hitaji flani, yule mtoto akimtumia mama tu ujue game imeisha.
Mimi nakumbuka enzi za utoto nilimuudhi baba mpk akaniambia hakuna kula msosi wa usiku ila ilipofika usiku mama akanipa ndoo nikachote maji nje ila akaniita kando akaniambia ndani ya ndoo kuna sahani ya chakula, kijana nikapiga msosi kwa mbinu ya mama.
Hizi mbinu za ushindi najiuliza wanawake mnazipata wapi hata sipati jibu