Magoya2000
JF-Expert Member
- May 7, 2017
- 641
- 1,265
Habari wana jamii! Kwanza poleni kwa msiba wa Mzee Kingunge. Niingie kwenye maada. Katika pita pita kwenye familia nyingi nimegundua kama familia (mke, mme) wakiwa na gari moja basi hilo gari mara nyingi litakuwa linatumiwa na mke. Wanaume wengi hawajali hivyo yeye ataamua kupata daladala. Shida nyingine inayoonekana kwenye jamii wanawake wengi wakiwa wanamiliki magari wanakuwa jeuri na viburi hawana heshima kwa waume zao. Mfano mzuri nilishuhudia jamaa yangu ndoa yao ilivunjika baada ya mkewe kununua gari tu. Ijapokuwa jamaa nae ana gari lake lakini mwanamke alianza jeuri. Je mchawi wa wanawake ni magari? Karibuni tujadili.